Zijue sifa na gharama za kumiliki silaha Tanzania

Mkuu kule Zanzibar sheria hairuhusu Raia kumiliki siraha ya Moto, Sasa kisheria utakuaje Tanzania Sheria ina ruhusu na Ukienda Zanzibar Sheria inakataza.
Katiba ya Jamuhuri ya Muungano iko juu ya katiba ya Zanzibar
 
Wengi

Wengi huwa wanasota sana wakifika ngazi ya wilaya na swali moja ambalo ni komon lakini ni gumu "kwa nn unataka kumiliki silaha" hapa inabidi utoe maelezo ya kutosha na kuishawishi "KUU"wilaya na ukijichanganya tuu unarudi hadi next year kule mkoani hakuna shida kwa sababu huwa ni kupitisha tuu majina yaliyotoka wlayani na kingine mhm ambacho watu hawakijui ni kuwa pamoja na kuwa ocd ndo anakuhoji na kukupa form za kujaza lakini DSO ndio mpitishaji mkuu, yaan yeye ndo huwa anapokea majina kutoka kwa ocd then kimya kimya atatuma vijana wake kupata profile yako kama unafaa au hufai kupewa chombo cha moto so siku unafika wilayani yeye anakua tayali ana info zako
Mkuu kuna sababu za kumiliki silaha zaidi ya sababu za kujilinda dhidi ya majambazi, vibaka, panya road au wahalifu wengine wowote wanaoweza kukudhuru?!
 
Huo mchakato ulinigharimu miaka miwili mpaka kupewa kitabu cha fire army licence.
Miaka miwili kutafuta chombo ambacho unaweza usikitumie maisha yako yote!!!!!!! Hii inataka moyo kwa kweli chonka...

Mimi uwa nakaa na mapanga mawili, moja sebuleni na la pili chumbani. Basi.
 
ANGALIZO
Maelezo yaliyotolewa katika uzi huu ni kwa ajili ya kuelimisha na kutoa taarifa kwa umma na hayapaswi kutafsiriwa kama ushauri wa kisheria. Sheria za umiliki wa silaha zinaweza kubadilika, na ni muhimu kushauriana na mwanasheria au mamlaka husika kwa taarifa zaidi na za kina. Mwandishi wa uzi huu hawajibiki kwa matumizi yoyote yasiyofaa ya taarifa zilizotolewa.

View attachment 3000368
Habari zenu wapendwa wa JamiiForums,

Katika kona za mijadala na vijiwe vya mazungumzo, suala la umiliki wa silaha limeibua maswali mengi na mitazamo tofauti miongoni mwa Watanzania. Wapo wanaoamini kwamba uwezo wa kifedha na umiliki wa mali ndio vigezo vikuu vya kupata haki ya kumiliki silaha, huku wengine wakiona ada za leseni kama kikwazo kikubwa. Lakini, je, uhalisia wa sheria zetu unatuelekeza wapi katika hili?

Katika jitihada za kufafanua ukweli na kuondoa dhana potofu, nimeandaa uzi huu kwa lengo la kuelimisha na kutoa mwanga juu ya sheria za umiliki wa silaha nchini Tanzania. Ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuelewa sheria hizi, si tu kwa ajili ya kujilinda, bali pia kwa ajili ya kuchangia katika usalama wa jamii yetu. Kifungu cha 11 cha Sheria ya Umiliki na Usimamizi wa Silaha, ya mwaka 2015 kimetaja sifa za mtu anayeweza kumiliki silaha nchini Tanzania. Sifa hizo ni pamoja na;​
  1. Kwanza, kama unataka kumiliki silaha, lazima uwe umetimiza miaka 25. Hii ni kuhakikisha kwamba silaha zinaangukia mikononi mwa watu wazima wenye uwezo wa kufanya maamuzi ya busara.​
  2. Pili, lazima uwe na cheti cha uwezo. Hii ni kama mtihani wa kuonyesha kwamba unajua jinsi ya kutumia silaha kwa usalama na kwa nia njema.​
  3. Tatu, ni lazima uwe raia wa Tanzania au uwe na kibali cha ukaazi cha kudumu. Hii ina maana kwamba wageni hawawezi tu kuja na kuanza kumiliki silaha hapa nchini.​
  4. Nne, ni muhimu sana kuwa na akili timamu na usiwe na tabia ya ugomvi. Tunataka silaha ziwe mikononi mwa watu wanaoweza kudhibiti hasira zao.​
  5. Tano, usiwe tegemezi wa dawa za kulevya au narkotiki. Hii ni wazi, tunataka kuepuka hatari zinazoweza kutokea mtu akiwa chini ya ushawishi wa vitu hivi.​
  6. Sita, usiwe na rekodi ya uhalifu. Kama umewahi kufanya makosa makubwa, basi huwezi kupewa leseni ya kumiliki silaha.​
  7. Na mwisho, usiwe na ulemavu wa akili au uzembe unaoweza kukufanya ushindwe kumiliki silaha kwa usalama.​
Sheria pia inasema kwamba kuna watu wachache wanaoweza kupewa leseni ya muda ya kumiliki silaha, kama vile walinzi wa viongozi, watalii wa uwindaji, na maafisa wanaowasindikiza wafungwa. Sasa, je, mnafikiri sifa hizi zilizopo kisheria zinatosha kutulinda? Au kuna kitu kinapaswa kubadilishwa?​

