Zijue sifa na gharama za kumiliki silaha Tanzania

Zijue sifa na gharama za kumiliki silaha Tanzania

Wengi
Mchakato wa kumiliki silaha ukishajaza fomu unaanzia serikali ya mtaa, kamati ya mtaa itakujadili na kukupa mukhtasari unakwenda kata, kata utajadiliwa na kamati ya ulinzi na usalama utapewa mukhtasari utakwenda kwa OCD atakuhoji atasaini fomu zako usubiri kuitwa kuhojiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya inayoongozwa na DC bahada ya hapo mapendekezo yao ndio yanapelekwa mkoa au makao makuu ya Polisi ndio unakwenda kupewa kitabu cha fire army licence.

Huo ndio mchakato wa kisheria bila kutumia rushwa kuruka stage.

Huo mchakato ulinigharimu miaka miwili mpaka kupewa kitabu cha fire army licence.
Wengi huwa wanasota sana wakifika ngazi ya wilaya na swali moja ambalo ni komon lakini ni gumu "kwa nn unataka kumiliki silaha" hapa inabidi utoe maelezo ya kutosha na kuishawishi "KUU"wilaya na ukijichanganya tuu unarudi hadi next year kule mkoani hakuna shida kwa sababu huwa ni kupitisha tuu majina yaliyotoka wlayani na kingine mhm ambacho watu hawakijui ni kuwa pamoja na kuwa ocd ndo anakuhoji na kukupa form za kujaza lakini DSO ndio mpitishaji mkuu, yaan yeye ndo huwa anapokea majina kutoka kwa ocd then kimya kimya atatuma vijana wake kupata profile yako kama unafaa au hufai kupewa chombo cha moto so siku unafika wilayani yeye anakua tayali ana info zako
 
Unajuwa kampuni za ulinzi wanalipwa bei gani kwa lindo la bunduki?

Hakuna kitu kama hicho.

Hapo inategemea na factors nyingi za Hilo LINDO maana Kuna malindo ya aina nyingi kwenye local company mengi bunduki wenyewe wanaweza Uikodi bila MTU @350,000 mpaka 450,000

Kwenye kampuni locally bunduki na mtu kwenye LINDO inaweza kua wastani 650,000 mpka 750,000 Ni tofauti na LINDO la ginnery au vituo vya mafuta mtu na bunduki inaweza kua wastani 950,000 mpaka milioni moja na laki kadhaa
 
Mbona kuna watu wanapita juu Kwa juu na wanapewa leseni ya kumiliki silaha hii ikoje
FB_IMG_1716640720560.jpg
 
Mkuu,
Lazima uiambie serikali dhumuni lako la kumiliki silaha ya Moto..

Nilikuaga mwoga Sana wa bunduki Ila nilikaaga huko kipind flani mpaka nikawa najicheka bunduki mpaka upige risasi it's a process yaan uweke risasi chemba , uweke usalama On, ndio ubonyeze trigger..

Nakumbuka tukio moja Kuna shortgun moja inayo tumia risasi za Moto Sasa risasi ikanasia ndani Ila hakuna MTU aliejua kuna risasi chemba yaan bahati mbaya mtu angegusa trigger ingekua balaa..

Kuna wengi tu Wana tafuta vibali then wanakua wanakodisha silaha kwenye makampuni ya ulinzi kwa @450,000 per bunduki monthly

All in all,
Kama hauna ulazima wa kumiliki silaha Ni Bora kuacha TU
Kuhusu risasi kunasa chemba: kila unaposhika bunduki unaambiwa ishike kwa kufuata taratibu zote unazotumia unaposhika bunduki yenye risasi. Kwa kifupi ni kuwa kwenye ku-handle bunduki, assume kuwa ina risasi na ufuate protocal zote unazofuata kwa bunduki yenye risasi. Yaani hakuna bunduki isiyo na risasi!
 
Wengi

Wengi huwa wanasota sana wakifika ngazi ya wilaya na swali moja ambalo ni komon lakini ni gumu "kwa nn unataka kumiliki silaha" hapa inabidi utoe maelezo ya kutosha na kuishawishi "KUU"wilaya na ukijichanganya tuu unarudi hadi next year kule mkoani hakuna shida kwa sababu huwa ni kupitisha tuu majina yaliyotoka wlayani na kingine mhm ambacho watu hawakijui ni kuwa pamoja na kuwa ocd ndo anakuhoji na kukupa form za kujaza lakini DSO ndio mpitishaji mkuu, yaan yeye ndo huwa anapokea majina kutoka kwa ocd then kimya kimya atatuma vijana wake kupata profile yako kama unafaa au hufai kupewa chombo cha moto so siku unafika wilayani yeye anakua tayali ana info zako
Haya yote ni kwa watu ''wakuja''. ''Watoto wa mjini'' hupelekewa leseni nyumbani.
 
Mkuu,
Hapo nazungumzia local companies mfano kule MWAKITOLIO NO.5 Kuna plant yaan bunduki bila MTU@ 350,000 mpaka 450,000 inategemea na aina ya bunduki yenyewe Ila nyingi Ni SHORTGUN

So Kuna watu nimeshuhudia Wana umiliki wa silaha kazi zao inakua Ni ku kodisha bunduki kwenye makampuni ya ulinzi kwa mikataba..

Ruksa kunikosoa ama kunirekebisha Ila Hili la kukodisha bunduki nimeli observe from EYE WITNESS ACCOUNT
Sijakataa watu kukodisha short gun kwa kampuni za ulinzi, lakini si kwa malipo hayo uliyosema, sidhani kama inazidi 100,000/= per month.
 
Kuna mmiliki bunduki yeyote amewahi kuitumia kuua majambazi ama kuzima uvamizi mahali?

Naona case nyingi wanatishatisha watu bar na mitaani na kuishia kujiuwa wao wenyewe na kuua watu kwenye ugomvi usio mbele wala nyuma.
 
Kuhusu risasi kunasa chemba: kila unaposhika bunduki unaambiwa ishike kwa kufuata taratibu zote unazotumia unaposhika bunduki yenye risasi. Kwa kifupi ni kuwa kwenye ku-handle bunduki, assume kuwa ina risasi na ufuate protocal zote unazofuata kwa bunduki yenye risasi. Yaani hakuna bunduki isiyo na risasi!
Nakubaliana nawe..
Hiyo siku jamaa alitoa risasi tano za Moto kwenye SHORTGUN chakavu akajua zimeisha kumbe Kuna moja ulikua imenasia ndani
 
Kwanza, kama unataka kumiliki silaha, lazima uwe umetimiza miaka 25. Hii ni kuhakikisha kwamba silaha zinaangukia mikononi mwa watu wazima wenye uwezo wa kufanya maamuzi ya busara
Dito alikuwa na umri gani?
 
Pesa ndogo Sana hii hope unazungumzia MAGOBOLE Yale yanayo tumia GOLOLI mkuu😊😊😊
Unajuwa mshahara wa askari security? Unajuwa wanaotowa lindo wanalipa bei gani kwa askari bila bunduki na askari mwenye bunduki?

Ukiweza kuyajuwa haya huwezi kubishana na mimi na kampuni kubwa zenye malindo makubwa ya bei kubwa wanajitosheleza hawawezi kukodi bunduki.
 
Back
Top Bottom