Pre GE2025 Zikiwa zimesalia siku chache, Wadau wazidi kuunga Mkono Maandamano ya Amani

Pre GE2025 Zikiwa zimesalia siku chache, Wadau wazidi kuunga Mkono Maandamano ya Amani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kipimo cha kujielewa siyo lazima uandamane. Kenya baada ya ushindi wa Rutto wameandamana sana, je kule ndiyo kujielewa?

Wewe unapoona CHADEMA wanadai KATIBA mpya, unadhani wana uchungu na mwananchi?

Sahau hiyo. Viongozi wa CHADEMA wanataka kutumia wananchi kuingia madarakani lakini nakuhakishia kuwa ni mafisadi kuliko hata hii CCM unayoiona. Waangalie tu kwenye ranks zao ni nani amewahi kuachia kiti chake kwa mChadema mwingine. Miaka yote ni hao hao
Wananchi wakiamua kuwapa nafasi ya uongozi CHADEMA huna la kufanya.
 
CCM Wana choice mbili,

1.Kuzuia maandamano wakose misaada.

2.Kuahirisha usafi wa jamaa zetu.

Nionavyo, usafi utaahirishwa.

Wananchi wajitokeze Kwa wingi kuandamana.

Maandamano Yana Raha yake, hata njaa huwezi ihisi.

Mungu ibariki Nchi yangu niipendayo TANZANIA.๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

Mungu bariki maandamano ya Amani,

Mungu ibariki CHADEMA.

Amen
 
Hiki ni kiwango kidogo sana cha uelewa wa mambo!! We endelea na maisha yako.
Twende kwa hoja na siyo sweeping statements. Mukizidiwa hoja mnaishia kuandika kejeli
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Hakuna maandamano yatakayofanyika wala kutokea .ninyi endeleeni na porojo zenu tu maana watanzania wapo Bize na CCM tu kwa sasa.
IMG-20240119-WA0008.jpg
IMG-20240119-WA0014.jpg
IMG-20240119-WA0013.jpg
IMG-20240119-WA0015.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Huku kukiwa Tayari kumetolewa ratiba kamili ya maandamano ya Chadema na Wananchi , ili kupeleka ujumbe duniani wa kushinikiza kuondolewa kwa miswada mibovu ya Sheria za Uchaguzi bungeni , Tayari lundo la Wadau wameunga Mkono jambo hilo wakiwemo Waandishi wa habari

View attachment 2875569

Hesabu ya leo inaonyesha kwamba zimesalia siku 6 tu kabla ya Wananchi kuingia barabarani kwa amani

View attachment 2875570

Taarifa nyingine zikionyesha kwamba mipango yote kuhusu Maandamano hayo yanayotarajiwa kuvunja rekodi ya mahudhurio imekamilika , huko Freeman Mbowe akiendelea kukutana na Wanadiplomasia wa dunia , huku akianza na Marekani , Kesho Uingereza

View attachment 2875574

Usiondoke JF , kwa vile mimi mtumishi wenu nitakuwepo kwa ajili ya kuhakikisha hamupitwi na lolote kuhusu uhondo huu
Hamasi watapinga.
 
Hamuwezi kuandamana ninyi na hakuna mtu mwenye akili timamu anao uwezo wa kuwaunga mkono chadema,ukiangalia kwa jicho pevu utagundua kuwa maeneo waliyotangaza kuanza maandamano yao chadema ni maeneo ambayo kuna Panya Road,so chadema anategemea sapoti ya vibaka kuhujumu nchi.
Panic ya hali ya juu.

Poleee
 
Back
Top Bottom