Kwa upande mwingine, gharama za kumiliki silaha kisheria ni kama zifuatazo :
(a) Kwa mtu asiye mtanzania.
- Dola za Marekani 150 kwa miezi sita kwa aina yoyote ya silaha
(b) Ada ya mafunzo ya uwezo
- Shilingi 40,000/=
(c) Upimaji wa uwezo wa mara kwa mara
- Shilingi 20,000/=
(d) Gharama za kurenew leseni
- Bastola Shilingi 70,000/=
- Bunduki Shilingi 35,000/=
- Bunduki za mzigo wa mbele Shilingi 35,000/=
- Nyinginezo Shilingi 35,000/=
- Bunduki ya risasi Shilingi 35,000/=
(e) Ada ya leseni ya ghala binafsi kwa mwaka
- Shilingi 1,000,000/=
(f) Ada ya kibali cha muuzaji wa silaha kwa mwaka
- Shilingi 500,000/=
(g) Ada ya kibali cha fundi bunduki kwa mwaka
- Shilingi 500,000/=
(h) Ada ya kibali cha usafirishaji wa silaha
- Shilingi 500,000/=​

Uzi huu umechambua sheria zinazosimamia umiliki wa silaha na gharama zinazohusiana na upatikanaji wa leseni za silaha nchini Tanzania. Uchambuzi huu unalenga kutoa mwanga na kuchochea tafakuri juu ya ufanisi wa sheria hizi katika kudumisha usalama na utulivu. Ni dhahiri kwamba uelewa wa sheria hizi ni muhimu kwa kila raia, na ni jukumu letu kama wanajamii kuhakikisha tunashiriki kikamilifu katika kujenga jamii yenye amani na usalama. Ni matumaini yangu kwamba, kupitia uchambuzi huu, wadau mbalimbali watapata uelewa juu ya suala hili kisheria.​

View: https://youtu.be/keuwPn4oyx4?si=Zdr6b_61moIMFQ3C

Badilisha heading iwe kumiliki bunduki.
Silaha ni zana mbalimbali mfano ngumi,kisu bastora, shotgun,fimbo,rungu,nk
 
Ni nadra mtu mwenye silaha kuvamiwa nyumbani, wahalifu wananusa, na wakija basi hao si majambazi bali wanakuja kukuuwa tu yani wanejiandaa kivita.

Wahalifu wa kawaida hawawezi kuvamia nyumba yenye silaha never, ndio sababu husikii matukio ya mmiliki wa silaha kupambana na majambazi hiyo ndio fact.
Mkuu sema vibaka siyo majambazi
 
Mkuu kule Zanzibar sheria hairuhusu Raia kumiliki siraha ya Moto, Sasa kisheria utakuaje Tanzania Sheria ina ruhusu na Ukienda Zanzibar Sheria inakataza.
Zanzibar ni nchi yenye sheria zake
 
Hii wiki ya 6 toka nilivojaza fomu na kuipeleka kwa OCD wilaya
Na nikaambiwa itajadiliwa kwenye kamati ya ulinzi na usalama wilaya na mkoa
Mpaka Leo sijapata mrejesho wowote japo nafatilia
Nawaza nisipokubaliwa na nimeshapoteza ela itakuwaje?
Wakuu hili swala linakuwaje najua umu Kuna wamiliki wa silaha
inachukuaga hata miaka mitatu mkuu
hawana haraka, na silaha unakuwa umeishailipia
 
Mchakato wa kumiliki silaha ukishajaza fomu unaanzia serikali ya mtaa, kamati ya mtaa itakujadili na kukupa mukhtasari unakwenda kata, kata utajadiliwa na kamati ya ulinzi na usalama utapewa mukhtasari utakwenda kwa OCD atakuhoji atasaini fomu zako usubiri kuitwa kuhojiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya inayoongozwa na DC bahada ya hapo mapendekezo yao ndio yanapelekwa mkoa au makao makuu ya Polisi ndio unakwenda kupewa kitabu cha fire army licence.

