Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
1. Nguvu gani? Unajuaje nguvu hiyo iko nje ya sayansi, na si kwamba ni ya kisayansi tu ila wewe huijui?1: Uchawi ni nguvu inayotumiwa na watu wenye maarifa maalum yasiyo ya kisayansi.
2:utajua huu ni uchawi endapo utaona kitu Cha kawaida ambacho ki ubinadamu hakiwezi kutendeka. Mfano ukapigwa makofi na mtu ambaye humuoni wewe utahisi nn
Nitakupa mfano, kwa mtu asiyejua chemistry, anaweza kuona mtu kavaa nguo za ajabu anapita na kunuiza maneno, halafu watu wanakufa.
Akamuona huyu mtu ni mchawi. Kasema maneno tu halafu watu wanakufa? Lazima atakuwa mchawi.
Kumbe hajui, yule mtu kapita akinyunyiza sumu ya cyanide ambayo ukiivuta hewani unakufa, na zile nguo za ajabu amezitumia kujikinga yeye na sumu hiyo.
Sasa hapo kama mtu una mawazo ya kuamini uchawi, bila hata kuhoji, utasema huu uchawi.
Wakati kuna sayansi inayoweza kuelezea vizuru tu mambo yote yaliyotokea.
2. Unaweza kuona unapigwa makofi na mtu usiyemuona kwa sababu una matatizo ya akili tu ya hallucination. Matatizo haya yapo mengi sana kwetu, na hatujayaagua vizuri. Ndiyo maana wenzetu wana majina mengi ya magonjwa ya akili, mara bipolar disorder, mara schizophrenia, mara obsessive-compulsive disorder etc, sisi tunajua "kichaa" tu.
Sasa katika jamii ambayo hata magonjwa ya akili hatujayachunguza vizuri na kuyaelewa, tutakimbilia vipi kusema mtu anayesema kapigwa kofi na mtu asiyemuona ameona jambo la uchawi na si jambo la hallucination na mental health issue?
Kwa nini tunapenda kukimbilia jibu rahisi la uchawi kabla ya kuchunguza mambo na kuyaelewa vizuri?