Tanzania kumejaa rushwa, sehemu nyingi huwezi kupata huduma bila rushwa. Pamoja na hilo Kuna baadhi ya taasisi ambazo hata utoe rushwa ya bilioni mia huwa hawapokei kabisa. Baadhi ni hizi hapa.
Tanesco- hawa jamaa Wana maadili Sana na kazi zao, ukienda kuomba kuanganisshiwa umeme hawatakuomba hata sh 10, hata ikitokea Dewji na yeye anataka huduma watakusikilizq kwanza wewe wa kwanza halafu Dewji atawekwa foleni.
2. Idara za maji za mikoa tofauti tofauti- hawa Ni Kama tanesco- hawana shida kabisa.
3. Uhamiaji- ukienda kufuatilia pasi ya kusafiria, nakuhakikishia huwezi kutoa hata sumni, utapata huduma zako zote ndani ya muda na bila mazingra ya rushwa.
4: Traffic polisi- hawa huwa hawana mambo mengi Kama una kosa watakupga faini, Kama Haina kosa lolotewatakuachia. Hawezi kuchukua hela yako wala kukusingizia kosa lolote, nawapongeza kwa hilo.
Wakuu ipi taasisi ambayo umewahi kupata huduma bila kutoa rushwa kabisa. Tuwapongeze.