Zielewe kazi za Usalama wa Taifa (TISS) na mipaka yake

Shukrani sana ,hakika umetufungua macho sana ,sina shaka maana Late Membe naye alikuwa mtu wa KITENGO hope ulipata madini mengi kutoka kwake.

Ni wazi SHUSHUSHU hawezi kujitangaza akiwa bar ,hao wanaojitangaza ni wehu tu wachukue mabar medi.

DAB alikuwa anaongoza GENGE la UHALIFU lakini walikuwa siyo "TEETH".
Teeth, ni Nani
 
Nimependa jibu lako japo Kuna maandishi kama hujawahi kufanya kazi serikalini, kuwa mchambuzi ,mshauri wa maswala ya kazi ya Marehemu pamoja na viongozi kadhaa aliofanya nao kazi pamoja ,yameniongezea maswali zaidi ila acha maswali haya nijijibu mwenyewe inatosha🙏🙏
Usibaki na maswali uliza, usipouliza akili ina kawaida ya kujitungia jibu jepesi kwenye masuala magumu.

Sijawahi kufanyakazi serikalini, kaka yangu alinisomesha hadi master's degree ili nimfanyie kazi yeye tu, wakati mwingine kazi za wenzake alizozileta kwangu. Nilipokuwa nafanyakazi nje ya nchi kama mtafiti na mshauri bado nilikuwa nafanyakazi za kaka yangu pia. Kwa maana nyingine mimi nilikuwa MSUKULE wa kazi nyingi za marehemu kaka yangu hadi ulipomkuta umauti. Sasa nimejitokeza tu kuelimisha kadri niwezavyo, sifungwi na kiapo chochote cha kazi yeyote.
 
Wakati mmoja nikakutana na Aunt yangu (mke wa baba yangu mdogo kabisa) kwenye daladala.... namsalimia naona kimya, mpaka nikaona niuchune tu. Nimerudi home namwambia mzee, akasema siku nyingine ukiona hajakuchangamkia muache tu. Nilikuja kujua baadae sana kumbe ni mfanyakazi wa idara, na siku ile alikuwa kazini anafuatilia drug dealers; baadae ndio nikaja nikajua pia kumbe baba mdogo na yeye ni nyoka 🤣 🤣 🤣

Those days watu walikuwa na ethics. Hata wakiongea, sauti zao ni za chini sana, akiwa anaongea na wewe meza hii, wa meza ya pili hawezi kusikia. Fast forward, mke wa baba yangu mkubwa akafariki. Loh, siku ya msiba namuona, former director mmoja msibani, 😳😳😳 kumbe yule mzee nae alikuwa nyoka tangu mwaka 1965 huko. That was the first time naongea na former director, nae haiba yake ilikuwa vile vile, very quite, very low voice; amechill tu sehemu kama sio yeye.

Anyways, mambo yanabadilika; siku hizi vijana wako nje nje... kidogo tu kashatoa mashine!
 
Vijana bana! 😂 hapo usikute anajidanganya wale wanaokuwaga kwenye misafar wanafaidi sanaaaa! Au wana mapesa sanaaaa! Au kuna watu anataka awavimbie, awalipe visasi au wamuogope... Wacha upumbavu! Hao watu ni Choosen from god!

Haipatikani hiyo status kizembezembe! Concentrate na mambo mengine
Pia hawaelewi kuwa hakuna kazi isiyo na misukosuko na frustration. Kitu chochote kikishaitwa "kazi", ujue ipo siku kitakukera tu 🤣 🤣 🤣
 
Sw
Membe S K Front companies, NGO's na Balozi zimekuwa zikiratibu Mambo ya ajabu kuliharibu taifa mbona watu makin huwa hawastuki wala kunusa Hadi tatizo litokee ?
Swali zuri, kama nilivyosema kwenye posts zangu za awali kwamba sikukusudia kufanya uchambuzi wa ufanisi wa TISS kwa namna yeyote badala yake kuweka wazi kazi na mipaka yake.

Nitoe angalizo tu kwamba mlaji au mtumiaji wa moja kwa moja wa shughuli au information za TISS ni rais na TISS yenyewe Tu. Hivyo umma hauna kipimo cha moja kwa moja cha ufanisi wa idara hii. Na uchambuzi wowote wa umma katika kupima ufanisi wa TISS paisipo "tukio la kitaifa la kiusalama" hautakuwa na maana wala mashiko.
 
