Zile dola milioni 30 zilizokutwa nyumbani kwa Magufuli ziliishia wapi?

Zile dola milioni 30 zilizokutwa nyumbani kwa Magufuli ziliishia wapi?

Katika zama hizi za mitandao ya kijamii, simu za viganjani zenye kila aina ya uwezo, zenye kuweza kupiga picha, kurekodi video, na kadhalika, ni vigumu sana kwa baadhi ya mambo kuendelea kuwa siri.

Tuliambiwa kwamba, baada ya Rais Magufuli kufariki, kwamba nyumbani kwake zilikutwa dola za Kimarekani milioni 30.

Sipati picha dola za Marekani milioni 30, zilizo taslimu, zinaweza kujaza magunia mangapi au masanduku mangapi au maboksi mangapi!

Hii ilikuwa ni miaka michache tu iliyopita. Ilikuwa ni 2021!

Mpaka leo hii sijawahi kuona ushahidi wowote ule ulio wa moja kwa moja au wa kimazingira.

Kwamba yakutwe mahela yote hayo nyumbani kwa Magufuli halafu asiwepo hata mtu mmoja mwenye simu janja kuweza kupiga picha au kurekodi video ya hayo mahela?

Haya, tusogeze muda mbele mpaka leo.

Watu ambayo miaka minne iliyopita tulikuwa hata hatuwajui, ila leo hii wamepata madaraka huko serikalini na tumeishia kuwajua kupitia mitandao ya kijamii kutokana na matendo yao ya kuonyesha utajiri wao!

Sikumbuki enzi za Magufuli kumuona mtu yeyote yule aliyekuwepo serikalini au kuwaona watoto wake, wakionyesha mabulungutu ya mahela waliyonayo.

Nakumbuka kipindi cha Magufuli, kuna mke wa waziri mmoja mwandamizi alimletea ukorofi askari mmoja wa barabarani.

Taarifa zilipomfikia Magufuli, kuna siku moja akalizungumzia hadharani hilo suala na akalikemea.

Leo hii huyu Rais tuliyenaye anaweza akamkemea nani kuhusu ufisadi, muonekano wa ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka, n.k.?

Mtu kama huyu hapa kwenye picha, anaonekana ni mtoto wake 2006 au 07, anatoa wapi jeuri ya kuonyesha mahela aliyonayo?

Pamoja na mapungufu yake yote, enzi za Magufuli hatukuona upumbavu na dharau kama hizi.

Jesca na yule kaka yake sidhani kama wamewahi kushika hata kibulungutu cha dola 10,000 tu.

Mke wa Magufuli sidhani hata kama anajua dola ni kitu gani…..
Hiyo claim ilikuwa completely nonsensical. Kama kifo chake kingetokana na military coup d'état angalau kungekuwa na sababu ya kuamini kwamba nyumba yake ilikuwa searched baada ya kifo chake!
 
Tatizo la Lissu hawezagi kuchuja mambo Ayo ndo mapungufu yake yeye waliaminisha Magufuli alikua mbaya wake wanamtandao ni watu hatari walimtumia mpaka Lissu na iko siku wanamtandao watawagombanisha Lissu na Polepole niko hapa
Ni kweli alikuwa mbaya kweli kwake.

Risasi 46 kama anaua chatu, Magu alikuwa Joka shetani.

Postive side ya Magufuli ilikuwa kwenye miundombinu tu.
 
Ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya ila wanamtandao walimuua kwanza alafu ndo wakampa jina baya ili watu wasiulize
 
Ni kweli alikuwa mbaya kweli kwake.

Risasi 46 kama anaua chatu, Magu alikuwa Joka shetani.

Postive side ya Magufuli ilikuwa kwenye miundombinu tu.
Ww ulikuwepo!? Et risasi 46, watanzania majinga sana, Yani nyie ukombozi mtausikia kwa nchi nyingine Yani upo brainwashed mnaishi kwa nadharia ambazo hazipo (propaganda at its best).
 
Ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya ila wanamtandao walimuua kwanza alafu ndo wakampa jina baya ili watu wasiulize
Nilitaka nikupe mimba nimengaili sometimes una akili
 
Ni kweli alikuwa mbaya kweli kwake.

Risasi 46 kama anaua chatu, Magu alikuwa Joka shetani.

Postive side ya Magufuli ilikuwa kwenye miundombinu tu. MIMI pia nilimpigia sana spana Magufuli but nilikuja kugundua na mimi nilitumiwa na wanamtandao bila kujua naomba nisamehewe but Magufuli hakua mbaya
 
Ni kweli alikuwa mbaya kweli kwake.

Risasi 46 kama anaua chatu, Magu alikuwa Joka shetani.

Postive side ya Magufuli ilikuwa kwenye miundombinu tu.
Umejuaje kama Magu ndiye aliyetoa amri?

Mkapa, kijazi, Mbuge, Mfugale kufa; nayo ilikuwa amri ya Magu? Unakumbuka hawa wote walikuwa na uhusiano gani?

Unafahamu kundi gani bado wapo hai, kasoro wawili?
 
Umejuaje kama Magu ndiye aliyetoa amri?

Mkapa, kijazi, Mbuge, Mfugale kufa; nayo ilikuwa amri ya Magu? Unakumbuka hawa wote walikuwa na uhusiano gani?

Unafahamu kundi gani bado wapo hai, kasoro wawili?
Kwasababu hakujishughulisha kutafuta waliofanya unyama, alimtumia Ndugai kuzima kamati ya bunge ya uchunguzi na alimnyima haki zake kama Mbunge.

Hii ni logic tu wala huhitaji kuwa ndugu wa Lissu kujua Magu ndio alitaka kumuua Lissu.

Na Lissu ana Mungu sana, wanakufa vibaya sanaaaa, wanamuacha
 
Kwasababu hakujishughulisha kutafuta waliofanya unyama, alimtumia Ndugai kuzima kamati ya bunge ya uchunguzi na alimnyima haki zake kama Mbunge
Inawezekana ilikuwa ni maamuzi za Ndugai tuu.

Magu kutokujishughulisha inaweza kuwa ni moja ya zile tabia zake mbofu za kuwa insensitive kwa wale aliowaona wanapunguza kasi ya maendeleo. Unakumbuka alivyowajibu hovyo wahanga wa mafuriko?
Hii ni logic tu wala huhitaji kuwa ndugu wa Lissu kujua Magu ndio alitaka kumuua Lissu.

Na Lissu ana Mungu sana, wanakufa vibaya sanaaaa, wanamuacha
Mungu atupe uhai tuu, haya yote yatajidhihirisha.
 
Kwamba kwasababu tuhuma dhidi ya Magu hazikuanikwa mitandaoni sana ukilinganisha na tuhuma dhidi ya Mama ndiyo kielelezo kwamba Magufuli alikua bora kuliko Mama ktk kukemea/kupambana na ufisadi? Sidhani. Sikuwahi kumuunga mkono Magufuli kwa ujumla, japo nakiri kuna baadhi ya sera zake zilikua na matokeo chanya kwa umma kwa ujumla, at least temporarily. Ila ninaamini huwezi kumsafisha Magu kwa mapungufu ya Mama.
 
Back
Top Bottom