Yani unavyoandika ni kama vile wanawake wenye hivyo vigezo mnavyovitaka wapo wengi sana kiasi cha kuwatosheleza wanaume wote wanaotaka kuoa, ninawajua wanaume wengi sana waliochelewa kuoa kwa kujidai wanafanya vetting ila mwisho wa siku wakaja kuoa hao hao huku wakidai kwamba ndio wana afadhali, by the way kikubwa ni kwamba hao wanawake wanaolewa tena baadhi ya wanaume wanaowaoa nao waliwahi kuwatukana kama mnavyowatukana ninyi sasa ninyi msio masimp mna kipi ambacho hao mnaowaita masimp hawana
Mwanamke kujitunza siyo tabu ila tabu inakuja pale ambapo wanaume wanatumia kila namna kuwarubuni na kuwashawishi wanawake, halafu wanawake wakikubali wanaanza kuwatukana kuwa ni ujinga wao, kana kwamba wanawake ni malaika wana uwezo wa kukwepa majaribu siku zote
Hoja yangu ni kwamba mkitaka wanawake wajitunze basi muache kuwatongoza kama hamna malengo nao, maana yake nanyi itabidi mkubali kujitunza sababu wanawake mabikira wakisema wote waanze kujitunza, basi wanaume mtakosa wanawake wa kufanya nao hadi ndoa je mko tayari
Kama hamko tayari basi acheni huu unafiki wa kujifanya mnarekebisha jamii kwa kukemea maovu ya wanawake tu na kuyafumbia macho ya wanaume, suala la ngono linahusisha jinsia mbili huwezi kuiambia jinsia moja iache halafu nyingine iendelee hiyo logically haiwezekani ni either zote ziendelee au zote ziache, vinginevyo ni sawa na kusema zile pande mbili za shilingi upande mmoja uko sahihi kuwa pale ila mwingine hauko sahihi kuwa pale
Sawa ndio maana nikakuambia kwamba huko kwenye dating sites hakuna wanawake tu bali pia kuna wanaume, je unataka kusema na hao wanaume walioko huko wamekosa wanawake huko mitaani kwao hadi wakatafute mitandaoni, halafu nimekuambia sababu ya wanaume wa kizungu kushindwa kuoa ni sheria kali za mgawanyo wa mali baada ya talaka na siyo sababu zenu za kijinga kama hizo
Sawa ninyi ambao siyo wanaume ili mradi mna jinsia ya kiume mnawazidi nini hao mnaodai ni wanaume ilimradi wana jinsia ya kiume, nakupa mifano ya watu maarufu Hamisa Mobeto mdangaji na single mother mwenye watoto wawili wa baba tofauti kaolewa na Aziz Ki haya wewe una kipi unachomzidi Aziz Ki na unadhani yeye hajaziona hizo bikira, Ruge kabla hajaanza kuumwa hadi kufariki alikuwa kwenye mipango ya kumuoa Nandy na mahari alishatoa pamoja na video yao na Billy wakifanya yao kitandani kusambaa haya wewe una kipi cha kumzidi Ruge na unadhani yeye pia hakuziona hizo bikira, hiyo nimekutajia mifano ya watu unaowajua lakini wapo wanaume wengi tu huku mitaani usiowajua wenye akili na heshima zao wanaoa hao hao wanawake mnaodai wana past mbaya na maisha yanaendelea, sisi humu huwa tunaandika uhalisia uliopo kwenye jamii ila ninyi mnaandika matamanio yenu na mihemko halafu mkiambiwa ukweli mnapanic na kuanza kuleta personal attacks hebu tokeni kwenye hizo ndoto nyevu mje kwenye uhalisia bana
Sasa unalazimisha kitu ambacho huna uhakika nacho au una uhakika gani na unachokisema, kwa mfano hata mimi ghafla tu nikaamua kusema kwamba wewe ni shoga au marioo kwa sababu unapenda vya bure ulisema unadanga kwa mijimama nitakuwa sahihi si ndio, kuwa mtu mzima siyo kuwa na akili au busara maana kuna watu wazima wengi tu wanazeeka na upumbavu wao na wewe ukiwa mmoja wapo ila nasisitiza tu jikite kwenye mada acha kutafuta namna ya kujifariji kupitia mimi
Natamani ningewaita hapa watu ninaofahamiana nao nje ya jf ambao wananifahamu vizuri kabisa tabia zangu, nakuhakikishia ungeumbuka na ungekosa kichaka cha kujifichia lakini sijataka kwa sababu sihitaji kuprove chochote kwako, hii mitazamo nimeanza kuwa nayo toka najiunga jf nikiwa binti mdogo naanza chuo hata simjui mwanaume
Wapo wenzio kama wewe waliosema "oo huyu atakuwa single mother mara mdangaji mara feminist" na majina mengine kibao waliyoona yanafaa kunipa, tena enzi hizo jf ilikuwa ya moto kwenye mada kama hizi uzi ukianzishwa wa kuwatukana wanawake ndani ya siku mbili una comments elfu moja watu wanakesha wanabishana, mimi nikiwa kinara wa kubishana na hao wanaume design yako hata kumi kwa mpigo na wote wanakaa wanaishia kunitukana baada ya kuishiwa hoja na kama unabisha uliza uelezewe
Kuna waliojifanya wanasaikolojia uchwara na wengine walijifanya manabii feki wakanitabiria na kusema "oo baada ya miaka mitano maisha yakishakuchapa, utabadili hiyo mitazamo yako na utarudi hapa kutuomba msamaha" lakini cha ajabu ni zaidi ya miaka mitano sasa na sijabadili chochote, ndio kwanza maisha yanazidi kuninyookea na wao ndio walisalimu amri hata jf siku hizi siwaoni wakianzisha zile nyuzi zao za kijinga tena
Sasa sijui wewe ni nani ambaye unahisi haya maneno kwangu ni mageni na kwamba yataniathiri chochote, ilihali mimi kwa uzoefu wangu wa kubishana na watu kama ninyi najua hiyo huwa ni njia tu ya kujifariji kwa kumshambulia mtoa hoja baada ya kuona umeishiwa hoja, na pia nakushangaa unavyopoteza muda kwa kujihisi wewe ndio wa kwanza 'kuwaamsha' hao wanaume wenzio unaodhani hawajui wanachofanya na hao wanawake