ZIELEWE KAZI YA USALAMA WA TAIFA (TISS) NA MIPAKA YAKE

Leo tuongelee TISS au USHUSHU au UNYOKA au IDARA au KITENGO. Kwasababu uelewa mdogo kwa idara hii na kazi zake miongoni mwa wananchi unafanya watu wengi wakose amani wanapokuwa na watu wanaowahisi ni mashushushu, na wakati mwingine watapeliwe na wajanja wanaojifanya watu wa idara.

IDARA YA USALAMA WA TAIFA
Idara ya usalama ni idara maalum chini ya ofisi ya rais. Naam, yaani ukiongelea ushushushu unaongelea idara kubwa ndani ya ikulu yenye mkurugenzi mkuu (Director General of Intelligence Services (DGIS)) na wakurugezi kadhaa wa vitengo mbalimbali (directorates directors) ambao nchi nyingine wanaitwa chiefs, mfano chief wa operesheni au chief wa wafanyakazi na mafunzo. Kutegemea na namna idara ilivyojipanga kunakuwa na ofisi za idara hii wilayani na mikoani.

HISTORIA FUPI YA USALAMA WA TAIFA
Kwenye nchi mbalimbali idara za usalama zilianza kwa kasi nyakati za vita baridi (Cold War) kati ya nchi za Soviet na NATO. Nchi za NATO na washabiki wake wakihofia mashushu wa Soviet kupandikizwa nchini kwao na kushawishi watu kudai sera za kikomunist huku nchi za Soviet na washirika wake zikihofia mashushu wa nchi za NATO na washirika wake kuingia na kushawishi watu wadai siasa za kibepari. Hivyo kama umenifuata vizuri hapa utajuwa kwamba idara ya usalama lengo lake la awali lilikuwa kulinda usalama wa dola dhidi ya adui wa nje na ndani.

KAZI ZA IDARA NA MIPAKA YAKE
Sasa vita baridi vimeisha tatizo nini? Matizo yanayohatarisha usalama wa taifa bado yapo tena mapya na makubwa tu: serikali kupinduliwa, ugaidi, mauaji ya kimbari ya kisiasa (genocide), ukiukwaji wa mikataba ya umoja wa mataifa kama vile madawa ya kulevya, silaha za maangamizi nk. Kwakuwa haya yote yanaweza kutekelezwa na watu wenye maarifa ya juu, akili kubwa, fedha na vitendea kazi vizuri; idara za usalama zinahitaji mfumo imara wa kukusanya taarifa au viashiria kila siku ya Mungu ili kuvichakata, kuvitafsiri, kutunza, na kutolea maamuzi kwa wakati. Mfumo huu hapa Tz tumeuremba kwa jina la kimombo: Tanzania Intelligence and Security Service (TISS), nchi nyingine zinaita Secret Services, nyingine Internal Security and Intelligence nk.

Kwa mantiki hiyo TISS imepewa majukumu makubwa matatu. Mosi, kukusanya taarifa za kintelijensia zihusuzo usalamawa taifa, kuzichakata, kuzitafsiri, kuzitunza, kushauri, na kuziwashirisha kwenye mamlaka husika kwa ajili ya maamuzi. Pili, kumtaarifu rais juu ya uwapo wa viashiria vya uhujumu, uwapo wa mashushu wa nje ya nchi ndani ya Tz au vibaraka wa wavunjifu wa amani na usalama ndani ya Tz na hivyo kupata baraka ya rais kuweka ufuatiliaji wa mambo hayo kwa wakati. Tatu, kushirikiana na wizara na taasisi nyingine za serikali nchini katika kazi zote zihusuzo idara na pia kushirikiana na idara za inchi nyingine kadri ipasavyo katika kutekeleza majukumu yake. Nne, kumhoji mtu au kikundi chochote cha watu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola pamoja na wizara husika.

MPANGO KAZI WA IDARA KWA KAWAIDA NA WAHUSIKA
Kwa kawaida kila siku ya kazi na siku za tukio maalum saa nne Asubuhi usalama wa taifa chini ya DGIS na mchambuzi wa taarifa zakiintelijensia (national intelligence analyst) inafanya mkutano unaoitwa DEBRIEFING kwa mkuu wa nchi. Kwenye mkutano huu mkuu wa nchi anapewa taarifa zote mpya zenye viashiria chanya (credible threats) na taarifa za ufuatiliaji unaoendelea pamoja na changamoto. Baada ya kupata taarifa kinachofuata ni uchambuzi wa taarifa, kutoa maazimio, kumshauri rais na kuomba ridhaa yake katika kutekelezaji.

