Zielewe kazi za Usalama wa Taifa (TISS) na mipaka yake

Zielewe kazi za Usalama wa Taifa (TISS) na mipaka yake

pesa zinatoka sana nchi inaliwaliwa we mpaka tunakuja kusikia watu wameweka pesa kwenye magunia hiyo idara inafanya nini..?
mara EPA mara escrow, mzee magu aliwatumia vilivyo wakati wake maana hii dhana ya wawekezaji ni nzuri lakini deep down ni tunanyonywa sana!.. hiyo idara kazi yake nini na makampuni yakigeni yaliyowekeza yanaleta janjajanja..??

kama kuna vitu wanashindwa kuitaka serikali ifanye basi wajue hawana nguvu! mfano wakitaka sheria fulani ipitishwe bungeni ili kuondoa changamoto ya wao kufanya kazi nakulinda masirahi ya taifa!,wakishindwa kufanya hivyo basi wao si lolote!!.
Nitaendelea kuwalaumu kwasababu si kwamba sikubalianinao ila nahitaji waichape kazi yao vyema natuone matokeo,maana ukisema wanaleta amani ndio amani ni muhimu lakini baada ya amani maisha mengine yanatakiwa yaendelee,amani ambayo haitakuletea tija ni sawa na uchawi tu!.

kama pia wanashindwa kuingilia uchumi wajitafakari uchumi ni jambo nyeti sana kwenye nchi yoyote,aibu kwa Tanzania kunyanyasika kwaajili ya sukari aibu sana!,halafu vipi hamuioni hiyo dollar inavyorarua pesa yetu..??
najua hakuna nchi isiyokosa changamoto lkn kuna changamoto ni changamtoto! miaka 60 nakenda ya uhuru uchumi wetu hautakiwi kuwa hapa!.
sasa someni halafu mkalale tena usingizi wa pono!
Kazi yao ni kutoa taarifa, watekelezaji ni wengine. Ni kama CAG
 
Hao wanaitwa PSU kimombo ni presidential security unit. Kazi yao ni kumlinda mkuu wa nchi dhidi ya shambulio la kimwili, ni kama walinzi wake. TISS wao kazi yao ni kulinda dola kwa taarifa. Ukifanya maandamano ukafika ikulu bila utaratibu utapambana na PSU, TISS hawahusiki moja kwa moja hapo.
Unatenganishaje psu na tiss?psu ni sehemu ya tiss hapo ni mgawanyo wa majukumu ndani ya tiss kupitia vitengo mbalimbali ikiwemo hili la psu

Hakuna namna yoyote ya kumtoa psu ndani ya tiss
 
Mkuu mleta mada, bandiko informative kama hili halafu unashindwa ku-cite legal authority yoyote ili kusupport na kuverify narration yako?!

Anyway, ngoja nimuite mkuu Eagle girl aje hapa kusabahi wananzengo. 😎

-Kaveli-
Amezungumza kwa mitazamo binafs ila title na maelezo naona vinapishana inawezekana akawa mtoto wa afisa au wale vijana waliokulia magorofani makumbusho au kuungaunga story za mtandaoni ambapo wengi tu
 
Kila mmoja ana maana yake, kwamimi "shushushu" ni mwenyewe UWT na "informer" ni mtoa habari kwa mashushushu.

Informer anaweza kuwa anatowa habari bila kujuwa anayempa ni UWT.
Mi nijuavyo hao kenge wote ni kitu au mtu mmoja tofaut ni lugha tu yaani shushishi ndo informer hawa kimtaan pia wanaitwa vipenyo sijui hawa ni wakusanya taarifa na wanazipeleka kwa kit3ngo husika zikachakatwe tayar kwa matumizi
 
Unatenganishaje psu na tiss?psu ni sehemu ya tiss hapo ni mgawanyo wa majukumu ndani ya tiss kupitia vitengo mbalimbali ikiwemo hili la psu

Hakuna namna yoyote ya kumtoa psu ndani ya tiss
Mkuu hapa umechanganya mambo ya kiufundi. Usalama wa DOLA na usalama wa RAIS. Usalama wa DOLA ndio intelligence ya nchi (TISS) iliyopo chini ofisi ya DOLA, yaani Ikulu. Usalama wa RAIS ndio PSU ambayo kazi yake ni kuhakikisha rais hashambuliwi kimwili. Rais anapanga mkutano Mwembe yanga kwa mfano, TISS watakuwa wameshamaliza kazi yao hata kabla mkutano haujatangazwa. Wao kazi yao ni kukusanya habari za kintelijensia, kuzichakata, kushauri na kutekeleza. PSU ndio watavamia Mwembe yanga baadae kabla ya mkutano wakiwa na mbwa wa kunusa milipuko na kuliweka eneo la mkutano salama kwa Rais. Hapo tena sio suala la Inteligence bali ni usalama wa rais.

