Pre GE2025 Zikiwa zimesalia siku chache, Wadau wazidi kuunga Mkono Maandamano ya Amani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Huku kukiwa Tayari kumetolewa ratiba kamili ya maandamano ya Chadema na Wananchi , ili kupeleka ujumbe duniani wa kushinikiza kuondolewa kwa miswada mibovu ya Sheria za Uchaguzi bungeni , Tayari lundo la Wadau wameunga Mkono jambo hilo wakiwemo Waandishi wa habari



Hesabu ya leo inaonyesha kwamba zimesalia siku 6 tu kabla ya Wananchi kuingia barabarani kwa amani



Taarifa nyingine zikionyesha kwamba mipango yote kuhusu Maandamano hayo yanayotarajiwa kuvunja rekodi ya mahudhurio imekamilika , huko Freeman Mbowe akiendelea kukutana na Wanadiplomasia wa dunia , huku akianza na Marekani , Kesho Uingereza



Usiondoke JF , kwa vile mimi mtumishi wenu nitakuwepo kwa ajili ya kuhakikisha hamupitwi na lolote kuhusu uhondo huu
 
Wadau wa Mwakaleli
 
Hamuwezi kuandamana ninyi na hakuna mtu mwenye akili timamu anao uwezo wa kuwaunga mkono chadema,ukiangalia kwa jicho pevu utagundua kuwa maeneo waliyotangaza kuanza maandamano yao chadema ni maeneo ambayo kuna Panya Road,so chadema anategemea sapoti ya vibaka kuhujumu nchi.
 
Aisee🤣
 
Unaogopa Nini wewe, waache waandamane na watoe dukuduku zao, kama maoni yao yanatija basi miswada irekebishwe, ccm na serikali mnaogopa Nini? Kupinga maandamano kunaashiria miswada hiyo haina tija kwa taifa
 
Hakuna sisimizi au pimbi yeyote wa CHADEMA atakayeandamana. Hawa wanafanya trending tu kwenye social media. Waoga hawana mfano
 
Hakuna maandamano, dalali hana nguvu hiyo
 
Haya Maandamano yanawahusu Watanzania wote wenye kujielewa.
Kipimo cha kujielewa siyo lazima uandamane. Kenya baada ya ushindi wa Rutto wameandamana sana, je kule ndiyo kujielewa?

Wewe unapoona CHADEMA wanadai KATIBA mpya, unadhani wana uchungu na mwananchi?

Sahau hiyo. Viongozi wa CHADEMA wanataka kutumia wananchi kuingia madarakani lakini nakuhakishia kuwa ni mafisadi kuliko hata hii CCM unayoiona. Waangalie tu kwenye ranks zao ni nani amewahi kuachia kiti chake kwa mChadema mwingine. Miaka yote ni hao hao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…