Zijue sifa na gharama za kumiliki silaha Tanzania

𝗨𝗻𝗮𝗵𝗶𝘁𝗮𝗷𝗶 𝗸𝘂𝗺𝗶𝗹𝗶𝗸𝗶 𝘀𝗶𝗹𝗮𝗵𝗮

Najua watu wengi wanatamani kuweza kumiliki silaha yani mtu awe nayo kama msaada kwenye kujilinda na masuala mbalimbali lakini je unaweza kumiliki silaha?



Kwanza kumbuka maelezo ninayokupa ni kukupatia Elimu kuhusu masuala ya kumiliki silaha kihalali. Jambo muhimu zaidi kwenye sheria ya umilikaji wa silaha inaweza kubadilika hivyo ni muhimu kutembelea mamlaka husika kupata taarifa zaidi.



Wengi wanatamani kumiliki silaha lakini Kuna taratibu zake za kufuata ili uweze kuwa mtu mmoja wapo mwenye Uwezo wa kumiliki silaha. Kupitia kifungu namba 11 cha sheria za umiliki na usimamizi wa silaha ya mwaka 2015 imetaja sifa za mtu atayeweza kumiliki silaha nchini Tanzania 👇
  • lazima uwe umetimiza miaka 25 hii ni kuamini kuwa mtu anayemiliki silaha ni mtu mzima pia ana Uwezo wa kufanya maamuzi ya busara.
  • lazima uwe na Ujuzi wa kutumia silaha ni kama mtihani lazima ujue jinsi ya kutumia kwa usalama na nia njema.


  • lazima uwe raia mtanzania au uwe na kibali cha ukaazi wa kudumu
  • lazima uwe na akili timamu pia mtu ambaye sie mgomvi.
  • usiwe mtumiaji wa dawa za kulevya
  • usiwe na rekodi ya mtu aliyefanya uhalifu
  • usiwe na ulemavu wa akili au uzembe

Pia sheria imezungumzia watu wengine wenye Uwezo wa kumiliki silaha ni wanaowalinda viongozi,watalii wa uwindaji,maafisa wanaosindikiza wafungwa.



Kibali cha kumiliki silaha 👇
• mmiliki anapaswa kuinunua silaha kwenye maduka yanayotambulika na serikali
• lazima upitie serikali za mtaa wako kamati ya mtaa itaweza kukujadili Kisha kata, Kisha utapelekwa kwa OCD
• mmiliki lazima uwende na risiti uliyonunulia silaha kwenye kituo cha polisi cha wilaya utakabidhiwa fomu na kujaza
• Fomu ya mmiliki itajadiliwa kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya akishapitishwa itapelekwa kweye kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa
• Mmiliki atapatiwa kibali na kasha kuruhusiwa kwenda kuchukua silaha yake kwenye duka halali alilonunulia

Gharama za kumiliki silaha zinaanzia dola 150 kwa raia ambaye sio mtanzania
 
Kuna tetesi zinasema kipindi Cha Uchaguzi nyote mnarudisha bomba mpaka Hali iwe shwari. Je Kuna ukweli kuhusu hili.
 
Zanzibar ni nchi na inasheria zake, ungesema Ukerewe hawaruhusu ndio ingekuwa hoja.
Hivi zanzibar ina jeshi?,na je kama haina inawezekanaje kuwa nchi yenye raisi bila jeshi?
Ama ni kijiji cha zanzibar🤷‍♂️
 
Mkuu nahitaji kufahamu mawili matatu kama hutojali
 
Nilikuaga mwoga Sana wa bunduki Ila nilikaaga huko kipind flani mpaka nikawa najicheka bunduki mpaka upige risasi it's a process yaan uweke risasi chemba , uweke usalama On, ndio ubonyeze trigger
Umetudanganya!
Mpaka upige risasi lazima kwanza safety lever (hiyo unayosema Usalama) iwe opened kwanza, koki( kuweka Chemba) then ndo u pull trigger. In most firearms huwezi kuweka Chemba without opening first the safety lever
 
Umetudanganya!
Mpaka upige risasi lazima kwanza safety lever (hiyo unayosema Usalama) iwe opened kwanza, koki( kuweka Chemba) then ndo u pull trigger. In most firearms huwezi kuweka Chemba without opening first the safety lever
Ukisoma maelezo nilielezea process Ila sijasema ipi inaanza au kufuata Ila ndizo principal zinazo ongoza kwenye kufyatua RISASI pia Silaha / bunduki zipo aina tofauti tofauti mkuu.

Wakati mwingine tusijifanye wajuaji na malimbukeni au mazumbukuku kujifanya ujuaji mwingi mfano.
Kuna SHORT GUN zinatumia RISASI ZA MOTO na KUNA ZINATUMIA RISASI ZA GOROLI SO KUNA SHORT GUN MOJA ILIKUA INATUMIA RISASI ZA MOTO KWENYE KUZITOA ZILE RISASI MOJA IKABAKIA/ NASIA CHEMBA IKAJULIKANA ZOTEEE ZIMETOKA KILICHO TOKEA kugusa trigger usalama ukawa upo off so ndicho kilicho saidia..
 
Maisha bhana umenikumbusha mwakitolyo mkuu.
 
Hapana anapokuja mh.Rais mkoa husika ndio wote mnatakiwa kuzikabidhi polis mpaka atakapoondoka ndio mnarudishiwa tena
Ikitokea mtu ana silaha na ayupo amesafiri mkoa mwingine inakuaje!!!?
 
Tuna zinunua wapi sasa?

Na bei ni ipi kwa aina zinazoruhusiwa?

Je kuna sheria za kumiliki silaha zingine au ni bunduki tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…