Zijue aina za utajiri wa kichawi zinazoshika kasi kwa sasa

Zijue aina za utajiri wa kichawi zinazoshika kasi kwa sasa

Kuheshima fikra, mitazamo na mawazo ya watu ni ishara ya mtu mwenye elimu.

Ila kwako inatia mashaka maana unathubutu kuita mitizamo ya watu ni ujinga, kuwa mstaarabu na heshimu mitizamo ya watu.
Mkuu,

Ukija hapa unahubiri habari kwamba mavi ni dawa ya kurefusha maisha, ukawaambia watu wale mavi ili wawe na maisha marefu, halafu mimi najua mavi hayarefushi maisha, in fact kula mavi kutasambaza kipindupindu, nikikwambia huo ni uongo, mavi hayarefushi maisha, yanaleta kipindupindu, nitakuwa sijaheshimu mawazo yako au nitakuwa nimekuambia ukweli muhimu tu ambao utanusuru maisha ya watu ambao hawatapata kipindupindu kwa kuamini uongo wako?

Kwa nini tunaweka kipaumbele kuheshimu mawazo ya watu, hata kama ni ya ujinga?

Wewe huoni kwamba ukinikataza kumuita mtu mjinga mjinga na wewe hujaheshimu mawazo yangu ya kumuona huyu mjinga na kusema hivyo?

Kwa nini tusibishane on the facts, nani mjinga, kwa nini mjinga, je kumuita mjinga mjinga ni sawa au si sawa?

Kwa nini tusiangalie ujinga kama dhana abstract, tukataka kuutokomeza?

Kwa nini kumuita mjinga mjinga liwe tatizo kama mtu ni mjinga kweli?

Unaelewa kwamba ujinga si tusi, ujinga ni hali ya kutojua kitu?
 
Hapo ndo utajua ujinga wa imani za uchawi.

Uchawi ungekuwa upo kweli, Waafrika tusingetawaliwa kama tunavyotawaliwa.

Maana sisi tumeshikilia sana imani za uchawi.

Wakati wenzetu wameshikilia sayansi, teknolojia na uchumi.
Ile ni sayansi
 
Imani zingine za ajabu sana mtu akishakua na pesa mtatafta sababu za utajiri wake hakuna utajiri wa hivo watu wanapambana
 
Imani zingine za ajabu sana mtu akishakua na pesa mtatafta sababu za utajiri wake hakuna utajiri wa hivo watu wanapambana
Kuna msiba umetokea huku kitaa tayari jamaa anakua accused Kwa kumuuaa mtoto wake kisa jamaa ana Mali😀😀
 
Wafanyakazi wana vinasaba Gani...na utajir....
Mm Huwa natamani research zifanyike yaan pale UDSM ianzishwe department ya witchcraft & associates
Najuuliza Nchi kama Norway ni namba Moja kwenye Fishing industry

Nchi ZILIZO undergo Industrial revolution na wenyewe wana amini KATIKA ushirikina....????

Bado tunasafari ndefu sana kama taifa....

Ahahah kweli mzee yaan watu wanashindw kuamin kbsa kua mafanikio yapo bila izo mambo
 
Ukifanikiwa kidogo watu huwa wanaamua kukutengenezea stori ambayo hujawahi kuiishi
Hasa hizi biashara za usafirishaji huwa kuna changamoto nyingi sana unajitahidi uiweke gari kwenye hali nzuri na marekebisho ya mara kwa mara unafunga tairi mpya ila zinapasuka gari inaanguka inaua watu Unaambiwa umetoa kafara.

Unapambana had na madereva wako unawaambia hutaki gari zako zikimbie, zifate utaratibu na Sheria za barabarani hutaki ligi ila unakuja kusikia bus imegongana uso kwa uso na imeua watu 9 na wafanyakazi wote waliokua wamekaa mbele na chanzo Cha ajali ni Lori lililo overtake bila tahadhari ila stori itatengenezwa kuwa mmliki wa bus ndo umetoa kafara

Kuna safar ndefu sana aiseee
 
Ile ni sayansi
Unajuaje hii ni sayansi na huu ni uchawi? Na unapofikiri kitu ni uchawi si sayansi, unajuaje kwamba hapo hufikiri hivyo kwa ujinga wako tu?

Mtu ambaye haelewi mchezo wa karata tatu anaweza kuona ni uchawi, wakati ni trick inayoweza kuelezewa kisayansi tu.

Sasa, na wewe unayefikiri unaona uchawi, unajuaje kwamba huoni mchezo kama karata tatu tu, ambao unaelezeka kisayansi, ila wewe bado hujauelewa unachezwa vipi tu?
 
Unajuaje hii ni sayansi na huu ni uchawi? Na unapofikiri kitu ni uchawi si sayansi, unajuaje kwamba hapo unafikiri hivyo kwa ujinga wako tu?

Mtu ambaye haelewi mchezo wa karata tatu anaweza kuona ni uchawi, wakati ni trick inayoweza kuelezewa kisayansi tu.

Sasa, na wewe unayefikiri unaona uchawi, unajuaje kwamba huoni mchezo kama karata tatu tu, ambao unaelezeka kisayansi, ila wewe bado hujauelewa unachezwa vipi tu?
Mimi nimesema Elon munsk anatumia sayansi na tunaona kabisa ni sayansi.
Sijsema kwamba uchawi ni sayansi
 
Ila waganga bana, masharti yao mengi ni huwa tushindwe tu.
Ndo ibilisi. Tangu lini ibilisi akupe mafanikio afu uishi Kwa raha? Raha ya ibilisi ni wewe ule msoto
 
Back
Top Bottom