Huo ndio mchakato wa kisheria bila kutumia rushwa kuruka stage.

Huo mchakato ulinigharimu miaka miwili mpaka kupewa kitabu cha fire army licence.
Mlolongo mrefu sana ila ni mzuri maana wakitoa holela holela wehu wengi watamiliki
 
Hii wiki ya 6 toka nilivojaza fomu na kuipeleka kwa OCD wilaya
Na nikaambiwa itajadiliwa kwenye kamati ya ulinzi na usalama wilaya na mkoa
Mpaka Leo sijapata mrejesho wowote japo nafatilia
Nawaza nisipokubaliwa na nimeshapoteza ela itakuwaje?
Wakuu hili swala linakuwaje najua umu Kuna wamiliki wa silaha
Ngoja waje
 
Labda driving licence ndio unaweza kuletewa nyumbani.

Fire army licence lazima ufike CAR mwenyewe hata kama ulitumia short cut kwenye maombi yako.
Hebu nisaidie namna ya kupata shortcut bila usumbufu wote huo
 
ANGALIZO
Maelezo yaliyotolewa katika uzi huu ni kwa ajili ya kuelimisha na kutoa taarifa kwa umma na hayapaswi kutafsiriwa kama ushauri wa kisheria. Sheria za umiliki wa silaha zinaweza kubadilika, na ni muhimu kushauriana na mwanasheria au mamlaka husika kwa taarifa zaidi na za kina. Mwandishi wa uzi huu hawajibiki kwa matumizi yoyote yasiyofaa ya taarifa zilizotolewa.

View attachment 3000368
Habari zenu wapendwa wa JamiiForums,

Katika kona za mijadala na vijiwe vya mazungumzo, suala la umiliki wa silaha limeibua maswali mengi na mitazamo tofauti miongoni mwa Watanzania. Wapo wanaoamini kwamba uwezo wa kifedha na umiliki wa mali ndio vigezo vikuu vya kupata haki ya kumiliki silaha, huku wengine wakiona ada za leseni kama kikwazo kikubwa. Lakini, je, uhalisia wa sheria zetu unatuelekeza wapi katika hili?

Katika jitihada za kufafanua ukweli na kuondoa dhana potofu, nimeandaa uzi huu kwa lengo la kuelimisha na kutoa mwanga juu ya sheria za umiliki wa silaha nchini Tanzania. Ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuelewa sheria hizi, si tu kwa ajili ya kujilinda, bali pia kwa ajili ya kuchangia katika usalama wa jamii yetu. Kifungu cha 11 cha Sheria ya Umiliki na Usimamizi wa Silaha, ya mwaka 2015 kimetaja sifa za mtu anayeweza kumiliki silaha nchini Tanzania. Sifa hizo ni pamoja na;​
  1. Kwanza, kama unataka kumiliki silaha, lazima uwe umetimiza miaka 25. Hii ni kuhakikisha kwamba silaha zinaangukia mikononi mwa watu wazima wenye uwezo wa kufanya maamuzi ya busara.​
  2. Pili, lazima uwe na cheti cha uwezo. Hii ni kama mtihani wa kuonyesha kwamba unajua jinsi ya kutumia silaha kwa usalama na kwa nia njema.​
  3. Tatu, ni lazima uwe raia wa Tanzania au uwe na kibali cha ukaazi cha kudumu. Hii ina maana kwamba wageni hawawezi tu kuja na kuanza kumiliki silaha hapa nchini.​
  4. Nne, ni muhimu sana kuwa na akili timamu na usiwe na tabia ya ugomvi. Tunataka silaha ziwe mikononi mwa watu wanaoweza kudhibiti hasira zao.​
  5. Tano, usiwe tegemezi wa dawa za kulevya au narkotiki. Hii ni wazi, tunataka kuepuka hatari zinazoweza kutokea mtu akiwa chini ya ushawishi wa vitu hivi.​
  6. Sita, usiwe na rekodi ya uhalifu. Kama umewahi kufanya makosa makubwa, basi huwezi kupewa leseni ya kumiliki silaha.​
  7. Na mwisho, usiwe na ulemavu wa akili au uzembe unaoweza kukufanya ushindwe kumiliki silaha kwa usalama.​
Sheria pia inasema kwamba kuna watu wachache wanaoweza kupewa leseni ya muda ya kumiliki silaha, kama vile walinzi wa viongozi, watalii wa uwindaji, na maafisa wanaowasindikiza wafungwa. Sasa, je, mnafikiri sifa hizi zilizopo kisheria zinatosha kutulinda? Au kuna kitu kinapaswa kubadilishwa?​

