Zijue Nyimbo zilizotengenezwa na producer Miika Mwamba

Zijue Nyimbo zilizotengenezwa na producer Miika Mwamba

Huyu mzungu ni kati ya maproducer bora kabisa waliowahi kutokea bongo fleva, zijue ngoma alizotengeneza:

1. Twenzetu - Chegge
2. Salome- Dully sykes
3. Mabinti wa Kitanga- Bwana Misosi
4. Barua - Daz Nundaz
5. Dingi na Taswira - Mandojo Domo Kaya
6. Wange na Baby gal - Mad Ice
7. Fagio la chuma - Fagio la Chuma
8. etc

Embu tajeni ngoma nyingine mnazokumbuka tumuenzi jembe letu kutoka finland. Na sasa kaacha muziki ni mkalimani.
Utakuwa hujatenda haki ikiwa Tamara ya Hard Mad hauitokuwepo kwenye hiyo list yako!!!
 
Ngoma linaaanza "Stop" let's gooooooo!!!! alafu Hapa ndiyo mwishoo mwishoooo kabisa-alisema brother man Aka misifaa alafu kwa mbali anamtaja MIIKA MWAMBAAAAAAAAAAA
Alafu MIIKA anamaliza na Dundo na vinanda makini hili goma alitendea haki sana MIIKA
 
Chidi benz ft mzee yusuf - Raha za dunia.hivi huyu jamaa anatumia jina gani kwenye social media?.

Alafu kuna mhindi alikuwa anaitwa Amit Mental alietengeneza nyimbo ya Noorah - vijimambo sjui yuko wapi huyu jamaa,kuna mwenye habari zake?
Amit alitengeneza pia Zeze ya TID, vituko uswahilini ya Suma G,
 
OCG naye yupo... ndani ya Tz na nje ya Tz.

Natumai mnakumbuka wimbo wa akwelina...
 
mikaa.jpg
Heeeh kumbe mdhungu
 
Amit alitengeneza pia Zeze ya TID, vituko uswahilini ya Suma G,
Zeze alitengeneza Bizzman. Kuna video ipo youtube akihojiwa na EAtv alisema hivyo. Aliitengezea studio za
P Funk, bongo records
 
Kuna nyimbo ya Papii kocha, kuna mahali kama anasema vile " oooh mika mwambaa eeh , mi nateswaa eeh mpenzi fantaa eee uko wapiii"
 
Back
Top Bottom