Zijue aina za utajiri wa kichawi zinazoshika kasi kwa sasa

Zijue aina za utajiri wa kichawi zinazoshika kasi kwa sasa

🥲🥲🥲

Yaani ajinyee sio
Ndio hivo mkuu. Yaani siku yakuanguka unaijua kabisa hata kwenye biashara huendi. Mpaka ukishamwaga mbolea ndio sasa unaweza ukaoga ukaingia ofisini umejipiga moka safi,suti kali, tai kama unataka na perform yako nani atakujua kama umejisaidia chumbani.

Utajiri mzuri huo hutesi mtu wala kumwaga damu
 
Hiyo ya Misukule..jamaa kaenda dukani kwa Muhindi kununua bidhaa kumbe na misukule yake nayo inabeba kwa wizi. Wakati wa kulipa Muhindi anamuambia jamaa pesa unayolipa mbona haifanani na mzigo uliyonunua..akijumlisha na ile waliyokuwa wanabeba misukule(Muhindi alikuwa nae wamo).
Muhindi kwa kumkomoa akaitaifisha ile Misukule na jamaa utajiri ukaisha.
Huyu jamaa WA kule Lindi?!!anaittwa bahati mbaya na Sasa kafa?!!au mwingine?
Maana inafanana na ya marehemu bahati mbaya

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hapana siwezi Kwa kweli maana kama ningetaka ningekua mchawi wa kutisha nimeishi na watu wanaendaa ngende mpk namba nilipewa za ngende,mpiga miti Kwa bibi yule,masasi Kwa mabula Tena yule kipindi cha chaguzi hapatikani anatembea na wabunge ,pande ,mpk njinjo Tena njinjo uganga wa mapenzi balaaa [emoji1][emoji1787][emoji16][emoji1787] ila kubwa naogopa Sanaa shirk na Haina msaada Kwa mwanadamu namuogopa Sana Mungu na ni Dhambi kubwa kuliko zote....



Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Inaweza kuwa yenyewe..maana ilikuwa kati ya Lindi au Mtwara mjini
Lindi ng'ap ni story ya kwelii kabisaa huyooo alikua ana kawaida ya kufunga mzigo anannua mzigo Wa 5m kumbe misukule yake wanabeba mzigo Wa 10m Ndo akaja kukamatwa Tena alikua mfanyakazi wa yule mhindi ndo alimshtua bosi akamuambia boss kua jamaa ana watu wanabeba Wengine kimazingara ndo alivyomaliza akaambiwa pesa aliyotoa ndogo maana Kuna watu walikua wanasaidia kubeba mzigo[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]ndo ikawa mwisho wa Bahati mbayaa akafirisika na mpk anakufa Hana kitu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Tembea uone mambo ya ajabu yaliyopo Tanzania hii, yaani ukiwa mtanzania tayari umeshajiunganisha na mambo ya shirki Moja Kwa moja[emoji3] neema ya mungu ikuokoe tu. Usione mtu ana push ndinga kali ana drip na ni kijana mdogo tu, we jua utajiri una Siri nyingi sana. Hizi ni baadhi ya aina ya utajiri watu wanatumia.

[emoji117]Utajiri wa Shilingi: Hapa unapewa coin inakuwa inakuingizia pesa ukikosea mashariti inapotea unarudi kapuku (rupee hizi wakinga ndo wanazo) hapa utaanza na kafara za kuku mwisho damu itahitajila

[emoji117]Utajiri wa nyoka: Hapa unapewa kanyoka kadogo kadiri kanavokua ndo utajiri wako unaongezeka na Kila mwaka inabidi utoe sadaka kurenew huyo nyoka ukibugi unarudi katika ufukara

[emoji117]Utajiri wa kafara: Huu wengi hawautaki siku hizi na hata wakitumia hawataki kuua ndugu zao siku hizi mtu ana magari anatoa kafara gari linaanguka watu wanateketea ova. Au mtu anafunga ofisi au taasisi halafu watumishi ndo wanateketea.

[emoji117]Utajiri wa kidonda: Hapa unakua na kidonda ambacho akiponi na kadiri unavotumia Mali zako ndo kinaongezeka. Unachagua wewe kidonda kiwe sehemu Gani ya mwili.

[emoji117]Utajiri wa kupunguzwa nguvu: Hapa unachagua kiungo kimoja ambacho kinatolewa nguvu kichawi, unakua nacho ila hakifanyi kazi. Mfano jicho, mtu anakua na macho yote mawili ila ni Moja ndo linafanya kazi kidole, mkono hata pumbu.

[emoji117]Misukule: Hapa unamiliki Misukule ambayo inakua inakufanyia shughuli zako zote huku wewe umekaa umekunja nne, huu upo vijijini Kwa shughuli za shamba

[emoji117]Utajiri wa punje: Hapa inaenda Kwa mganga anakupa jogoo lililoshiba usishangae likala punje mbili tatu tu na hio ndo inakua miaka yako ya kusumbua ukiwa tajiri

[emoji117]Utajiri wa Chuma ulete: Huu nao watu hawautaki siku hizi maana kuumbuka nje nje. Kuna mzee mmoja aliwahi vutishwa mavi duka lake lilinuka kinyesi watu walichezesha mkeka[emoji1787][emoji1787].

[emoji117]Utajiri wa kafara ya ndugu wa damu unaempenda: Hapa utake utamtoa usitake utamtoa ama ufe wewe[emoji3][emoji3] ibilisi anakuchagulia

Jamani zinatosha ila mambo ni mengi muda mchache watu wana macho lakini hawaoni mtu anamasikio lakini hasikii yaani kwa kifupi hakuna pesa ya shortcut yenye mwisho mzuri.

Nawasilisha.
Mboni umewathahau wale ndugu dhetu "Fuliimathon" au siku hizi hawana hela?
 
Back
Top Bottom