Kwa upande mwingine, gharama za kumiliki silaha kisheria ni kama zifuatazo :
(a) Kwa mtu asiye mtanzania.
- Dola za Marekani 150 kwa miezi sita kwa aina yoyote ya silaha
(b) Ada ya mafunzo ya uwezo
- Shilingi 40,000/=
(c) Upimaji wa uwezo wa mara kwa mara
- Shilingi 20,000/=
(d) Gharama za kurenew leseni
- Bastola Shilingi 70,000/=
- Bunduki Shilingi 35,000/=
- Bunduki za mzigo wa mbele Shilingi 35,000/=
- Nyinginezo Shilingi 35,000/=
- Bunduki ya risasi Shilingi 35,000/=
(e) Ada ya leseni ya ghala binafsi kwa mwaka
- Shilingi 1,000,000/=
(f) Ada ya kibali cha muuzaji wa silaha kwa mwaka
- Shilingi 500,000/=
(g) Ada ya kibali cha fundi bunduki kwa mwaka
- Shilingi 500,000/=
(h) Ada ya kibali cha usafirishaji wa silaha
- Shilingi 500,000/=​

Uzi huu umechambua sheria zinazosimamia umiliki wa silaha na gharama zinazohusiana na upatikanaji wa leseni za silaha nchini Tanzania. Uchambuzi huu unalenga kutoa mwanga na kuchochea tafakuri juu ya ufanisi wa sheria hizi katika kudumisha usalama na utulivu. Ni dhahiri kwamba uelewa wa sheria hizi ni muhimu kwa kila raia, na ni jukumu letu kama wanajamii kuhakikisha tunashiriki kikamilifu katika kujenga jamii yenye amani na usalama. Ni matumaini yangu kwamba, kupitia uchambuzi huu, wadau mbalimbali watapata uelewa juu ya suala hili kisheria.​

View: https://youtu.be/keuwPn4oyx4?si=Zdr6b_61moIMFQ3C

Hivi aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora marehemu Ukiwaona Ditopile Mzuzuli alikuwa ana sifa zote hizo?
 
Habari, wana-JamiiForums naomba kufahamu taratibu, sheria na hatua za kufuata kuweza kumiliki silaha (Bunduki) kwa ajili ya usalama wangu.

Ningependa pia kufahamu iwapo naweza kuchagua aina ya silaha husika aidha kama ni semi-automatic pistol pekee au naweza kumiliki semi-automatic machine gun kubwa?

Nia na dhumuni la kuhitaji kumiliki silaha ni kuwa tayari kujilinda endapo ikitokea watu (wasiokuwa polisi) wakatokea kuniteka kama ambavyo matukio haya yanazidi kuongezeka na kushamiri kwa kasi.

Asante.
 
Hii wiki ya 6 toka nilivojaza fomu na kuipeleka kwa OCD wilaya
Na nikaambiwa itajadiliwa kwenye kamati ya ulinzi na usalama wilaya na mkoa
Mpaka Leo sijapata mrejesho wowote japo nafatilia
Nawaza nisipokubaliwa na nimeshapoteza ela itakuwaje?
Wakuu hili swala linakuwaje najua umu Kuna wamiliki wa silaha
Huwez poteza hela yako sababu kama umenunua dukani Silaha yako unaweza rudisha recept na kutoa maelezo kama umekosa leseni kwahyo watakata 20% ya pesa ulionunulia na nyingne kurudishiwa
 
ANGALIZO
Maelezo yaliyotolewa katika uzi huu ni kwa ajili ya kuelimisha na kutoa taarifa kwa umma na hayapaswi kutafsiriwa kama ushauri wa kisheria. Sheria za umiliki wa silaha zinaweza kubadilika, na ni muhimu kushauriana na mwanasheria au mamlaka husika kwa taarifa zaidi na za kina. Mwandishi wa uzi huu hawajibiki kwa matumizi yoyote yasiyofaa ya taarifa zilizotolewa.

View attachment 3000368
Habari zenu wapendwa wa JamiiForums,

Katika kona za mijadala na vijiwe vya mazungumzo, suala la umiliki wa silaha limeibua maswali mengi na mitazamo tofauti miongoni mwa Watanzania. Wapo wanaoamini kwamba uwezo wa kifedha na umiliki wa mali ndio vigezo vikuu vya kupata haki ya kumiliki silaha, huku wengine wakiona ada za leseni kama kikwazo kikubwa. Lakini, je, uhalisia wa sheria zetu unatuelekeza wapi katika hili?

