Ziko wapi fursa za mitaji kwa vijana wenye mawazo yenye tija kwa jamii na dunia?

Ziko wapi fursa za mitaji kwa vijana wenye mawazo yenye tija kwa jamii na dunia?

TRABSOH

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
351
Reaction score
559
Wakuu habari!
Mimi ni kijana wa makamo nimekuwa nikiona mtandaoni kwa mataifa ya Europe na Asia kukiwa na makampuni mengi yanayojihusisha na shughuli za fundraising kwa miradi na mawazo ya kibiashara yenye tija kwa jamìi na ulimwengu na kuwasaidia vijana kufikia malengo yao huku wakiongeza ajira na kupunguza ugumu wa maisha kwa watu wa mataifa yao kwa kutoa ajira na fursa zingine zitokanazo na shughuli ZA biashara au miradi yao.

Lakini kwa mazingira yetu naona miradi mingi inayowezeshwa ni Ile inayoanzishwa na taasisi za serikali au NGO ninaelewa kwasababu wanaaminika zaidi.
Lakini kimsingi kwa taratibu zetu kisheria na hali ya uchumi ni ngumu kwa vijana wengi wahitimu au wa mtaani wenye umri wa miaka 18 -30 kuweza kuunda kampuni na kusajili au kuweza kuunda na kusajili NGO ili waweze kuyafanya mawazo yao kuaminika kuwezeshwa kifedha au kwa vifaa japo natambua WaPo wenye uwezo huo lakini wengi hatuna ubavu huo.
Mimi nina mradi wangu ninaotamani kuwezeshwa kwa vifaa na eneo Ili niweze kuuendesha na utakuwa na tija kwa jamii na kwa mazingira pia kwa kiasi kikubwa lakini kwasabbu sina mtaji na mashirika mengi yanayotoa nafasi ya uwezeshaji kifedha yanazingatia sana miradi iliokwisha kuanza na mimi siwezi kuanza kwasababu sina pa kuanzia.
Kwahiyo nmekuja kwenu kutaka kufahamishwa kufunguliwa macho juu ya fursa za mitaji kwa vijana wenye mawazo yenye tija kwa jamii na dunia aidha kwa mashindano au kwa kupitia uchujaji wa wazo husika na tija zake na uwezekano wa utekelezaji wake. Umaskini mbaya wapendwa
Asanteni natumaini WaPo wa kunifungua macho!
 
Mkuu wangu serikali ya CCM haipo Kwa ajili ya vijana ipo Kwa ajili ya wao Kwa wao na familia zao na Koo zao,

Hata wakiwekaa mikopo Kwa vijanaa mpk iwafikie aiseee n mlolongo mrefu km kuizunguka Dunia 🤔🤔🤔
 
Back
Top Bottom