Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii inakukumbusha wapi? Kamata sauti za dhahabu za Hemed Maneti, Mohamed Shaweji na Mohamed Salum "Gotagota". Katika solo yupo Shaaban Yohana "Wanted". Bendi ni Vijana Jazz, Kibao ni 'Siri ya Ndani' na mwaka ni 1990.
Duh, Mkuu,nimesoma hilo cover nikaona kile kibao cha Nyongise. Bila shaka ni utunzi wa Mzee John Kitine. Yaani kuuona tu huo wimbo, nimekumbuka mbali sana.
Nilikuwa Kigoma naangalia game ya kandanda kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mwanzoni kabisa mwa 1990 (enzi hizo hakuna cha EPL kwenye TV). Kuna rafiki yangu niliyesoma naye Primary anaitwa Kabeya Moses, huku tunaangalia mpira na sikioni amewka karedio kake kadogo anasikiliza muziki Nyongise ukivurumishwa kupitia RTD enzi hizo.
leo nimeisikiliza nyimbo ya Urafiki Jazz wana Chaka chuwa inasema...
''biashara ya njugu na korosho haikufai mama wee, Gezaulole mama, Gezaulole Mama wee''
Dah Juma Mrisho Ngulimba wa Ngulimba amefanya kazi sana mle...
Jerry Nashon ameimba Immaculata (Makulata) kwa lugha ya Kijaluo.
Mkuu wangu Ibrah....
Habari za miaka mkuu...
Hicho kikosi cha Pambamoto kilikuwa ni kikali sana mkuu...Ni kama Barcelona ya sasa...Kikosi kilikuwa kimesheheni vipaji kama Hemed Maneti Ulaya, Kida Waziri, Adam Bakari, Eddy Sheggy, Hamza Kalala, Kulwa Mlonge, Hamis Mnyupe, Hassan Shaw, Abuu Semhando, Shaaban Yohana, Shaban Dogodogo na wengine...
Nakumbuka mwaka huo wa 1990 ndipo Vijana Jazz walitoa albam yenye vibao kama Ngapulila, Ogopa Tapeli, Mwisho wa mwezi, Chanjo kwa watoto, Penzi haligawanyiki na Telegram (Jamaa alimdanganya boss wake kapokea Telegram inayomjulisha kifo cha kaka yake...Boss akampa pole kwa msiba uliompata,akatoa fedha,gari na wafanyakazi kumsindikiza kwenda kijijini...Kufika kijijini hakukuwa na msiba wala nini....)
John Kitime yeye alijiunga na Vijana Jazz mwaka 1991 kama sikosei, na hii ni baada ya Hamza Kalala, Eddy Sheggy na Adam Bakari kujiondoa Vijana Jazz na kwenda kuanzisha Washirika Tanzania Stars Band 'Watu njata njata'...
Akiwa Vijana Jazz Kitime alitunga vibao vitamu kama Nyongise(Nyongise nigenenene nyongisee......) na Malaine.....
Hakika ya kale yalikuwa zaidi ya dhahabu...

Msaada wenu wana jf msaada wa rekodi ya nyimbo hizi za zilipendwa online 1. DALILI-MSONDO NGOMA 2. CHEUSI MAGALA NO.1-OTTU JAZZ 3. MALARIA-MSONDO NGOMA 4. NIPELEKE KWA BABA NO.2-OTTU JAZZ 5. SI WAZURI BINADAMU-MLIMANI PARK ORCHESTRA Kama kuna mdau ataweza kuniaploadia online au anafahamu link ambayo nitaweza kuzipata nyimbo hizi, nitashukuru sana
kuna wimbo unasema:-
Naikumbuka siku ileeee ulipokuja asubuhi na mapema,
ukifoka kwa ukali , kwamba ni mimi niliyetaka vunja ndoa yako.
Namshukuru baba mwenye nyumba,
aliyelizua panga lako,
lisishuke maungoni na kunipa kilema cha maisha.
Chorus:-
ukweli ulikuja kwa hasira sana (ehhh bwana ehhh)
bila kufahamu undani wa mambo yenyewe.
wimbo huo nautafuta sana, sikumbuki jina lake wala walioupiga

Mkereketwa_Huyu asante sana.NI wimbo wa msondo na unaitwa Kilema Cha Maisha.
Mkereketwa_Huyu asante sana.
Je unaweza kuwa na wimbo huu?