Utaalamu wa ofisi ya usalama upo kichwani mwa mtu niliyemtaja hapo juu: NATIONAL INTELLIGENCE ANALYST. Wala sio DGIS kama wengi tunavyodhani, DGIS ni bosi tu anayeongoza ofisi na ndio maana akiteuliwa anatangazwa mchana kweupe, na wala haitaji kwenda kusoma huko SCOTLAND YARD tulikozoea kusikia wanakwenda kusomea ushushushu. Nimeona watu wakihoji kwanini ma DGIS wanateuliwa na kutenguliwa hadi kufikia 4 tangu mama Samia ashike madaraka. Niwatoe hofu kwamba tunayetakiwa kushangaa akitenguliwa ni mtu ambaye hatuwezi kumjua kwa urahisi: NATIONAL INTELLIGENCE ANALYST. Mtu huyu akiteuliwa umma haujui wala akitenguliwa haujui. Lakini huyo ndio mtu anayetakiwa awe maili million kadhaa kabla ya wabaya wanaoweza kuhatarisha usalama wa taifa. Mara nyingi anafanyakazi kwa kushirikiana na watu kadhaa.

MIPAKA NA MIIKO YA WATU WA USALAMA WA TAIFA
Pigia mstari point inayofuata: SHUSHUSHU WA TISS HARUHUSIWI KUFANYAKAZI YA KUSIMAMIA SHERIA KAMA ILIVYO KWA POLISI. Pigia tena mstari point inayofuata: SHUSHUSHU WA TISS HARUHUSIWI KUMFUATILIA MTU KWASABABU MTU HUYO ANAJIHUSISHA NA MAANDAMANO YA KIKATIBA AU ANASHIRIKI AU KURATIBU MALALAMIKO DHIDI YA SERIKALI KWA NJIA ZINAZOFUATA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI.

Mfanyakazi wa TISS ana miiko mitatu mikubwa anayotakiwa kuizingatia awapo kazini. (i) kutotangaza kazi yake kwa njia yeyote isipokuwa kwa wanafamilia wakaribu tu. Mkurugenzi mkuu peke yake ndio anayetambulika tangu siku anaapishwa; (ii) kutunza siri za kazi zake zote. Yaani mlaji/mtumiaji wa taarifa za shushu ni rais na idara ya usalama tu, sio umma; (iii) kutotangaza chanzo au vyanzo vya taarifa au kumtaja raia aliyesaidia kupata taarifa za kintelijensia.

MASWALI NA MAJIBU
Nadhani baada ya kusoma bandiko hili utajiuliza TAKUKURU NI USALAMA WA TAIFA? ASKARI KANZU NI USALAMA WA TAIFA? Je wale vijana wanaokesha Best Bite, Break point, Kinondoni Biafara na Mlimani city bila kuwa na kazi maalum nao ni usalama wa taifa? Je wale tunaokunywa nao kisha wakalewa na kujitangaza watu wa idara nao ni usalama? Kama wanajitaganza USALAMA HUU KWELI UPO SALAMA?

Niseme kwa kunong'ona..!! Kimsingi kila wizara, kila shirika, kila kampuni kubwa, kila mkoa, kila wilaya, na kila kwenye shughuli kubwa ya kiuchumi tegemea kwa 90% uwapo wa watu wa usalama. Sasa wapo watu wa usalama wa ngazi mbalimbali; wapo wakudumu kwenye vituo vyao, wapo wafuatiliaji wa tukio/mtu, wapo wasaidizi walioajiriwa kwa kazi maalum ambao yawezekana wala hawajui wanafanyakazi ya idara na wapo wanaofanya ushushushu kwa mujibu wa kazi zao, mfano aliyekuwa kwenye kikosi cha usalama wa kiongozi wa juu Dar akipangiwa kazi nyingine Mufindi ujuwe amehama nyani na msitu wake.

Yote kwa yote huwezi kumjuwa mtu wa usalama aliyeiva kwenye kazi yake na anayefuata kanuni ya kazi yake. Unaweza kuhisi tu. Mtu wa usalama akijitagaza mtilie shaka hapo hapo kwasababu tayari anauweka usalama wa taifa kwenye hatari na yeye mwenyewe pia. Huyo anaweza kuwa MWEHU wa usalama wake mwenyewe. Muhimu usimwogope kama wewe ni raia mwema maana yeye analinda dola, na yeye sio polisi.

