Zijue taasisi ambazo hazipokei rushwa hata kwa mtutu wa bunduki

Zijue taasisi ambazo hazipokei rushwa hata kwa mtutu wa bunduki

Tanzania kumejaa rushwa, sehemu nyingi huwezi kupata huduma bila rushwa. Pamoja na hilo Kuna baadhi ya taasisi ambazo hata utoe rushwa ya bilioni mia huwa hawapokei kabisa. Baadhi ni hizi hapa.

1. Tanesco - hawa jamaa Wana maadili Sana na kazi zao, ukienda kuomba kuanganishiwa umeme hawatakuomba hata sh 10, hata ikitokea Dewji na yeye anataka huduma watakusikiliza kwanza wewe wa kwanza halafu Dewji atawekwa foleni.

2. Idara za maji za mikoa tofauti tofauti - hawa ni Kama Tanesco- hawana shida kabisa.

3. Uhamiaji - ukienda kufuatilia pasi ya kusafiria, nakuhakikishia huwezi kutoa hata sumni, utapata huduma zako zote ndani ya muda na bila mazingira ya rushwa.

4: Traffic polisi - hawa huwa hawana mambo mengi Kama una kosa watakupiga faini, Kama Haina kosa lolote watakuachia. Hawezi kuchukua hela yako wala kukusingizia kosa lolote, nawapongeza kwa hilo.

Wakuu ipi taasisi ambayo umewahi kupata huduma bila kutoa rushwa kabisa. Tuwapongeze.
Walimu wangekuwa wanatumia mbinu kama hizi katika kufundisha hakika wahitimu waliojiajiri wangekuwa wengi zaidi
 
Mie kusema kweli ningeiweka TASAC kama ya kwanza kabisa. wako vyema sana hawa watu.
Japo Mama SSH ameshabariki kuiondoshea baadhi ya majukumu yake, ila yajayo ni vichekesho

Hakika umenena TASAC wako vizuri sana walitakiwa kuwepo nafasi nzuri tu kwenye list ya mleta mada
 
We jamaa uko nchi gani?
Au mimi ndo sijaelewa mwandiko wako umekaa kinyume nyume yaani umeandika kwa codes mpaka mtu atazamishe maandishi kwenye kioo ndio aelewe?
Anyway hapo kwenye list yako umewasahau manesi wa hospital za serikali hawa "hawanaga" mambo ya rushwa kabisa yaani wanakusikiliza vizuri na kukujali utapewa huduma nzuri mpaka upone hata kabla ya kumeza dawa
Pia kuna hawa viumbe wa kuitwa police hawanaga mambo ya rushwa kabisa wala njaa za vihela vyenu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Halafu jamaa kawasahau TRA yaani hawa ndo huwezi kusikia kabisa wakija kukudaria biashara yako watakupa stahiki yako bila taabu, mfano kama ulitakiwa kukadiriwa 388000 kwa mwaka watakwambia 1600000 kwa mwaka hata ujipendekeze vipi kuwapa chochote ili upungunziwe hawatakuelewa.

Bado kuna maafisa mikopo wa bank,huna vigezo vya kukopa husika watakushauri uvipate kwanza ndo uje ukope

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Hongera zao! Wajengewe sanamu po pote pale Tanzania.
Siku wakiacha rushwa ujue CCM itakuwa imeshakabidhi madaraka.
 
Back
Top Bottom