Tatizo wananchi wengi tunadhani kila anayefanyakazi ofisi ya rais ni TISS na kwamba kila mpelelezi ni TISS. Mpishi wa rais tunadhani TISS, anayetumwa akanunue dafu la rais tunadhani TISS, anayemshonea rais nguo tunadhani TISS. Mwisho wa siku tunashusha hadhi na usomi wa taasisi kubwa nchini inayolinda usalama wa dola yetu: TISS.
 
MI ipo ndani ya wigo wa TISS
Hapana hicho ni kitengo maalumu ndani ya jeshi ambacho hakiuhusiani hivyo na idara jeshi linavitengo vyake pia kama ilivyo polis au takukuru nk
Ndani jw kuna kitengo cha upelelezi
Ila mwisho wa siku tiss ipo kila sehemu yaani ni rahis tiss akapachikwa ndani ya jeshi bila jeshi kujua kuliko jeshi kumpachika mpelelezi wake ndani ya tiss

Sababu kubwa ni malengo ya upelelezi na matumiz ya taarifa yako ni yepi
 
Mkuu hapa umechanganya mambo ya kiufundi. Usalama wa DOLA na usalama wa RAIS. Usalama wa DOLA ndio intelligence ya nchi (TISS) iliyopo chini ofisi ya DOLA, yaani Ikulu. Usalama wa RAIS ndio PSU ambayo kazi yake ni kuhakikisha rais hashambuliwi kimwili. Rais anapanga mkutano Mwembe yanga kwa mfano, TISS watakuwa wameshamaliza kazi yao hata kabla mkutano haujatangazwa. Wao kazi yao ni kukusanya habari za kintelijensia, kuzichakata, kushauri na kutekeleza. PSU ndio watavamia Mwembe yanga baadae kabla ya mkutano wakiwa na mbwa wa kunusa milipuko na kuliweka eneo la mkutano salama kwa Rais. Hapo tena sio suala la Inteligence bali ni usalama wa rais.

Tatizo wananchi wengi tunadhani kila anayefanyakazi ofisi ya rais ni TISS na kwamba kila mpelelezi ni TISS. Mpishi wa rais tunadhani TISS, anayetumwa akanunue dafu la rais tunadhani TISS, anayemshonea rais nguo tunadhani TISS. Mwisho wa siku tunashusha hadhi na usomi wa taasisi kubwa nchini inayolinda usalama wa dola yetu: TISS.
iko hivi
Mkurugenzi wa idara ya usalama chini yake kuna hao psu
Ni kwamba psu wanawajibika kwa mkurugenzi wa idara

Ndio mana hata makazi ya psu yapo ndani ya makzi ya idara ya usalama ambapo hukuti polis wala jw pale ila psu wapo kwa sababu ya muunganiko na asili yao

Upatikanaji wao mafunzo yao wanapikwa pamoja mbele ndo wanatenganishwa kulingana na majukumi

Ni kama ccp mafunzo yao mwishoni ndo wanatenganishwa we utakuwa trafik ffu special unit, upelelezi nk
 
Mkuu hapa umechanganya mambo ya kiufundi. Usalama wa DOLA na usalama wa RAIS. Usalama wa DOLA ndio intelligence ya nchi (TISS) iliyopo chini ofisi ya DOLA, yaani Ikulu. Usalama wa RAIS ndio PSU ambayo kazi yake ni kuhakikisha rais hashambuliwi kimwili. Rais anapanga mkutano Mwembe yanga kwa mfano, TISS watakuwa wameshamaliza kazi yao hata kabla mkutano haujatangazwa. Wao kazi yao ni kukusanya habari za kintelijensia, kuzichakata, kushauri na kutekeleza. PSU ndio watavamia Mwembe yanga baadae kabla ya mkutano wakiwa na mbwa wa kunusa milipuko na kuliweka eneo la mkutano salama kwa Rais. Hapo tena sio suala la Inteligence bali ni usalama wa rais.

