Zijue sifa na gharama za kumiliki silaha Tanzania

Zijue sifa na gharama za kumiliki silaha Tanzania

Maelezo ya kumiliki kibali yamejitosheleza, tunaomba maelezo ya kumiliki hiyo silaha yenyewe, Je silaha zinapatikana wapi? Na bei yake,
Pia katika matumizi au aina, Asante.
( A ) Polisi
( B ) Jeshini
( C ) Kwengineko
Kama upo Dar nenda duka la jeshi Mzinga Upanga au duka la Tanganyika Arms.

Polisi hawauzi silaha.
 
Kuna mmiliki bunduki yeyote amewahi kuitumia kuua majambazi ama kuzima uvamizi mahali?

Naona case nyingi wanatishatisha watu bar na mitaani na kuishia kujiuwa wao wenyewe na kuua watu kwenye ugomvi usio mbele wala nyuma.
Ni nadra mtu mwenye silaha kuvamiwa nyumbani, wahalifu wananusa, na wakija basi hao si majambazi bali wanakuja kukuuwa tu yani wanejiandaa kivita.

Wahalifu wa kawaida hawawezi kuvamia nyumba yenye silaha never, ndio sababu husikii matukio ya mmiliki wa silaha kupambana na majambazi hiyo ndio fact.
 
Ni nadra mtu mwenye silaha kuvamiwa nyumbani, wahalifu wananusa, na wakija basi hao si majambazi bali wanakuja kukuuwa tu yani wanejiandaa kivita.

Wahalifu wa kawaida hawawezi kuvamia nyumba yenye silaha never, ndio sababu husikii matukio ya mmiliki wa silaha kupambana na majambazi hiyo ndio fact.
📌
 
Labda driving licence ndio unaweza kuletewa nyumbani.

Fire army lazima ufike CAR mwenyewe hata kama ulitumia short cut kwenye maombi yako.
Exaggeration is a way of saying something in a funny way. Bila shaka hata hiyo leseni ya udereva watu wanaposema unapelekewa nyumbani huwa hawamaanishi ki-ukweli. Au ule msemo wa polisi trafiki kumwambia mkewe aanze kutakata nyanya na vitunguu anakwenda kutafuta mboga huku hana hata senti tano mfukoni....
 
Bora waweke iwe na masharti magumu kumiliki maana hili taifa kwasasa idadi ya vilaza ni kubwa sana na hiyo ni hatari sana kwa usalama wa raia.
 
ANGALIZO
Maelezo yaliyotolewa katika uzi huu ni kwa ajili ya kuelimisha na kutoa taarifa kwa umma na hayapaswi kutafsiriwa kama ushauri wa kisheria. Sheria za umiliki wa silaha zinaweza kubadilika, na ni muhimu kushauriana na mwanasheria au mamlaka husika kwa taarifa zaidi na za kina. Mwandishi wa uzi huu hawajibiki kwa matumizi yoyote yasiyofaa ya taarifa zilizotolewa.

View attachment 3000368
Habari zenu wapendwa wa JamiiForums,

Katika kona za mijadala na vijiwe vya mazungumzo, suala la umiliki wa silaha limeibua maswali mengi na mitazamo tofauti miongoni mwa Watanzania. Wapo wanaoamini kwamba uwezo wa kifedha na umiliki wa mali ndio vigezo vikuu vya kupata haki ya kumiliki silaha, huku wengine wakiona ada za leseni kama kikwazo kikubwa. Lakini, je, uhalisia wa sheria zetu unatuelekeza wapi katika hili?

