Ngoja nikusaidie kitu inawezekana kigoma huijiui vizuri
Kigoma haina umeme wa uhakika hata baada ya kuunga grid ya taifa kwa baadhi ya wilaya bado mambo yaliendelea kuwa Yale Yale ya kukatika umeme mara kwa mara, hadi jana anaingia kigoma mjini kulikua hamna umeme zaidi ya masaa ma 4 sasa sijui ni umeme upi wa uhakika unao zungumzia
Kwenye miundo mbinu ya barabara serikali imejitahidi kwa kiasi Fulani imefanya vizuri tangu kipindi cha "Mjomba", sasa hivi kuna maeneo ukifika unakuta barabara zina tengenezwa Kila siku kwa hilo naunga mkono hoja
Hapa kwenye Elimu bado kuna shida Sana, hadi Leo bado kuna shule tena za mjini watoto wanakaa chini kwenye madarasa mapya yaliyo jengwa kwa mkopo wa COVID 19, kwenye vyoo vya shule ndio usiseme kabisa ni vituko achilia mbali walimu na vifaa vya kufundishia
Kwenye maji na penyewe ni shida vile vile, japo kigoma ina ziwa Tanganyika lakini maji ni shida, kuna maeneo wana kaa hadi siku 7 bila maji yani ni mgao kwa kwenda mbele, ukienda wilaya za mbali na ziwa watu wengine huko wanategemea maji ya mito na mabwawa ambayo sio salama kwa afya zao,
kuna mradi mkubwa wa maji aliuacha magufuli, ika semekana utakua ni mwarobaini wa shida ya maji kigoma lakini shida Iko pale pale
sasa ni uhakika upi wa maji unao zungumzia wewe
Muambieni ukweli ili atatue shida za wenye nchi sio kumsifia hata kwa vitu ambavyo havipo,