ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Mkuu safi sana, naomba uutafte huu wimbo hapa chini aise naupenda sana ila nimeishia kuurekodi na simu kidogo juzi siku ya muungano naomba nitafutie ''full song'' nitashukuru sana.
Mkuu unaweza kunipa Jina la Mwimbaji/waimbaji wa hii ngoma???
 
Mkuu kuna wimbo wa minuo umeimbwa na
MAQUIS ORIGINAL
MINUO
niangalizie kama utaupata kwenye
Play list natanguliza shukurani sana
Mkuu hii sina kwa Files zangu ila nina Nyimbo Kumi za Marquiz Ikiwa ni Pamoja na ile ya NI WEWE PEKEE ambayo teyari nmekwisha iweka kwenye Blog yetu.
Aksante
 
Mkuu Popo si ndege,sijajua hii makala umeiandika lini,ila nimejikuta kama leo nasikiliza redio Phillips. Unaposema washindani wakubwa kabisa wa Vijana Jazz enzi hizo basi ni Washirika Tanzania Stars. Hivyo vibao vimenikumbusha mbali sana. Vibao kama Kisa,Penzi la Ulaghai,Watoto Wamekuja juu, Yaliyopita si ndwele(Dansi-Raggae Style-NIMEKUSAMEHE),
Julie,Shakaza.
Lakini umenikumbusha Bantu Group Band(Baba Jane 1&2),bila kusahau MCA International(KASORO YANGU),ilikua ni shida sana jamani

Mjumbe nimekujaaaaa kuwashitaki baba mkweeee wanguuuu, daaaa hatari sana.
 
Vibao vyote ninavyo, kasoro 'shakaza' na 'watoto wamekuja juu' sina.

Mkuu huu ni mwaka wa pili natafuta wimbo wa

Pig black - Nini mnataka

Vipi unao?
 
Vibao vyote ninavyo, kasoro 'shakaza' na 'watoto wamekuja juu' sina.
Mkuu ukinipatia wimbo wa Vijana Jazz(Kapu la Mjanja-Original Version) nitakushukuru sana. Nasema ni Original Varsion kwa sababu nadhan ulirudiwa na sauti ya Marehemu Eddie Sheggy kuna dada aliimba,hapo sijaridhika.
 
Ni kweli mkuu upo lakini sio
original. Ntautafuta original
nikiupata ntakustua
Mkuu ukinipatia wimbo wa Vijana Jazz(Kapu la Mjanja-Original Version) nitakushukuru sana. Nasema ni Original Varsion kwa sababu nadhan ulirudiwa na sauti ya Marehemu Eddie Sheggy kuna dada aliimba,hapo sijaridhika.
 
Kuna wimbo una kibwagizo kinachosema, "....ni mashaka ya maisha, wema hawana maisha...." Mwenye huo wimbo anitumie tafadhali.
 
Habarini, leo nimepanda daladala nikasikia nyimbo mbili za bendi fulani za zamani, nilikuwa dogo ila nilikuwa najitambua! Nimeusikia wimbo huu nimekumbuka mbali sana tabora, nimeshawishika nitafute hizi nyimbo na zingine za kina hamza kalala komando ila sijui pa kuzipata.
Nimesikia hizi nyimbo mbili chini ktk daladala ila sizijui majina wala walioimba nikajikuta nimesafirishwa mpaka miaka ya 90s.
-Bwana mwangusi nakupa pole sana watu hao ni walaghai wanaitwa matapeli......

Mwingine huu;

-hunijali kwa chumvi hunijali kwa sukari tabu nyingi ninapata na watoto......

-Vijana wengi hukosa adabu iieee wakishajua huyo si mama yake ieeee humdharau na kumsimanga iiieeeee.......

Old is gold!!

Mkuu, hizi nyimbo mbili ulizozitaja ni za Vijana Jazz - Pambo Moto chini ya Marehemu Hemed Maneti enzi hizo. Wa kwanza ulioutaja (Bwana Mwangusi) unaitwa 'Ogopa Matapeli," yule mwenye sauti tamu ya hajabu aliye imba huu wimbo ni Eddy Sheggy (R.I.P.) Huo wimbo wa pili (hunijali kwa chumvi) unaitwa "Penzi Haligawanyiki, Pt. I' uliimbwa na Chiriku Maneti na mkewe Kida Waziri. Baada ya kusikiliza hii dozi ya Vijana, niambie kwa akili yako....unaweza kweli kulinganisha na bongo fleva huu muziki wetu wa dansi? Muziki wa dansi ni kiboko ya mabishololo wa muziki.
 
daaah hatimaye nimepata wimbo niliokuwa nautafuta wa papii kocha_salima, mkuu naomba pia kama ntapata wimbo ule, siri ya niniii, nahis wa Hussein jumbe
 
Back
Top Bottom