Katika jitihada za kufafanua ukweli na kuondoa dhana potofu, nimeandaa uzi huu kwa lengo la kuelimisha na kutoa mwanga juu ya sheria za umiliki wa silaha nchini Tanzania. Ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuelewa sheria hizi, si tu kwa ajili ya kujilinda, bali pia kwa ajili ya kuchangia katika usalama wa jamii yetu. Kifungu cha 11 cha Sheria ya Umiliki na Usimamizi wa Silaha, ya mwaka 2015 kimetaja sifa za mtu anayeweza kumiliki silaha nchini Tanzania. Sifa hizo ni pamoja na;​
  1. Kwanza, kama unataka kumiliki silaha, lazima uwe umetimiza miaka 25. Hii ni kuhakikisha kwamba silaha zinaangukia mikononi mwa watu wazima wenye uwezo wa kufanya maamuzi ya busara.​
  2. Pili, lazima uwe na cheti cha uwezo. Hii ni kama mtihani wa kuonyesha kwamba unajua jinsi ya kutumia silaha kwa usalama na kwa nia njema.​
  3. Tatu, ni lazima uwe raia wa Tanzania au uwe na kibali cha ukaazi cha kudumu. Hii ina maana kwamba wageni hawawezi tu kuja na kuanza kumiliki silaha hapa nchini.​
  4. Nne, ni muhimu sana kuwa na akili timamu na usiwe na tabia ya ugomvi. Tunataka silaha ziwe mikononi mwa watu wanaoweza kudhibiti hasira zao.​
  5. Tano, usiwe tegemezi wa dawa za kulevya au narkotiki. Hii ni wazi, tunataka kuepuka hatari zinazoweza kutokea mtu akiwa chini ya ushawishi wa vitu hivi.​
  6. Sita, usiwe na rekodi ya uhalifu. Kama umewahi kufanya makosa makubwa, basi huwezi kupewa leseni ya kumiliki silaha.​
  7. Na mwisho, usiwe na ulemavu wa akili au uzembe unaoweza kukufanya ushindwe kumiliki silaha kwa usalama.​
Sheria pia inasema kwamba kuna watu wachache wanaoweza kupewa leseni ya muda ya kumiliki silaha, kama vile walinzi wa viongozi, watalii wa uwindaji, na maafisa wanaowasindikiza wafungwa. Sasa, je, mnafikiri sifa hizi zilizopo kisheria zinatosha kutulinda? Au kuna kitu kinapaswa kubadilishwa?​

Kwa upande mwingine, gharama za kumiliki silaha kisheria ni kama zifuatazo :
(a) Kwa mtu asiye mtanzania.
- Dola za Marekani 150 kwa miezi sita kwa aina yoyote ya silaha
(b) Ada ya mafunzo ya uwezo
- Shilingi 40,000/=
(c) Upimaji wa uwezo wa mara kwa mara
- Shilingi 20,000/=
(d) Gharama za kurenew leseni
- Bastola Shilingi 70,000/=
- Bunduki Shilingi 35,000/=
- Bunduki za mzigo wa mbele Shilingi 35,000/=
- Nyinginezo Shilingi 35,000/=
- Bunduki ya risasi Shilingi 35,000/=
(e) Ada ya leseni ya ghala binafsi kwa mwaka
- Shilingi 1,000,000/=
(f) Ada ya kibali cha muuzaji wa silaha kwa mwaka
- Shilingi 500,000/=
(g) Ada ya kibali cha fundi bunduki kwa mwaka
- Shilingi 500,000/=
(h) Ada ya kibali cha usafirishaji wa silaha
- Shilingi 500,000/=​

Uzi huu umechambua sheria zinazosimamia umiliki wa silaha na gharama zinazohusiana na upatikanaji wa leseni za silaha nchini Tanzania. Uchambuzi huu unalenga kutoa mwanga na kuchochea tafakuri juu ya ufanisi wa sheria hizi katika kudumisha usalama na utulivu. Ni dhahiri kwamba uelewa wa sheria hizi ni muhimu kwa kila raia, na ni jukumu letu kama wanajamii kuhakikisha tunashiriki kikamilifu katika kujenga jamii yenye amani na usalama. Ni matumaini yangu kwamba, kupitia uchambuzi huu, wadau mbalimbali watapata uelewa juu ya suala hili kisheria.​


View: https://youtu.be/keuwPn4oyx4?si=Zdr6b_61moIMFQ3C

Asante kwa elimu maana siku zote nilikua nafikiri mpaka mtu awe nama bilioni ya pesa ndio anaweza kupata leseni kumbe cheap namna hii. Barikiwa mleta uzi👏
 
Maelezo ya kumiliki kibali yamejitosheleza, tunaomba maelezo ya kumiliki hiyo silaha yenyewe, Je silaha zinapatikana wapi? Na bei yake,
Pia katika matumizi au aina, Asante.
( A ) Polisi
( B ) Jeshini
( C ) Kwengineko
Biashara ya silaha ni biashara kama zilivyo nyingine, na sheria inatoa vibali kwa watu kufanya biashara hii. Kwahiyo, wapo watu wanaouza silaha hizi kihalali kabisa bila longolongo. 👇​
IMG_20240527_190508.jpg
 
