Zijue aina za utajiri wa kichawi zinazoshika kasi kwa sasa

Zijue aina za utajiri wa kichawi zinazoshika kasi kwa sasa

Mkuu hapa umeuma nje ,inategemea kopera ni WA mbinu gani ,wapo aina saba Ila tatu ndo muhimu Sana :
1: Kuna wakutengezwa na miti shamba
2: wa talasimu
3: huyu unamtengeza kichawi kutumia duara
Wa pili na tatu wanaiba siyo chini ya millioni hamsini kwa wiki .
Ila utafuga mifugo wanakunywa damu hatari Sana
Na ukichoka naye hasa watatu unamtupa kwenye maji yenye kina kirefu na Mali unabaki nayo bila bughudha
Hawataki damu za watu kweli
 
Mkuu hapa umeuma nje ,inategemea kopera ni WA mbinu gani ,wapo aina saba Ila tatu ndo muhimu Sana :
1: Kuna wakutengezwa na miti shamba
2: wa talasimu
3: huyu unamtengeza kichawi kutumia duara
Wa pili na tatu wanaiba siyo chini ya millioni hamsini kwa wiki .
Ila utafuga mifugo wanakunywa damu hatari Sana
Na ukichoka naye hasa watatu unamtupa kwenye maji yenye kina kirefu na Mali unabaki nayo bila bughudha
Baharini si ndipo penye kina kirefu?

Afu roho chafu inakufa kufaje nakati tayari ina connection na roho ya shetani (immortal creature)?

Hapa kuna washamba utawadaka PM ili wanase kwenye hiyo no. 3 japo ni uwongo per 100%

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Tembea uone mambo ya ajabu yaliyopo Tanzania hii, yaani ukiwa mtanzania tayari umeshajiunganisha na mambo ya shirki Moja Kwa moja[emoji3] neema ya mungu ikuokoe tu. Usione mtu ana push ndinga kali ana drip na ni kijana mdogo tu, we jua utajiri una Siri nyingi sana. Hizi ni baadhi ya aina ya utajiri watu wanatumia.

[emoji117]Utajiri wa Shilingi: Hapa unapewa coin inakuwa inakuingizia pesa ukikosea mashariti inapotea unarudi kapuku (rupee hizi wakinga ndo wanazo) hapa utaanza na kafara za kuku mwisho damu itahitajila

[emoji117]Utajiri wa nyoka: Hapa unapewa kanyoka kadogo kadiri kanavokua ndo utajiri wako unaongezeka na Kila mwaka inabidi utoe sadaka kurenew huyo nyoka ukibugi unarudi katika ufukara

[emoji117]Utajiri wa kafara: Huu wengi hawautaki siku hizi na hata wakitumia hawataki kuua ndugu zao siku hizi mtu ana magari anatoa kafara gari linaanguka watu wanateketea ova. Au mtu anafunga ofisi au taasisi halafu watumishi ndo wanateketea.

[emoji117]Utajiri wa kidonda: Hapa unakua na kidonda ambacho akiponi na kadiri unavotumia Mali zako ndo kinaongezeka. Unachagua wewe kidonda kiwe sehemu Gani ya mwili.

[emoji117]Utajiri wa kupunguzwa nguvu: Hapa unachagua kiungo kimoja ambacho kinatolewa nguvu kichawi, unakua nacho ila hakifanyi kazi. Mfano jicho, mtu anakua na macho yote mawili ila ni Moja ndo linafanya kazi kidole, mkono hata pumbu.

[emoji117]Misukule: Hapa unamiliki Misukule ambayo inakua inakufanyia shughuli zako zote huku wewe umekaa umekunja nne, huu upo vijijini Kwa shughuli za shamba

[emoji117]Utajiri wa punje: Hapa inaenda Kwa mganga anakupa jogoo lililoshiba usishangae likala punje mbili tatu tu na hio ndo inakua miaka yako ya kusumbua ukiwa tajiri

[emoji117]Utajiri wa Chuma ulete: Huu nao watu hawautaki siku hizi maana kuumbuka nje nje. Kuna mzee mmoja aliwahi vutishwa mavi duka lake lilinuka kinyesi watu walichezesha mkeka[emoji1787][emoji1787].

[emoji117]Utajiri wa kafara ya ndugu wa damu unaempenda: Hapa utake utamtoa usitake utamtoa ama ufe wewe[emoji3][emoji3] ibilisi anakuchagulia

Jamani zinatosha ila mambo ni mengi muda mchache watu wana macho lakini hawaoni mtu anamasikio lakini hasikii yaani kwa kifupi hakuna pesa ya shortcut yenye mwisho mzuri.

Nawasilisha.

Kama utani utani ila watu wengi wanaishi humo
 
Hiyo mganga nae anakuwa tajiri au anaendelea kutaabika na umaskini akisubiri mumpelelee kuku
 
Back
Top Bottom