Zijue aina za utajiri wa kichawi zinazoshika kasi kwa sasa

Zijue aina za utajiri wa kichawi zinazoshika kasi kwa sasa

Tembea uone mambo ya ajabu yaliyopo Tanzania hii, yaani ukiwa mtanzania tayari umeshajiunganisha na mambo ya shirki Moja Kwa moja😀 neema ya mungu ikuokoe tu. Usione mtu ana push ndinga kali ana drip na ni kijana mdogo tu, we jua utajiri una Siri nyingi sana. Hizi ni baadhi ya aina ya utajiri watu wanatumia.

👉Utajiri wa Shilingi: Hapa unapewa coin inakuwa inakuingizia pesa ukikosea mashariti inapotea unarudi kapuku (rupee hizi wakinga ndo wanazo) hapa utaanza na kafara za kuku mwisho damu itahitajila

👉Utajiri wa nyoka: Hapa unapewa kanyoka kadogo kadiri kanavokua ndo utajiri wako unaongezeka na Kila mwaka inabidi utoe sadaka kurenew huyo nyoka ukibugi unarudi katika ufukara

👉Utajiri wa kafara: Huu wengi hawautaki siku hizi na hata wakitumia hawataki kuua ndugu zao siku hizi mtu ana magari anatoa kafara gari linaanguka watu wanateketea ova. Au mtu anafunga ofisi au taasisi halafu watumishi ndo wanateketea.

👉Utajiri wa kidonda: Hapa unakua na kidonda ambacho akiponi na kadiri unavotumia Mali zako ndo kinaongezeka. Unachagua wewe kidonda kiwe sehemu Gani ya mwili.

👉Utajiri wa kupunguzwa nguvu: Hapa unachagua kiungo kimoja ambacho kinatolewa nguvu kichawi, unakua nacho ila hakifanyi kazi. Mfano jicho, mtu anakua na macho yote mawili ila ni Moja ndo linafanya kazi kidole, mkono hata pumbu.

👉Misukule: Hapa unamiliki Misukule ambayo inakua inakufanyia shughuli zako zote huku wewe umekaa umekunja nne, huu upo vijijini Kwa shughuli za shamba

👉Utajiri wa punje: Hapa inaenda Kwa mganga anakupa jogoo lililoshiba usishangae likala punje mbili tatu tu na hio ndo inakua miaka yako ya kusumbua ukiwa tajiri

👉Utajiri wa Chuma ulete: Huu nao watu hawautaki siku hizi maana kuumbuka nje nje. Kuna mzee mmoja aliwahi vutishwa mavi duka lake lilinuka kinyesi watu walichezesha mkeka🤣🤣.

👉Utajiri wa kafara ya ndugu wa damu unaempenda: Hapa utake utamtoa usitake utamtoa ama ufe wewe😀😀 ibilisi anakuchagulia

Jamani zinatosha ila mambo ni mengi muda mchache watu wana macho lakini hawaoni mtu anamasikio lakini hasikii yaani kwa kifupi hakuna pesa ya shortcut yenye mwisho mzuri.

Nawasilisha.
Kuamini uchawi ni ujinga tu.

Na watanzania wengi wanaoamini uchawi ni wajinga.
 
Kula raha maisgja mafupi kwani aliyewekewa masharti ni wewe? Peleka idea zako za kibiashara upate uwezeshwaji ili kesho na keshokutwa akishushwa uwe unampiga tafu,sidhani km hayo masharti yake asipoyatekeleza km yana impact hadi kwa aliowawezesha na km ingekuwa hivyo wale matajiri waliopata kwa njia hyo watoto wao waliowasomesha shule bora elimu yao ingefutika vichwani mwao,omba upigwe jeki laana ni yake
Ibilisi atamtamani amchukue nae😀😀
 
Mimi toka nitake shortcut nikajikuta nimeharibu kila kitu,mpaka sasa sitaki shortcut

Niliamin kabisa maisha hayana shortcut

Hata kama utatumia shortcut,kumbuka kuna siku itafika utalazimika kutumia njia halali ambayo ni ndefu
Ni kweli Kila jambo Lina mwisho
 
Hiyo ya Misukule..jamaa kaenda dukani kwa Muhindi kununua bidhaa kumbe na misukule yake nayo inabeba kwa wizi. Wakati wa kulipa Muhindi anamuambia jamaa pesa unayolipa mbona haifanani na mzigo uliyonunua..akijumlisha na ile waliyokuwa wanabeba misukule(Muhindi alikuwa nae wamo).
Muhindi kwa kumkomoa akaitaifisha ile Misukule na jamaa utajiri ukaisha.
 
Kuna jamaa alipachikwa kidonda cha mgongoni, mpaka sasa anahangaika na kidonda ila Mali ipo. Kikitoa usaha, pesa zinaongezeka. Ila hii ni poa, unajitesa mwenyewe, hata Mungu anaikubali.
Mungu hahusiki na upumbavu kama huo acheni kumsingizia maana alisema "Me atakula kwa jasho"

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo ya Misukule..jamaa kaenda dukani kwa Muhindi kununua bidhaa kumbe na misukule yake nayo inabeba kwa wizi. Wakati wa kulipa Muhindi anamuambia jamaa pesa unayolipa mbona haifanani na mzigo uliyonunua..akijumlisha na ile waliyokuwa wanabeba misukule(Muhindi alikuwa nae wamo).
Muhindi kwa kumkomoa akaitaifisha ile Misukule na jamaa utajiri ukaisha.
Mhindi nae aliaga😲😲 dunia Ina mambo
 
Back
Top Bottom