Zifahamu athari za kunywa maji kupita kiasi

Zifahamu athari za kunywa maji kupita kiasi

Basi mimi ni fundi wa kunywa maji
1. Kiwango sahihi cha unywaji wa maji ni
Uzito wako gawa kwa 24, jibu linalopatikana hapo ni kiwango cha maji unachopaswa kunywa kwa lita.
2. Usinywe maji mengi kwa wakati mmoja, jitahidi kunywa maji kidogo kidogo.
 
big_in, Maji yote hayo ya nini?Umekuwa tembo?

Zingatia unachoambiwa humu na wataalamu, kwani jukwaa hili kuna watu wajuvi sana.
 
1. Kiwango sahihi cha unywaji wa maji ni
Uzito wako gawa kwa 24, jibu linalopatikana hapo ni kiwango cha maji unachopaswa kunywa kwa lita.
2. Usinywe maji mengi kwa wakati mmoja, jitahidi kunywa maji kidogo kidogo.
Kwanini tugawe kwa24
 
Kama mwili wako utajizoesha kuwa na maji muda wote utapata adhari utakapokosa maji ata muda mfupi tu, ni vyema ukaruhusu mwili uweze kuzuia maji mwilini na kuyatumia kwa rate inayokuwezesha kufika point B kutokea point A isiyokuwa na maji ama kukuwezesha kufikia muda t2 kutokea t1 ulipokunywa maji. Otherwise ukiugua ugonjwa wa kuhara ukachelewa drip ni kwaheri mwalimu[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana JF,
Wakati mwingine tunapojadili au kutafsiri maandiko ya watu ni vyema kuweka chanzo cha makala husika na au kuweka wasifu wa mhusika.

Mimi si mtaalamu wa sayansi ya unywaji maji ila ni mtaalamu wa afya/daktari LAKINI naona kuna maelezo yanayotolewa kwa jumlajumla bila tahadhali yoyote. Hii inaweza kuwabadili watu kutoka kwenye jambo jema kiafya na kuwapeleka kwenye hali tata kwa kuogopeshwa na maelezo waliyoyasoma.

Suala la unywaji maji hutegemea vichocheo vywa mwili ambavyo humpa taarifa binadamu/mnyama juu ya uhitaji wa maji/kiu. Upataji wa kiu hutegemea zaidi na size ya mwili wa mtu, hali ya hewa, aina ya kazi au mazoezi na utimamu wa vichocheo husika vya mwili juu ya utoaji taarifa ya kiu.

Ni kweli kwamba unywaji wa maji mengi unaweza kuwa na madhara kwa mhusika kutokana na moja kudilute kiasi cha madini yaliyoko mwilini lakini pia kutokana na mfumo wa mzunguko wa damu kuwa hauna nafasi ya ziada ya kubeba kiasi cha maji yaliyonywewa basi unaweza kusababisha kujaa kwa mfumo/overload.

Madhara tajwa hapo juu huweza kujitokeza zaidi pale binadamu au mnyama anapotundikiwa maji/drip. Lakini kutokana na mfumo wa mrejesho hasi/feefback kwa upande wa anaekunywa maji si rahisi kusababisha hilo labda tu kama mfumo wake wa kuondoa kiu na kuridhika/satisfaction utakuwa una shida.

Kitaalamu kwa siku, inakisiwa kisayansi kuwa kwa ujumla (jasho, kupumua, choo kikubwa, kuongea pamoja na mkojo) vinasababisha kiwango cha maji lita moja na nusu kutoka mwilini. Njia ipi hutoa zaidi, hutegemeana na hali ya mazingira husika
Hivyo ni vizuri kurudisha kiasi hiki cha maji mwilini japo si kwa wakati mmoja.

Ni kweli kwamba kadri unavyokunywa maji ndivyo mwili utakubali kutoa maji kama jasho au mkojo. Na kadri usivyokunywa maji ya kutosha ndivyo mwili hautayatoa hayo maji, hii haimaanishi kuwa uko salama zaidi au na afya njema bali mwili unang'ang'ania maji hayo kutokana na kutokuwa na maji toshelevu. Hivyo, kama ukipata choo kitakuwa kigumu, mkojo utakuwa ni wanjano/concentrated, jasho kidogo na lenye chumvi nyingi. Hii ni hatari kwa afya kwani mwili utabakiza uchafu mwingi mwilini kwa kukosa maji ya kuandamana na huo uchafu.

Nini kifanyike?
Tii kiu yako, kunywa maji kwani mahesabu mengi hayazingatii hali ya mazingiira uliyopo ambapo kila mmoja huitaji ku-adjust kulingana na hali yake na mazingira. Isipokuwa kwa wale wenye shida maalumu kama matatizo ya digo nk.

Pale unapoona wewe unakunywa maji mengi kupindukia kuzidi watu wanaokuzunguka, fika kwa wataalamu wa afya wakufanyie uchunguzi kwani matatizo ya vichocheo tajwa hapo juu yapo.

Kunywa maji kwa afya.
 
Unywaji wa maji wa Watu waliopo London tusiufananishe na hapa kwetu Dar. Huko unaweza ukanywa glasi 2 au 3 kwa siku na mwili ukawa kawaida tu.

Hali ya hewa ya huko na huku ni tofauti Sana. Labda kipindi cha summer ambacho ni miezi 2 tu ndio kunakua na joto.

Nikiwa huko nitafata ushauri wake ila nikiwa huku ni lita 2.5 kwa siku ni lazima.
 
Jua ni Kali sana Dar,Maji ni Muhimu ila kwa kiasi
 
Back
Top Bottom