SEMA NIMESEMA

Membe S K
Mtama, Rondo Chiponda
Lindi Tanzania
Tel: +255689463664
email: smembe426@gmail.com
Hongera
Umejitahidi kuandika mengi but ulichoandika hapa it's too general ambacho hata mtoto wa form 4 anakijua kama ni mtu wa movies na hadithi.

Tukitaka tuzipate hadithi za hawa jamaa zenyewe tena za Tanzania kwamba wao ni nani na wanafanya mission gani na mission gani walishawahi zifanya na walizifanyaje vipi ndo watu wataelewa lakini katu mtu wa kawaida hawezi kukwambia what they do inside

All in all umejitahidi
 
Wakikuambia wanachofanya na namna wanavyofanya basi juwa wewe ni (a) mmoja wao, (b) rais wa nchi au boss wao (c) wamefanya editing wakakufungashia uongo uutumie kutengenezea movie pasipo kukupa mbinu zao halisi au (d) anayekuambia alishaacha hiyo kazi na anakupa product ambayo iko expired. Ukiwa nje unachoweza kujua ni hiki unachosema hata mtu wa form four anaweza kukijuwa.

When you know your limit then you know.
 
Sw

Swali zuri, kama nilivyosema kwenye posts zangu za awali kwamba sikukusudia kufanya uchambuzi wa ufanisi wa TISS kwa namna yeyote badala yake kuweka wazi kazi na mipaka yake.

Nitoe angalizo tu kwamba mlaji au mtumiaji wa moja kwa moja wa shughuli au information za TISS ni rais na TISS yenyewe Tu. Hivyo umma hauna kipimo cha moja kwa moja cha ufanisi wa idara hii. Na uchambuzi wowote wa umma katika kupima ufanisi wa TISS paisipo "tukio la kitaifa la kiusalama" hautakuwa na maana wala mashiko.
Ndiyo,
Membe S K naona unazingatia Security Clearance.
Nimekusoma.
 
Usibaki na maswali uliza, usipouliza akili ina kawaida ya kujitungia jibu jepesi kwenye masuala magumu.

Sijawahi kufanyakazi serikalini, kaka yangu alinisomesha hadi master's degree ili nimfanyie kazi yeye tu, wakati mwingine kazi za wenzake alizozileta kwangu. Nilipokuwa nafanyakazi nje ya nchi kama mtafiti na mshauri bado nilikuwa nafanyakazi za kaka yangu pia. Kwa maana nyingine mimi nilikuwa MSUKULE wa kazi nyingi za marehemu kaka yangu hadi ulipomkuta umauti. Sasa nimejitokeza tu kuelimisha kadri niwezavyo, sifungwi na kiapo chochote cha kazi yeyote.
Hapo uliposema Ulikuwa MSUKULE wake nafikiri ushamaliza majibu ya maswali yangu yote hasa kwakuwa darasa ulilotoa juu pia linaeleza namna za ufanyaji kazi wao Kwa ujumla nimekuelewa vzr kwasasa sina swali Tena nimekuelewa vyema🙏
 
Teeth, ni Nani
Hiyo ni Jargon tu , sio kila unapotaka kusema Ng'ombe lazima utumie neno ng'ombe au cow muda mwngne unaweza sema MOO wenye Akili wanaelewa unamaanisha nn

Hata maji yakizidi unga unajitetea Kwa kutumia maana ya neno , kwahyo ww utakayetafsir Teeth ni Meno yupo atakayetafsri Kwa kuelewa hoja iliyopo juu.
 
Umesema kwenye majukumu ya TISS ni kuripoti, juu ya matishio ya usalama ya ndani na nje!
Swali langu je TISS, hawawezi kuwajulisha serikali juu ya mikataba mibovu wanayoingia? Au Siyo majukumu yake?
Pili, Kama wanafanya kazi kwa maslahi ya Serikali na Siyo nchi ni hatari Sana.
Duh umeuliza kwa hasira na uchungu inavyoonyesha.

Nasikitika TISS hawana jukumu la moja kwa moja kwenye ubovu wa mikataba. Isipokuwa kama mikataba hiyo ina vipengere vinavyo compromise usalama wa taifa basi idara ya usalama itamulika mkataba huo, kutoa maazimio na kushauri. Lakini kumbuka ushauri wa TISS sio AMRI.
 
Ilikuwa ni kazi ya ndoto yangu, na ndoto ikaishia ndotoni
ZIELEWE KAZI YA USALAMA WA TAIFA (TISS) NA MIPAKA YAKE

Leo tuongelee TISS au USHUSHU au UNYOKA au IDARA au KITENGO. Kwasababu uelewa mdogo kwa idara hii na kazi zake miongoni mwa wananchi unafanya watu wengi wakose amani wanapokuwa na watu wanaowahisi ni mashushushu, na wakati mwingine watapeliwe na wajanja wanaojifanya watu wa idara.

