Katika zama hizi za mitandao ya kijamii, simu za viganjani zenye kila aina ya uwezo, zenye kuweza kupiga picha, kurekodi video, na kadhalika, ni vigumu sana kwa baadhi ya mambo kuendelea kuwa siri.
Tuliambiwa kwamba, baada ya Rais Magufuli kufariki, kwamba nyumbani kwake zilikutwa dola za Kimarekani milioni 30.
Sipati picha dola za Marekani milioni 30, zilizo taslimu, zinaweza kujaza magunia mangapi au masanduku mangapi au maboksi mangapi!
Hii ilikuwa ni miaka michache tu iliyopita. Ilikuwa ni 2021!
Mpaka leo hii sijawahi kuona ushahidi wowote ule ulio wa moja kwa moja au wa kimazingira.
Kwamba yakutwe mahela yote hayo nyumbani kwa Magufuli halafu asiwepo hata mtu mmoja mwenye simu janja kuweza kupiga picha au kurekodi video ya hayo mahela?
Haya, tusogeze muda mbele mpaka leo.
Watu ambayo miaka minne iliyopita tulikuwa hata hatuwajui, ila leo hii wamepata madaraka huko serikalini na tumeishia kuwajua kupitia mitandao ya kijamii kutokana na matendo yao ya kuonyesha utajiri wao!
Sikumbuki enzi za Magufuli kumuona mtu yeyote yule aliyekuwepo serikalini au kuwaona watoto wake, wakionyesha mabulungutu ya mahela waliyonayo.
Nakumbuka kipindi cha Magufuli, kuna mke wa waziri mmoja mwandamizi alimletea ukorofi askari mmoja wa barabarani.
Taarifa zilipomfikia Magufuli, kuna siku moja akalizungumzia hadharani hilo suala na akalikemea.
Leo hii huyu Rais tuliyenaye anaweza akamkemea nani kuhusu ufisadi, muonekano wa ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka, n.k.?
Mtu kama huyu hapa kwenye picha, anaonekana ni mtoto wake 2006 au 07, anatoa wapi jeuri ya kuonyesha mahela aliyonayo?
Pamoja na mapungufu yake yote, enzi za Magufuli hatukuona upumbavu na dharau kama hizi.
Jesca na yule kaka yake sidhani kama wamewahi kushika hata kibulungutu cha dola 10,000 tu.
Mke wa Magufuli sidhani hata kama anajua dola ni kitu gani…..