Zijue aina za utajiri wa kichawi zinazoshika kasi kwa sasa

1: Uchawi ni nguvu inayotumiwa na watu wenye maarifa maalum yasiyo ya kisayansi.

2:utajua huu ni uchawi endapo utaona kitu Cha kawaida ambacho ki ubinadamu hakiwezi kutendeka. Mfano ukapigwa makofi na mtu ambaye humuoni wewe utahisi nn
1. Nguvu gani? Unajuaje nguvu hiyo iko nje ya sayansi, na si kwamba ni ya kisayansi tu ila wewe huijui?

Nitakupa mfano, kwa mtu asiyejua chemistry, anaweza kuona mtu kavaa nguo za ajabu anapita na kunuiza maneno, halafu watu wanakufa.

Akamuona huyu mtu ni mchawi. Kasema maneno tu halafu watu wanakufa? Lazima atakuwa mchawi.

Kumbe hajui, yule mtu kapita akinyunyiza sumu ya cyanide ambayo ukiivuta hewani unakufa, na zile nguo za ajabu amezitumia kujikinga yeye na sumu hiyo.

Sasa hapo kama mtu una mawazo ya kuamini uchawi, bila hata kuhoji, utasema huu uchawi.

Wakati kuna sayansi inayoweza kuelezea vizuru tu mambo yote yaliyotokea.

2. Unaweza kuona unapigwa makofi na mtu usiyemuona kwa sababu una matatizo ya akili tu ya hallucination. Matatizo haya yapo mengi sana kwetu, na hatujayaagua vizuri. Ndiyo maana wenzetu wana majina mengi ya magonjwa ya akili, mara bipolar disorder, mara schizophrenia, mara obsessive-compulsive disorder etc, sisi tunajua "kichaa" tu.

Sasa katika jamii ambayo hata magonjwa ya akili hatujayachunguza vizuri na kuyaelewa, tutakimbilia vipi kusema mtu anayesema kapigwa kofi na mtu asiyemuona ameona jambo la uchawi na si jambo la hallucination na mental health issue?

Kwa nini tunapenda kukimbilia jibu rahisi la uchawi kabla ya kuchunguza mambo na kuyaelewa vizuri?
 
Nitakupa mfano, kwa mtu asiyejua chemistry, anaweza kuona mtu kavaa nguo za ajabu anapita na kunuiza maneno, halafu watu wanakufa.
Hio nguvu ni Kwa watu maalum boss mbona definition imeelezea vizuri sio Kila mtu
 
Unaweza kuona unapigwa makofi na mtu usiyemuona kwa sababu una matatizo ya akili tu ya hallucination.
Unaleta hoja za kisayansi ambazo zinapingana na biblia hata Imani zingine Sasa ibaki hivi sayansi ni sanyansi na uchawi pia upo mungu pia yupo hutaki unaacha
 
Toa exp Kwa wengine
 
Dunia Ina mambo
 
Hio nguvu ni Kwa watu maalum boss mbona definition imeelezea vizuri sio Kila mtu
Hiyo ni "Deus ex Machina".

Wagiriki wa kale walikuwa wanapenda sana maigizo. Wanatenga sehemu, wanakaa, wanaagalia maigizo.

Na katika maigizo yao, story inavyozidi kuchanganya, inavyozidi kuwa complex, ndivyo watu walivyoipenda zaidi.

Sasa, kukawa na stories nyingine zinakuwa so complex mpaka kuzimaliza vizuri inakuwa tabu, yani story inakosa resolution nzuri.

Basi, ili kumaliza stories kama hizo, wakawa wanatumia device moja inaitwa "Deus ex Machina".

Yani wanalishusha limungu lao kubwa la mbao, linamaliza matatizo yote yaliyotokea katika hadithi hiyo.

Mapaka leo, muandishi wa hadithi akiandika hadithi ambayo ameipa resolution ya kulazimisha mambo yamalizike tu, anaambiwa kwamba katumia "Deus ex Machina".

Katika waandishi, hili ni tusi kwamba umemaliza mambo ghafla kwa nguvu bila kutoa resolution ya kimantiki.

Ndicho ulichofanya hapa.

Deus ex Machina.

 
Ok ni vile siko interested na kubishana Sina fact Sina contents, nakupa point 3 muhimu
 
Unaleta hoja za kisayansi ambazo zinapingana na biblia hata Imani zingine Sasa ibaki hivi sayansi ni sanyansi na uchawi pia upo mungu pia yupo hutaki unaacha
Hapana, huwezi kunilazimisha kuacha wakati hoja zako hazina mashiko.

Hujathibitisha uchawi upo. Hujathibitisha Mungu yupo.

Kuna watu ,Mombasa walikutwa wanachez auchi nje ya gari. Raia wakaaminishwa kwamba hao ni wezi wameiba gari, lakini gari ilikuwa imefungwa alarm ya uchawi, wamerogeka, wakapaki gari na kuanza kucheza uchi kutokana na nguvu ya uchawi.

Raia wa Kenya ambao wanapenda kuamini uchawi wakaamini.

Polisi wakachunguza kidogo tu, wakagundua kuwa ule ulikuwa ni mpango tu kati ya wale watu na mganga mmoja wa kienyeji.

Wale watu wamelipwa kucheza uchi ili mganga wa kienyeji ajiongezee soko.

Sasa hapo kwa nyie mnaoamini uchawi mngeshikwa kijinga na kirahisi tu.

Wakati habari nzima ilipangwa tu, hakuna uchawi hapo.

Sasa unajuaje na wewe unavyoamini uchawi huamini utapeli wa watu tu?

Unaweza kuisoma habari hii kwa undani zaidi hapa.


 
Ok ni vile siko interested na kubishana Sina fact Sina contents, nakupa point 3 muhimu
Uko interested na kubishana, ndiyo maana umebishana mpaka hapa.

Iila huwezi tu, kwa sababu umesimamia imani za uongo, huwezi kuwa na facts kwenye imani za uongo, wewe unakwenda counter-factual. Huwezi kwenda na facts.

Hakuna fact ya kuthibitisha uwepo wa uchawi, hizo ni imani za kijinga tu.
 
Chuma ulete ina limitations... Inakupa mahitaji muhimu tuu. Pesa yake huwezi hata kununua nguo nzuri sana sana utaishia malonya kwakuwa ukichuma sana kwa siku ni mwekundu na kuipata tena hiyo inaweza kukuchukua mpaka siku 14
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…