Tatizo wananchi wengi tunadhani kila anayefanyakazi ofisi ya rais ni TISS na kwamba kila mpelelezi ni TISS. Mpishi wa rais tunadhani TISS, anayetumwa akanunue dafu la rais tunadhani TISS, anayemshonea rais nguo tunadhani TISS. Mwisho wa siku tunashusha hadhi na usomi wa taasisi kubwa nchini inayolinda usalama wa dola yetu: TISS.
Je raia wanalindwa na nani? Kama TISS inalinda dola na PSU wanalinda Rais,
 
Bahatika siku moja ushike id ya psu na huyo unayemwita tiss angalia
Officials id zao

Hakuna namna yoyote ya kumtenganishi psu na usalama boss wao ni rais sponsor usalama wa taifa jukumu lake moja ni kulinda viongozi wakuu wa nchi kupitia kitengo cha psu sasa
 
ZIELEWE KAZI YA USALAMA WA TAIFA (TISS) NA MIPAKA YAKE

Leo tuongelee TISS au USHUSHU au UNYOKA au IDARA au KITENGO. Kwasababu uelewa mdogo kwa idara hii na kazi zake miongoni mwa wananchi unafanya watu wengi wakose amani wanapokuwa na watu wanaowahisi ni mashushushu, na wakati mwingine watapeliwe na wajanja wanaojifanya watu wa idara.

IDARA YA USALAMA WA TAIFA
Idara ya usalama ni idara maalum chini ya ofisi ya rais. Naam, yaani ukiongelea ushushushu unaongelea idara kubwa ndani ya ikulu yenye mkurugenzi mkuu (Director General of Intelligence Services (DGIS)) na wakurugezi kadhaa wa vitengo mbalimbali (directorates directors) ambao nchi nyingine wanaitwa chiefs, mfano chief wa operesheni au chief wa wafanyakazi na mafunzo. Kutegemea na namna idara ilivyojipanga kunakuwa na ofisi za idara hii wilayani na mikoani.

HISTORIA FUPI YA USALAMA WA TAIFA
Kwenye nchi mbalimbali idara za usalama zilianza kwa kasi nyakati za vita baridi (Cold War) kati ya nchi za Soviet na NATO. Nchi za NATO na washabiki wake wakihofia mashushu wa Soviet kupandikizwa nchini kwao na kushawishi watu kudai sera za kikomunist huku nchi za Soviet na washirika wake zikihofia mashushu wa nchi za NATO na washirika wake kuingia na kushawishi watu wadai siasa za kibepari. Hivyo kama umenifuata vizuri hapa utajuwa kwamba idara ya usalama lengo lake la awali lilikuwa kulinda usalama wa dola dhidi ya adui wa nje na ndani.

KAZI ZA IDARA NA MIPAKA YAKE
Sasa vita baridi vimeisha tatizo nini? Matizo yanayohatarisha usalama wa taifa bado yapo tena mapya na makubwa tu: serikali kupinduliwa, ugaidi, mauaji ya kimbari ya kisiasa (genocide), ukiukwaji wa mikataba ya umoja wa mataifa kama vile madawa ya kulevya, silaha za maangamizi nk. Kwakuwa haya yote yanaweza kutekelezwa na watu wenye maarifa ya juu, akili kubwa, fedha na vitendea kazi vizuri; idara za usalama zinahitaji mfumo imara wa kukusanya taarifa au viashiria kila siku ya Mungu ili kuvichakata, kuvitafsiri, kutunza, na kutolea maamuzi kwa wakati. Mfumo huu hapa Tz tumeuremba kwa jina la kimombo: Tanzania Intelligence and Security Service (TISS), nchi nyingine zinaita Secret Services, nyingine Internal Security and Intelligence nk.

Kwa mantiki hiyo TISS imepewa majukumu makubwa matatu. Mosi, kukusanya taarifa za kintelijensia zihusuzo usalamawa taifa, kuzichakata, kuzitafsiri, kuzitunza, kushauri, na kuziwashirisha kwenye mamlaka husika kwa ajili ya maamuzi. Pili, kumtaarifu rais juu ya uwapo wa viashiria vya uhujumu, uwapo wa mashushu wa nje ya nchi ndani ya Tz au vibaraka wa wavunjifu wa amani na usalama ndani ya Tz na hivyo kupata baraka ya rais kuweka ufuatiliaji wa mambo hayo kwa wakati. Tatu, kushirikiana na wizara na taasisi nyingine za serikali nchini katika kazi zote zihusuzo idara na pia kushirikiana na idara za inchi nyingine kadri ipasavyo katika kutekeleza majukumu yake. Nne, kumhoji mtu au kikundi chochote cha watu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola pamoja na wizara husika.