Katika jitihada za kufafanua ukweli na kuondoa dhana potofu, nimeandaa uzi huu kwa lengo la kuelimisha na kutoa mwanga juu ya sheria za umiliki wa silaha nchini Tanzania. Ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuelewa sheria hizi, si tu kwa ajili ya kujilinda, bali pia kwa ajili ya kuchangia katika usalama wa jamii yetu. Kifungu cha 11 cha Sheria ya Umiliki na Usimamizi wa Silaha, ya mwaka 2015 kimetaja sifa za mtu anayeweza kumiliki silaha nchini Tanzania. Sifa hizo ni pamoja na;​
  1. Kwanza, kama unataka kumiliki silaha, lazima uwe umetimiza miaka 25. Hii ni kuhakikisha kwamba silaha zinaangukia mikononi mwa watu wazima wenye uwezo wa kufanya maamuzi ya busara.​
  2. Pili, lazima uwe na cheti cha uwezo. Hii ni kama mtihani wa kuonyesha kwamba unajua jinsi ya kutumia silaha kwa usalama na kwa nia njema.​
  3. Tatu, ni lazima uwe raia wa Tanzania au uwe na kibali cha ukaazi cha kudumu. Hii ina maana kwamba wageni hawawezi tu kuja na kuanza kumiliki silaha hapa nchini.​
  4. Nne, ni muhimu sana kuwa na akili timamu na usiwe na tabia ya ugomvi. Tunataka silaha ziwe mikononi mwa watu wanaoweza kudhibiti hasira zao.​
  5. Tano, usiwe tegemezi wa dawa za kulevya au narkotiki. Hii ni wazi, tunataka kuepuka hatari zinazoweza kutokea mtu akiwa chini ya ushawishi wa vitu hivi.​
  6. Sita, usiwe na rekodi ya uhalifu. Kama umewahi kufanya makosa makubwa, basi huwezi kupewa leseni ya kumiliki silaha.​
  7. Na mwisho, usiwe na ulemavu wa akili au uzembe unaoweza kukufanya ushindwe kumiliki silaha kwa usalama.​
Sheria pia inasema kwamba kuna watu wachache wanaoweza kupewa leseni ya muda ya kumiliki silaha, kama vile walinzi wa viongozi, watalii wa uwindaji, na maafisa wanaowasindikiza wafungwa. Sasa, je, mnafikiri sifa hizi zilizopo kisheria zinatosha kutulinda? Au kuna kitu kinapaswa kubadilishwa?​

Kwa upande mwingine, gharama za kumiliki silaha kisheria ni kama zifuatazo :
(a) Kwa mtu asiye mtanzania.
- Dola za Marekani 150 kwa miezi sita kwa aina yoyote ya silaha
(b) Ada ya mafunzo ya uwezo
- Shilingi 40,000/=
(c) Upimaji wa uwezo wa mara kwa mara
- Shilingi 20,000/=
(d) Gharama za kurenew leseni
- Bastola Shilingi 70,000/=
- Bunduki Shilingi 35,000/=
- Bunduki za mzigo wa mbele Shilingi 35,000/=
- Nyinginezo Shilingi 35,000/=
- Bunduki ya risasi Shilingi 35,000/=
(e) Ada ya leseni ya ghala binafsi kwa mwaka
- Shilingi 1,000,000/=
(f) Ada ya kibali cha muuzaji wa silaha kwa mwaka
- Shilingi 500,000/=
(g) Ada ya kibali cha fundi bunduki kwa mwaka
- Shilingi 500,000/=
(h) Ada ya kibali cha usafirishaji wa silaha
- Shilingi 500,000/=​

Uzi huu umechambua sheria zinazosimamia umiliki wa silaha na gharama zinazohusiana na upatikanaji wa leseni za silaha nchini Tanzania. Uchambuzi huu unalenga kutoa mwanga na kuchochea tafakuri juu ya ufanisi wa sheria hizi katika kudumisha usalama na utulivu. Ni dhahiri kwamba uelewa wa sheria hizi ni muhimu kwa kila raia, na ni jukumu letu kama wanajamii kuhakikisha tunashiriki kikamilifu katika kujenga jamii yenye amani na usalama. Ni matumaini yangu kwamba, kupitia uchambuzi huu, wadau mbalimbali watapata uelewa juu ya suala hili kisheria.​

View: https://youtu.be/keuwPn4oyx4?si=Zdr6b_61moIMFQ3C

Ngoja niagize bunduki langu
 
Back
Top Bottom