IDARA YA USALAMA WA TAIFA
Idara ya usalama ni idara maalum chini ya ofisi ya rais. Naam, yaani ukiongelea ushushushu unaongelea idara kubwa ndani ya ikulu yenye mkurugenzi mkuu (Director General of Intelligence Services (DGIS)) na wakurugezi kadhaa wa vitengo mbalimbali (directorates directors) ambao nchi nyingine wanaitwa chiefs, mfano chief wa operesheni au chief wa wafanyakazi na mafunzo. Kutegemea na namna idara ilivyojipanga kunakuwa na ofisi za idara hii wilayani na mikoani.

HISTORIA FUPI YA USALAMA WA TAIFA
Kwenye nchi mbalimbali idara za usalama zilianza kwa kasi nyakati za vita baridi (Cold War) kati ya nchi za Soviet na NATO. Nchi za NATO na washabiki wake wakihofia mashushu wa Soviet kupandikizwa nchini kwao na kushawishi watu kudai sera za kikomunist huku nchi za Soviet na washirika wake zikihofia mashushu wa nchi za NATO na washirika wake kuingia na kushawishi watu wadai siasa za kibepari. Hivyo kama umenifuata vizuri hapa utajuwa kwamba idara ya usalama lengo lake la awali lilikuwa kulinda usalama wa dola dhidi ya adui wa nje na ndani.

KAZI ZA IDARA NA MIPAKA YAKE
Sasa vita baridi vimeisha tatizo nini? Matizo yanayohatarisha usalama wa taifa bado yapo tena mapya na makubwa tu: serikali kupinduliwa, ugaidi, mauaji ya kimbari ya kisiasa (genocide), ukiukwaji wa mikataba ya umoja wa mataifa kama vile madawa ya kulevya, silaha za maangamizi nk. Kwakuwa haya yote yanaweza kutekelezwa na watu wenye maarifa ya juu, akili kubwa, fedha na vitendea kazi vizuri; idara za usalama zinahitaji mfumo imara wa kukusanya taarifa au viashiria kila siku ya Mungu ili kuvichakata, kuvitafsiri, kutunza, na kutolea maamuzi kwa wakati. Mfumo huu hapa Tz tumeuremba kwa jina la kimombo: Tanzania Intelligence and Security Service (TISS), nchi nyingine zinaita Secret Services, nyingine Internal Security and Intelligence nk.

Kwa mantiki hiyo TISS imepewa majukumu makubwa matatu. Mosi, kukusanya taarifa za kintelijensia zihusuzo usalamawa taifa, kuzichakata, kuzitafsiri, kuzitunza, kushauri, na kuziwashirisha kwenye mamlaka husika kwa ajili ya maamuzi. Pili, kumtaarifu rais juu ya uwapo wa viashiria vya uhujumu, uwapo wa mashushu wa nje ya nchi ndani ya Tz au vibaraka wa wavunjifu wa amani na usalama ndani ya Tz na hivyo kupata baraka ya rais kuweka ufuatiliaji wa mambo hayo kwa wakati. Tatu, kushirikiana na wizara na taasisi nyingine za serikali nchini katika kazi zote zihusuzo idara na pia kushirikiana na idara za inchi nyingine kadri ipasavyo katika kutekeleza majukumu yake. Nne, kumhoji mtu au kikundi chochote cha watu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola pamoja na wizara husika.

MPANGO KAZI WA IDARA KWA KAWAIDA NA WAHUSIKA
Kwa kawaida kila siku ya kazi na siku za tukio maalum saa nne Asubuhi usalama wa taifa chini ya DGIS na mchambuzi wa taarifa zakiintelijensia (national intelligence analyst) inafanya mkutano unaoitwa DEBRIEFING kwa mkuu wa nchi. Kwenye mkutano huu mkuu wa nchi anapewa taarifa zote mpya zenye viashiria chanya (credible threats) na taarifa za ufuatiliaji unaoendelea pamoja na changamoto. Baada ya kupata taarifa kinachofuata ni uchambuzi wa taarifa, kutoa maazimio, kumshauri rais na kuomba ridhaa yake katika kutekelezaji.