MPANGO KAZI WA IDARA KWA KAWAIDA NA WAHUSIKA
Kwa kawaida kila siku ya kazi na siku za tukio maalum saa nne Asubuhi usalama wa taifa chini ya DGIS na mchambuzi wa taarifa zakiintelijensia (national intelligence analyst) inafanya mkutano unaoitwa DEBRIEFING kwa mkuu wa nchi. Kwenye mkutano huu mkuu wa nchi anapewa taarifa zote mpya zenye viashiria chanya (credible threats) na taarifa za ufuatiliaji unaoendelea pamoja na changamoto. Baada ya kupata taarifa kinachofuata ni uchambuzi wa taarifa, kutoa maazimio, kumshauri rais na kuomba ridhaa yake katika kutekelezaji.

Utaalamu wa ofisi ya usalama upo kichwani mwa mtu niliyemtaja hapo juu: NATIONAL INTELLIGENCE ANALYST. Wala sio DGIS kama wengi tunavyodhani, DGIS ni bosi tu anayeongoza ofisi na ndio maana akiteuliwa anatangazwa mchana kweupe, na wala haitaji kwenda kusoma huko SCOTLAND YARD tulikozoea kusikia wanakwenda kusomea ushushushu. Nimeona watu wakihoji kwanini ma DGIS wanateuliwa na kutenguliwa hadi kufikia 4 tangu mama Samia ashike madaraka. Niwatoe hofu kwamba tunayetakiwa kushangaa akitenguliwa ni mtu ambaye hatuwezi kumjua kwa urahisi: NATIONAL INTELLIGENCE ANALYST. Mtu huyu akiteuliwa umma haujui wala akitenguliwa haujui. Lakini huyo ndio mtu anayetakiwa awe maili million kadhaa kabla ya wabaya wanaoweza kuhatarisha usalama wa taifa. Mara nyingi anafanyakazi kwa kushirikiana na watu kadhaa.

MIPAKA NA MIIKO YA WATU WA USALAMA WA TAIFA
Pigia mstari point inayofuata: SHUSHUSHU WA TISS HARUHUSIWI KUFANYAKAZI YA KUSIMAMIA SHERIA KAMA ILIVYO KWA POLISI. Pigia tena mstari point inayofuata: SHUSHUSHU WA TISS HARUHUSIWI KUMFUATILIA MTU KWASABABU MTU HUYO ANAJIHUSISHA NA MAANDAMANO YA KIKATIBA AU ANASHIRIKI AU KURATIBU MALALAMIKO DHIDI YA SERIKALI KWA NJIA ZINAZOFUATA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI.

Mfanyakazi wa TISS ana miiko mitatu mikubwa anayotakiwa kuizingatia awapo kazini. (i) kutotangaza kazi yake kwa njia yeyote isipokuwa kwa wanafamilia wakaribu tu. Mkurugenzi mkuu peke yake ndio anayetambulika tangu siku anaapishwa; (ii) kutunza siri za kazi zake zote. Yaani mlaji/mtumiaji wa taarifa za shushu ni rais na idara ya usalama tu, sio umma; (iii) kutotangaza chanzo au vyanzo vya taarifa au kumtaja raia aliyesaidia kupata taarifa za kintelijensia.

MASWALI NA MAJIBU
Nadhani baada ya kusoma bandiko hili utajiuliza TAKUKURU NI USALAMA WA TAIFA? ASKARI KANZU NI USALAMA WA TAIFA? Je wale vijana wanaokesha Best Bite, Break point, Kinondoni Biafara na Mlimani city bila kuwa na kazi maalum nao ni usalama wa taifa? Je wale tunaokunywa nao kisha wakalewa na kujitangaza watu wa idara nao ni usalama? Kama wanajitaganza USALAMA HUU KWELI UPO SALAMA?