Mkuu form za maombi zinapatikanaje?
Maombi unayafanya kwa kuandika barua kwa msajili wa silaha. Lakini anatakiwa kufata hatua na taratibu zilizowekwa katika kanuni za ulinzi na udhibiti wa silaha na risasi za mwaka 2016. Taratibu hizo nikama zifufuatao:​
  1. Kuwasilisha Maombi: Mwombaji anatakiwa kuwasilisha barua ya maombi pamoja na nyaraka zote muhimu kwa Msajili wa Silaha.​
  2. Vigezo vya Msingi: Mwombaji lazima atimize vigezo vilivyotajwa kwenye kanuni ya 28, kama vile kuwa na sehemu ya kuhifadhia silaha (armoury), wafanyakazi waliofunzwa na kuthibitishwa, na kuwa mwanachama wa zamani au wa sasa wa Jeshi la Ulinzi au Serikali Kuu.
  3. Uthibitisho wa Kifedha: Mwombaji anapaswa kuonyesha uwezo wa kifedha wa kuendesha biashara hiyo kwa kuambatanisha taarifa za benki na maombi yake.​
  4. Kuidhinisha: Maombi ya mwombaji yanapaswa kuidhinishwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.​
  5. Ushauri na Bodi: Msajili atatoa kibali cha kuuza silaha baada ya kushauriana na Bodi ya Ushauri na Udhibiti wa Silaha.​
Lakini ni bora kuwasiliana na mtaalumu wa masuala ya sheria hizi ili kukusaidia kufanya zoezi hili kwa urahisi na haraka🙏​
 
Kuna mmiliki bunduki yeyote amewahi kuitumia kuua majambazi ama kuzima uvamizi mahali?

Naona case nyingi wanatishatisha watu bar na mitaani na kuishia kujiuwa wao wenyewe na kuua watu kwenye ugomvi usio mbele wala nyuma.
Ole Sendeka
 
Miaka ya nyuma huko Boko jamaa walikuja mida ya saa nane usiku, tukawashtukia mapema wao hawana habari huko nje. Walikuwa kama nane, mmoja akaja karibu na dirisha langu si nikamtisha kwa maneno " hapo hapo ulipo simama" kama vile askari mwenye siraha. Eeeh! Bwana hizo mbio siyo za mwanadamu wa kawaida....walitawanyika na kupoteana. Baadaye wakapiga risasi juu, mimi sikujibu. Ndiyo ilikuwa mwisho wetu, walitupiga kama mbwa koko na kuchukua hadi pilau yetu. Sirudii tena kuwatisha kama sina na hapa ipo.
 
Miaka ya nyuma huko Boko jamaa walikuja mida ya saa nane usiku, tukawashtukia mapema wao hawana habari huko nje. Walikuwa kama nane, mmoja akaja karibu na dirisha langu si nikamtisha kwa maneno " hapo hapo ulipo simama" kama vile askari mwenye siraha. Eeeh! Bwana hizo mbio siyo za mwanadamu wa kawaida....walitawanyika na kupoteana. Baadaye wakapiga risasi juu, mimi sikujibu. Ndiyo ilikuwa mwisho wetu, walitupiga kama mbwa koko na kuchukua hadi pilau yetu. Sirudii tena kuwatisha kama sina na hapa ipo.
😂😂😂, pole aise
 
Mchakato wa kumiliki silaha ukishajaza fomu unaanzia serikali ya mtaa, kamati ya mtaa itakujadili na kukupa mukhtasari unakwenda kata, kata utajadiliwa na kamati ya ulinzi na usalama utapewa mukhtasari utakwenda kwa OCD atakuhoji atasaini fomu zako usubiri kuitwa kuhojiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya inayoongozwa na DC bahada ya hapo mapendekezo yao ndio yanapelekwa mkoa au makao makuu ya Polisi ndio unakwenda kupewa kitabu cha fire army licence.

Huo ndio mchakato wa kisheria bila kutumia rushwa kuruka stage.

Huo mchakato ulinigharimu miaka miwili mpaka kupewa kitabu cha fire army licence.
Mbona mlolongo mrefu hivyo wakati nchi nyingine nyingi bunduki zinanunuliwa dukani kama bidhaa nyingine ya kawaida tu!
 
Back
Top Bottom