ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Jamani natafuta wimbo wa OMARI MKALI wimbo wa kitambo kidogo unaitwa Kibuyu, hapa nina uhakika kuna kila aina ya watu natumaini nitaupata mwenye nao nauomba tafadhali.
 
Huu wimbo nimeutafuta toka 2005 mpaka leo sijaupata. vipi ntaupataje?!
 
Huu wimbo nimeutafuta toka 2005 mpaka leo sijaupata. vipi ntaupataje?!
Sijui unaishi wapi, ila kama unaishi dar, huo wimbo utaupata pale, temeke mwisho, zinaposhusha basi za kusini, Wale wananyimbo nyingi za zamani. nikikosa wimbo mtandaoni naenda pale, nyimbo nyingine mtandaoni huwa haziimbi mpaka mwisho.
 
Huu zuhura, ambao Laddy Champion, mzee Zahir alihama nao toka J.KT. Ruvu, uko vizuri mkuu.
 
Vijana wa zamani mnaojua vitu. Bado wimbo wenye maneno haya sijaupata na kama mliutuma sijaziona.
Maneno yake ni hivi
Nakwenda ilula kwa wakwe zangu wakanieleza, na maneno mengi ya kwamba yeye ana uwezo
"Leo isiwe sababu ya kunitangaza mimi eehe na kuniaharibia jina langu ehe toto tundu.
Penzi langu la kusuasua
 
Sijui unaishi wapi, ila kama unaishi dar, huo wimbo utaupata pale, temeke mwisho, zinaposhusha basi za kusini, Wale wananyimbo nyingi za zamani. nikikosa wimbo mtandaoni naenda pale, nyimbo nyingine mtandaoni huwa haziimbi mpaka mwisho.
Nisaidie namba zao,,inbox.
 
29 January 2023
Wanamuziki nguli wanaounda kundi la Maquis Original na staili yao ya Sendema ya Motoo wakitumbuiza katika onesho lao la Re-Union ukumbi wa Ngalawa katika hoteli ya Royal Village jijini Dodoma Ijumaa January 28, 2023
Vumbi Dekula Kahanga, Nkashama Kanku Kelly, Mukumbule Parash, Tshimanga Asossa, Chimbwiza Mbangu ‘Nguza Vicking’ Big Sound, Abuu Omari .....
Source : Muhidin Michuzi
 
Hii ndio Taarifa iliyotufikia hivi punde , na kwamba Mzee Hussein Jumbe amefikwa na umauti katika Hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam leo 10/4/2023

Enzi za Uhai wake aliwahi kutumikia bendi za DDC MLIMANI PARK na MSONDO NGOMA

Aliwahi kutamba na Kibao chake cha "Nachechemea"

Apumzike kwa Amani .
 
"si wazuri binadamu usione wafurahi"

"Mtendee la muhimu hatoridhika, akisha kusalimu moyoni akasirika"

Ooohhh.

Bonge la Wimbo.
Hapa ni wakati wa vijembe. Baada ya kuimba wimbo huu Bitchuka akiwa OSS ndio ukawa mwisho wa vijembe kutoka Juwata.
 
Hana wemaa usimwone kucheka oooh

Mtendee wemaa lakini hatoridhikaaa

Apita kusalimu moyoni kakasirikaaaa
 
wakuu umoufia kwenu,naomba please anajua pa kuupata au mwenye nao huu wimbo "chaupele mpenzi"

waniambia niliwache rhumba nami sikuzoea,sitaweza kuliacha rhumba sababu yakooo..aisee mwenye nao anisaidie nimeutafuta sana,nikachoka ila jana bongo radio online wakaupiga ,nimepata mzuka wakuutafuta tena
 
Twende na wimbo wa "Mtu ni afya mwananchi elewa eeh, tusiwe wavivu kuzijenga vyema afya zetu"

Mwenye kujua ni bendi gani iliyoimba wimbo huu aniambie pliz. Na pia kama kuna mtu anao basi atuwekee hapa tafadhalini.
 
Daaaah,umenikumbusha mbaaali enzi hizo RTD tu akina Juma ngondae.
 
We acha tu ndugu yangu, kuna nyimbo mtu ukizisikia lazima utoe chozi bila kujijua.
Nautafuta sana mwimbo huu.
Na hisi na huu utakua unaujua[emoji1787]

"Na vijijini oooh ni kiswahili chatumika×2

Kiswahili lughaaa ya Taifaaaa.

[emoji13][emoji13]
Mwingine,,,,Tusilime tulivyozoea,tutumie mbolea,Kwa maagizo ya wataalamuu,njaa haitatokea.
 
Huu wimbo kama sikosei umeimbwa na Washirika Tanzania Stars, Njata one,
waimbaji Muhina Panduka 'Toto Tundu', Mohamed Shaweji, Adam Bakar, Madaraka Moris 'Kiwembe' na wengineo.

Naweza kurekebishwa.
 
Habari
Naomba kufaham jina la nyimbo ya jagwa music kuna mistar kadhaa naikumbuka
"Habar za saahiz kwanza nakusalimia
Kusahau mi siwez,sababu nazingatia
Siyo wewe mpuuz
Ahsante
 
Wanaitwa Them Mushrooms - Itawezakanaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…