Zijue sifa na gharama za kumiliki silaha Tanzania

Maelezo ya kumiliki kibali yamejitosheleza, tunaomba maelezo ya kumiliki hiyo silaha yenyewe, Je silaha zinapatikana wapi? Na bei yake,
Pia katika matumizi au aina, Asante.
( A ) Polisi
( B ) Jeshini
( C ) Kwengineko
Kama upo Dar nenda duka la jeshi Mzinga Upanga au duka la Tanganyika Arms.

Polisi hawauzi silaha.
 
Kuna mmiliki bunduki yeyote amewahi kuitumia kuua majambazi ama kuzima uvamizi mahali?

Naona case nyingi wanatishatisha watu bar na mitaani na kuishia kujiuwa wao wenyewe na kuua watu kwenye ugomvi usio mbele wala nyuma.
Ni nadra mtu mwenye silaha kuvamiwa nyumbani, wahalifu wananusa, na wakija basi hao si majambazi bali wanakuja kukuuwa tu yani wanejiandaa kivita.

Wahalifu wa kawaida hawawezi kuvamia nyumba yenye silaha never, ndio sababu husikii matukio ya mmiliki wa silaha kupambana na majambazi hiyo ndio fact.
 
πŸ“Œ
 
Labda driving licence ndio unaweza kuletewa nyumbani.

Fire army lazima ufike CAR mwenyewe hata kama ulitumia short cut kwenye maombi yako.
Exaggeration is a way of saying something in a funny way. Bila shaka hata hiyo leseni ya udereva watu wanaposema unapelekewa nyumbani huwa hawamaanishi ki-ukweli. Au ule msemo wa polisi trafiki kumwambia mkewe aanze kutakata nyanya na vitunguu anakwenda kutafuta mboga huku hana hata senti tano mfukoni....
 
Bora waweke iwe na masharti magumu kumiliki maana hili taifa kwasasa idadi ya vilaza ni kubwa sana na hiyo ni hatari sana kwa usalama wa raia.
 
Asante kwa elimu maana siku zote nilikua nafikiri mpaka mtu awe nama bilioni ya pesa ndio anaweza kupata leseni kumbe cheap namna hii. Barikiwa mleta uziπŸ‘
 
Maelezo ya kumiliki kibali yamejitosheleza, tunaomba maelezo ya kumiliki hiyo silaha yenyewe, Je silaha zinapatikana wapi? Na bei yake,
Pia katika matumizi au aina, Asante.
( A ) Polisi
( B ) Jeshini
( C ) Kwengineko
Biashara ya silaha ni biashara kama zilivyo nyingine, na sheria inatoa vibali kwa watu kufanya biashara hii. Kwahiyo, wapo watu wanaouza silaha hizi kihalali kabisa bila longolongo. πŸ‘‡​
 
Mkuu form za maombi zinapatikanaje?
Maombi unayafanya kwa kuandika barua kwa msajili wa silaha. Lakini anatakiwa kufata hatua na taratibu zilizowekwa katika kanuni za ulinzi na udhibiti wa silaha na risasi za mwaka 2016. Taratibu hizo nikama zifufuatao:​
  1. Kuwasilisha Maombi: Mwombaji anatakiwa kuwasilisha barua ya maombi pamoja na nyaraka zote muhimu kwa Msajili wa Silaha.​
  2. Vigezo vya Msingi: Mwombaji lazima atimize vigezo vilivyotajwa kwenye kanuni ya 28, kama vile kuwa na sehemu ya kuhifadhia silaha (armoury), wafanyakazi waliofunzwa na kuthibitishwa, na kuwa mwanachama wa zamani au wa sasa wa Jeshi la Ulinzi au Serikali Kuu.
  3. Uthibitisho wa Kifedha: Mwombaji anapaswa kuonyesha uwezo wa kifedha wa kuendesha biashara hiyo kwa kuambatanisha taarifa za benki na maombi yake.​
  4. Kuidhinisha: Maombi ya mwombaji yanapaswa kuidhinishwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.​
  5. Ushauri na Bodi: Msajili atatoa kibali cha kuuza silaha baada ya kushauriana na Bodi ya Ushauri na Udhibiti wa Silaha.​
Lakini ni bora kuwasiliana na mtaalumu wa masuala ya sheria hizi ili kukusaidia kufanya zoezi hili kwa urahisi na harakaπŸ™​
 
Kuna mmiliki bunduki yeyote amewahi kuitumia kuua majambazi ama kuzima uvamizi mahali?

Naona case nyingi wanatishatisha watu bar na mitaani na kuishia kujiuwa wao wenyewe na kuua watu kwenye ugomvi usio mbele wala nyuma.
Ole Sendeka
 
Miaka ya nyuma huko Boko jamaa walikuja mida ya saa nane usiku, tukawashtukia mapema wao hawana habari huko nje. Walikuwa kama nane, mmoja akaja karibu na dirisha langu si nikamtisha kwa maneno " hapo hapo ulipo simama" kama vile askari mwenye siraha. Eeeh! Bwana hizo mbio siyo za mwanadamu wa kawaida....walitawanyika na kupoteana. Baadaye wakapiga risasi juu, mimi sikujibu. Ndiyo ilikuwa mwisho wetu, walitupiga kama mbwa koko na kuchukua hadi pilau yetu. Sirudii tena kuwatisha kama sina na hapa ipo.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚, pole aise
 
Mbona mlolongo mrefu hivyo wakati nchi nyingine nyingi bunduki zinanunuliwa dukani kama bidhaa nyingine ya kawaida tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…