Mkuu usibishe Kwa mazoea uchawi upo. Huenda wewe na mimi sio wachawi ila ww utake usitake uchawi upo na hayo niloyasema yapo Tena Kuna zaidi ya hayo but who knows? Naomba niishie hapo
Mkuu,
Nimekuuliza maswali mawili madogo tu umeshindwa kuyajibu.
1. Uchawi ni nini?
2. Ukiona kitu, utajuaje huu ni uchawi na si kitu kingine tu ambacho kinaweza kupata maelezo bila kutumia hoja ya uchawi, kitu ambacho wewe hukielewi tu?
Mtu asiyeelewa mchezo wa karata tatu, akifanyiwa trick kama hajajua karata tatu inachezwaje, anaweza kuamini kuwa karata tatu ni uchawi, lakini, karata tatu ni ujanja tu, si uchawi. Hata wewe ukijifunza unaweza kuchezesha karata tatu.
Mababu na mabibi zetu wa kale, walipokutana na wazungu, wazungu wakaweza kutumia vyombo vya umeme kupiga muziki, babu na bibi zetu waliwaona wazungu kama wachawi. Neno "mzungu" katika Kiswahili cha kale na lugha nyingi za makabila ya kibantu ni neno linalowakilisha miungu, ndiyo maana neno mzungu liko karibu sana na neno Mungu. Tuliwaona wazungu kama miungu kwa sababu walikuwa wanafanya mambo ambayo tuliamini ni uchawi.
Hatukuelewa dawa zao zinavyofanya kazi, zilivyoweza kutibu kwa haraka tukawaona wana uchawi.
Hatukuelewa silaha zao zinavyoweza kuua kutoka mbali, tukaona huu ni uchawi, mpaka kwenye vita vya Maji Maji tukawajibu kwa uchawi ambao tulifikiri utageuza risasi kuwa maji, obviously uchawi wetu haukufanya kazi ndiyo maana tukashindwa vita.
Wazungu waliweza kutabiri jua linavyopatwa (solar eclipse), sisi hatukujua jiografia, tukaona huo ni uchawi.
Sasa, na wewe leo, hicho unachokiita uchawi, unajuaje ni uchawi kweli, na si kingine tu ambacho hujakijua ambacho si uchawi?
Hujajibu maswali haya.