Zijue taasisi ambazo hazipokei rushwa hata kwa mtutu wa bunduki

Zijue taasisi ambazo hazipokei rushwa hata kwa mtutu wa bunduki

294064359_5183275751779296_2053035389600415542_n.jpg
 
Mapesa ya laana hayo ndio maana watu mnapata strokes mnajifia hovyo hovyo.

Milaana ya ajabu ajabu ya kudhulumu watu.

Nature comes back to you with a fierce KARMA.
PESA ZA MASIKITIKO IS A CURSE WENGI HAWAFAHAMU HILI, unapokea huku mtoaji analia ni laana, kibaya upepo mchafu huwakumba familia ya mla rushwa, watashiba sana lakini Subiri tu. Kama sio kizazi hicho kuumia basi hata kijacho!
 
Tanzania kumejaa rushwa, sehemu nyingi huwezi kupata huduma bila rushwa. Pamoja na hilo Kuna baadhi ya taasisi ambazo hata utoe rushwa ya bilioni mia huwa hawapokei kabisa. Baadhi ni hizi hapa.

Tanesco- hawa jamaa Wana maadili Sana na kazi zao, ukienda kuomba kuanganisshiwa umeme hawatakuomba hata sh 10, hata ikitokea Dewji na yeye anataka huduma watakusikilizq kwanza wewe wa kwanza halafu Dewji atawekwa foleni.

2. Idara za maji za mikoa tofauti tofauti- hawa Ni Kama tanesco- hawana shida kabisa.

3. Uhamiaji- ukienda kufuatilia pasi ya kusafiria, nakuhakikishia huwezi kutoa hata sumni, utapata huduma zako zote ndani ya muda na bila mazingra ya rushwa.

4: Traffic polisi- hawa huwa hawana mambo mengi Kama una kosa watakupga faini, Kama Haina kosa lolotewatakuachia. Hawezi kuchukua hela yako wala kukusingizia kosa lolote, nawapongeza kwa hilo.

Wakuu ipi taasisi ambayo umewahi kupata huduma bila kutoa rushwa kabisa. Tuwapongeze.
Ongeza na mahakama, Yani burudani Yani.
 
PESA ZA MASIKITIKO IS A CURSE WENGI HAWAFAHAMU HILI, unapokea huku mtoaji analia ni laana.
Hizi KANUNI ZA ASILI huwa sio za maskhara hata kidogo.

Litakupata jambo zito wala hutajua limetoka wapi....

Unapigwa stroke unabaki kulia lia tu oooh nimerogwaa... kumbe ulidhulumu watu.

Tunakuzika tunaendelea kutafuna kitimoto na bia. CASE CLOSED.
 
Nadhani Takukuru ingeanzisha shindano tukawa tunapigia kura ili mshindi akawa anapata tuzo na wafanyakazi wake kupongezwa kwa namna fulani ya zawadi za kukumbukwa.
 
Uhamiaji kote majanga..makao makuu nje wana vishoka wao ,ukishalipa unaelekezwa then afisa anapigiwa simu ...mipakani ndio kabisa .bus likikaribia mpakani konda anauliza Kama huna passport umwone ..
 
1. RITA.

Huwezi kupata cheti cha kuzaliwa au kifo kwa shortcuts. Lazima ufuate hatua zote... lazima uambatanishe vielelezo vyote. huwez eti kutoa rushwa upewe cheti wakati huna leaving certificates, baptism certificate, voter ID etc...

2. NIDA.

Nani anaweza kupata au mtumishi gani anaweza kupokea rushwa ili akupe kitambulisho cha nida au namba bila hujajaza taarifa zako zinazotakiwa?
 
MAHakama na polisi Kuna mabango kibao, hatupokei Wala usitoe rushwa, lakini huko ndio makao makuu ya rushwa

Back
Top Bottom