Kitambo hiyo muajir alinitupia virago washkaj wakanishaur km vp niende mahakaman.
Nikaenda pale mnara wa saa jengo la pemben hv kuna ofis ya uwakil mule baada ya kutoa maelezo ya kina+vielelezo jamaa wakaniambia hiyo kesi unashinda fasta ila niweke 20m ubaon,nikawaambia sasa km wana uhakika nitashinda na nikishinda nitalipwa malipo mlima kwa nin wao wanataka niwalipe kabla, TUKASHINDWANA.
Wakat natoka mule ndan kuna mzee alikua kakaa kwa fundi saa pale nje akaniita na kunivuta chemba na kuanza kunipanga kuwa yey ni wakil msom tena ni sinia ameshasimamia kesi nyingi akaanza kunitolea nyaraka na vitambulisho ili kusadifu anachokisema mwishowe akataka nimueleze jambo langu.
Nikaanza kwa kumwambia kuwa sina hata mia kwa hiyo mwishowe asije akaniambia kuhusu pesa, nikamweleza mwanzo mwisho na nikamuonesha makabrasha yangu.
Yule mzee akashaur tuanze kazi mara moja kwa kufungua kesi ktk mahakama ya kazi na yey akawa ndio wakil wangu kwa makubaliano kuwa nitampa robo ya kile nitakacholipwa na mwajir.
Ikawa kila siku ya kesi tunakutana samora mkabala na jengo la harbour view nalipia kahawa aliyokunywa na safar ya mahkaman tunaenda mdogomdogo tukitoka mahakaman nampa elf tano mpaka kesi ilipoisha kwa ushind wa upande wetu.
Mungu ambarik yule mzee.
Sent using
Jamii Forums mobile app