Utaalamu wa ofisi ya usalama upo kichwani mwa mtu niliyemtaja hapo juu: NATIONAL INTELLIGENCE ANALYST. Wala sio DGIS kama wengi tunavyodhani, DGIS ni bosi tu anayeongoza ofisi na ndio maana akiteuliwa anatangazwa mchana kweupe, na wala haitaji kwenda kusoma huko SCOTLAND YARD tulikozoea kusikia wanakwenda kusomea ushushushu. Nimeona watu wakihoji kwanini ma DGIS wanateuliwa na kutenguliwa hadi kufikia 4 tangu mama Samia ashike madaraka. Niwatoe hofu kwamba tunayetakiwa kushangaa akitenguliwa ni mtu ambaye hatuwezi kumjua kwa urahisi: NATIONAL INTELLIGENCE ANALYST. Mtu huyu akiteuliwa umma haujui wala akitenguliwa haujui. Lakini huyo ndio mtu anayetakiwa awe maili million kadhaa kabla ya wabaya wanaoweza kuhatarisha usalama wa taifa. Mara nyingi anafanyakazi kwa kushirikiana na watu kadhaa.

MIPAKA NA MIIKO YA WATU WA USALAMA WA TAIFA
Pigia mstari point inayofuata: SHUSHUSHU WA TISS HARUHUSIWI KUFANYAKAZI YA KUSIMAMIA SHERIA KAMA ILIVYO KWA POLISI. Pigia tena mstari point inayofuata: SHUSHUSHU WA TISS HARUHUSIWI KUMFUATILIA MTU KWASABABU MTU HUYO ANAJIHUSISHA NA MAANDAMANO YA KIKATIBA AU ANASHIRIKI AU KURATIBU MALALAMIKO DHIDI YA SERIKALI KWA NJIA ZINAZOFUATA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI.

Mfanyakazi wa TISS ana miiko mitatu mikubwa anayotakiwa kuizingatia awapo kazini. (i) kutotangaza kazi yake kwa njia yeyote isipokuwa kwa wanafamilia wakaribu tu. Mkurugenzi mkuu peke yake ndio anayetambulika tangu siku anaapishwa; (ii) kutunza siri za kazi zake zote. Yaani mlaji/mtumiaji wa taarifa za shushu ni rais na idara ya usalama tu, sio umma; (iii) kutotangaza chanzo au vyanzo vya taarifa au kumtaja raia aliyesaidia kupata taarifa za kintelijensia.

MASWALI NA MAJIBU
Nadhani baada ya kusoma bandiko hili utajiuliza TAKUKURU NI USALAMA WA TAIFA? ASKARI KANZU NI USALAMA WA TAIFA? Je wale vijana wanaokesha Best Bite, Break point, Kinondoni Biafara na Mlimani city bila kuwa na kazi maalum nao ni usalama wa taifa? Je wale tunaokunywa nao kisha wakalewa na kujitangaza watu wa idara nao ni usalama? Kama wanajitaganza USALAMA HUU KWELI UPO SALAMA?

Niseme kwa kunong'ona..!! Kimsingi kila wizara, kila shirika, kila kampuni kubwa, kila mkoa, kila wilaya, na kila kwenye shughuli kubwa ya kiuchumi tegemea kwa 90% uwapo wa watu wa usalama. Sasa wapo watu wa usalama wa ngazi mbalimbali; wapo wakudumu kwenye vituo vyao, wapo wafuatiliaji wa tukio/mtu, wapo wasaidizi walioajiriwa kwa kazi maalum ambao yawezekana wala hawajui wanafanyakazi ya idara na wapo wanaofanya ushushushu kwa mujibu wa kazi zao, mfano aliyekuwa kwenye kikosi cha usalama wa kiongozi wa juu Dar akipangiwa kazi nyingine Mufindi ujuwe amehama nyani na msitu wake.

Yote kwa yote huwezi kumjuwa mtu wa usalama aliyeiva kwenye kazi yake na anayefuata kanuni ya kazi yake. Unaweza kuhisi tu. Mtu wa usalama akijitagaza mtilie shaka hapo hapo kwasababu tayari anauweka usalama wa taifa kwenye hatari na yeye mwenyewe pia. Huyo anaweza kuwa MWEHU wa usalama wake mwenyewe. Muhimu usimwogope kama wewe ni raia mwema maana yeye analinda dola, na yeye sio polisi.

SEMA NIMESEMA

Membe S K
Mtama, Rondo Chiponda
Lindi Tanzania
Tel: +255689463664
email: smembe426@gmail.com
zi
 
Back
Top Bottom