Niseme kwa kunong'ona..!! Kimsingi kila wizara, kila shirika, kila kampuni kubwa, kila mkoa, kila wilaya, na kila kwenye shughuli kubwa ya kiuchumi tegemea kwa 90% uwapo wa watu wa usalama. Sasa wapo watu wa usalama wa ngazi mbalimbali; wapo wakudumu kwenye vituo vyao, wapo wafuatiliaji wa tukio/mtu, wapo wasaidizi walioajiriwa kwa kazi maalum ambao yawezekana wala hawajui wanafanyakazi ya idara na wapo wanaofanya ushushushu kwa mujibu wa kazi zao, mfano aliyekuwa kwenye kikosi cha usalama wa kiongozi wa juu Dar akipangiwa kazi nyingine Mufindi ujuwe amehama nyani na msitu wake.

Yote kwa yote huwezi kumjuwa mtu wa usalama aliyeiva kwenye kazi yake na anayefuata kanuni ya kazi yake. Unaweza kuhisi tu. Mtu wa usalama akijitagaza mtilie shaka hapo hapo kwasababu tayari anauweka usalama wa taifa kwenye hatari na yeye mwenyewe pia. Huyo anaweza kuwa MWEHU wa usalama wake mwenyewe. Muhimu usimwogope kama wewe ni raia mwema maana yeye analinda dola, na yeye sio polisi.

SEMA NIMESEMA

Membe S K
Mtama, Rondo Chiponda
Lindi Tanzania
Tel: +255689463664
email: smembe426@gmail.com
Nimepata kitu kikubwa tu
 
Nimeupenda Uzi na unaeleweka vzr ila Nina maswali madogo nataman kufahamu Je

1: Mleta Uzi ni miongoni mwa Teeth au unamaarifa tu kuhusu Teeth ?
Maana hapo chini naona Hadi namba za simu na email kiasi Cha kufanya mtoa comment fulan Kuomba kuunganishwa na kifurushi kama inawezskana 🙏

2: Kama jibu ni Yes yaani ni mwanachama je hii inaweza ikawa ni miongoni mwa njia za recruitment ya kupata walengwa ?🙏
Jiandae kupugwa angakuwa tss asingeweka hizo details zake, kwa namna yoyote ile ila kimjini mjini inaweza kumsaidia kupata maokoto hawa ndo wale kwenye maofisin wanapiga makaunda na kuweka mazingira waonekane tiss flani wajanja wa mjini
 
Duh umeuliza kwa hasira na uchungu inavyoonyesha.

Nasikitika TISS hawana jukumu la moja kwa moja kwenye ubovu wa mikataba. Isipokuwa kama mikataba hiyo ina vipengere vinavyo compromise usalama wa taifa basi idara ya usalama itamulika mkataba huo, kutoa maazimio na kushauri. Lakini kumbuka ushauri wa TISS sio AMRI.
Duuu huna ujuacho na inawezekana hata kazi za kibalozo huzijui ndani ya tiss matumiz yake

Kabisa kabisa

Uchumi upo ndani ya idara miaka 30 ijayo tufanye nini tufikie azma flan
 
Jiandae kupugwa angakuwa tss asingeweka hizo details zake, kwa namna yoyote ile ila kimjini mjini inaweza kumsaidia kupata maokoto hawa ndo wale kwenye maofisin wanapiga makaunda na kuweka mazingira waonekane tiss flani wajanja wa mjini
Uko sahihi ila soma maswali yang vzr utaelewa kwann nimeuliza maana naona umekimbilia kusema nitapigwa unafikr mm Natumia mate kufikiri badala ya ubongo

pili unafaham kama kaka yake alikuwa ni mwanachama anayefahamika Kwa kiwango kikubwa Tena sio wa level ndogo,

tatu unafaham pia kama hizo nafas zinaendag pia kifamilia kwasb mwanafamilia Huwa anachunguzika kirahs toka akiwa mdgo
mwisho unajua ni kwanini Uzi wake haujapigwa burn nayeye mwenyew amekuwa mtoa majibu ya kila aina ya swali, na ni platinum member Tena verified what if amekuja pia Kwa kazi maalumu ya kubrain wash wa TZ juu ya dhana mbovu kuhus idara ?

usinijibu majibu Baki nayo mwenyew
 
Sawasawa kaka, hivi wewe una uhusiano Na hayati mheshimiwa Benard Membe au majina tu yamefanana ???
Samahani kaka Steve
Unauliza swali ukiwa una mfahamu vzr mtoa mada mbona umetaja jina la steve wakati yeye hakuna alipotaja jina steve maana kwenye username yake kaandika initial tu Membe S.K?😁😁😁 anyway huyu ni mdogo wake ndio maana unaona Membe na hiyo initial K yanafanana na hayati
 
Back
Top Bottom