Zijue tabia za Kanisani

Zijue tabia za Kanisani

Umewahi kumshuhudia nani akitazama ngono kanisani?? Au evidence yako ni ipi?? Au unatoa hoja kufurahisha watu.
Kanisani kwetu tunazima,Simu sio sahihi ibadani,ni rahisi mtu kutoka nje ye ibada akiperuzi yake
 
Kwanini tupimiane kiwango cha maombi? Kwanini nikatishiwe sala yangu?
Mungu wetu sio Mungu wa machafuko, kumbuka kuna kiongozi wa maombi hivyo uwe makini kufuata maelekezo yake
 
Kwa akina dada vaa nguo yenye kusitiri mwili wako, ficha matiti yako na usionyeshe mapaja na matako yako ukiwa kanisani - haswa ikiwa umeketi mbele au unaongoza nyimbo za sifa na ibada. Kwa nini umkengeushe nabii na waabudu wengine?

Ukiwa kanisani, zima simu yako. Epuka kutafuna big G. Na usitupe takataka kanisani.

Ukiwa na changamoto ya kusikia usingizi wakati wa ibada, kaa safu ya katikati nyuma kabisa. Unaweza pia kupiga miayo huko.

Acha kuwatazama watu wanapoomba na kusifu - wewe pia umeenda kanisani kuabudu na kusifu hivyo sifu na uombe kama wao.

Acha kuchezea kurasa za biblia hovyo hovyo maana kufanya hivyo ni kukosa adabu - unaweza kufanya hivyo kibinafsi ukiwa nyumbani kwako.

Tafadhali jali watoto wanaolia. Usiondoke kabla ibada haijamaliza, isipokuwa kama utapata dharura.

Kama lilivyo shirika lingine lolote, kanisa pia lina bili - usiende kanisani mikono mtupu nenda na sadaka.

Ikiwa hujui kuimba ama huwa unaimba off-tune kama mimi, tafadhali punguza sauti yako[emoji1787]

Wengine wakimaliza kuomba tafadhali nyamaza. Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko (1Kor 14:33).

Kwa wanandoa, peaneni mabusu mkiwa nyumbani au kwenye gari na sio ibadani.

Nakutakia ibada njema.

Ubarikiwe.
Bonge la meseji, naomba niikopi na ku-share kwenye social groups tafadhali
 
Back
Top Bottom