Zifahamu athari za kunywa maji kupita kiasi

Good comment, ila hujashauri kwa wastani kiasi gani cha maji kitumike kwa mtu mzima tuliyopo ktk Tropical Countries
 
Good comment, ila hujashauri kwa wastani kiasi gani cha maji kitumike kwa mtu mzima tuliyopo ktk Tropical Countries

Sayansi inaeleza kuwa jumla ya upoteaji wa maji kwa siku ni lita kwa wastani ni lita 1.5, lakini hii inaweza kuongezeka zaidi au kupungua kulingana na:
-ukubwa wa mwili
-aina ya kazi
-mazoezi
-hali ya hewa/mazingira
-joto la mwili wako/mgonjwa
-uwepo wa magonjwa mengine yanayoweza kuathiri matumizi ya maji mwilini

Ukizingatia tu baadhi ya vitu tajwa hapo juu, huwezi kutoa jibu la jumla kwa kila mmoja anywe maji kiasi gani kwa kuwa yuko kwenye eneo la ki-Tropic. Ingawa, cha kwanza ni kurudisha hiyo lita 1.5 kwa siku kama wastani wa kwanza.
Kwani kila mmoja kwenye eneo tajwa bado anaweza kuwa na mazingira tofauti ya mwili wake na shughuli.

Mfano:
  • mfanyakazi anaeshinda kwenye chumba chenye air condition.
  • machinga anaeuza kanga juani
  • mkulima anaeshinda shamba
-mfanyakazi kwenye mazingira ya boiler
nk.

Kila mmoja atahitaji adjustment/ongezeko kulingana na sababu mbalimbali zinazofanya kuongeza au kupunguza utoaji vs uchukuaji wa maji yaliyopungua.

NB: Kama hauna shida yoyote kiafya, wewe tii kiu yako na kujenga mazoea ya kunywa maji, feedback mechanism ya mwili ipo kukulinda kama kitoshelezi cha mwili kimefikiwa.

Pia ukitaka kuwa na uhakika/precisely unaweza kumwona mtaalamu aliyekaribu nawe umweleze aina ya kazi na vyote unavyochukua kwa siku kama vinywaji na chakula ili kuwa na uhakika ni kiasi gani uchukue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…