Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nanreen......Eddy(mtoto wa Tambaza almaarufu kama msomi wa Tambaza huyu) kwa kweli alikuwa anavutia hasa,alikuwa ana sauti ya kipekee kabisa,sikiliza nyimbo alizoimba kama Wivu,Mwisho wa mwezi,Ngapulila(Vijana Jazz), Julie,Nelson Mandela,Yaliyopita si ndwele(Washirika Tanzania Stars), Shakaza(Bima Lee Orch), Milima ya kwetu(Super Rainbow), Ngondoigwe,Baba Jane(Bantu Group) utagundua ni kwa nini nasema Eddy Sheggy 'Mzee Shakaza'(R.I.P) alikuwa na sauti ya kipekee........Japo wadogo zake Francis na Christian Sheggy walijaribu kumuiga,hawakuweza.....Jamaa alikuwa sayari nyingine kabisa.......
Hebu angalia kitu hiki ulichokiomba ambacho Eddy alikitunga na kukiimba akiwa na Super Rainbow,aliimba kwa kushirikiana na Nanah Njige.....Kitu Milima ya kwetu...
Milima ya Kwetu
Nikitazama milima ya kwetu ee,
machozi yanitoka kwa uchungu na mawazo,
tulitoka wawili ninarudi peke yangu,
baba na mama wataniuliza bibi yako yuko wapi ee,
Ndugu jamaa wataniuliza bibi yako yuko wapi eee,
japokuwa ninakaribia kufika nyumbani ee,
Ninatamani gari isifikie upeesi,
kwa ile aibu nitakayopata mbele ya wazazi ii,
kwa vile ni miezi michache imepita nilitoka na bibi yangu,
(Eddy)
Nitasema nini kwa baba mimi najuta aa,
kwa pesa zake nyiingi alizopotezaa,
harusi ilifanyika kwa gharama kubwa sana,
watu walikula na kunywa na kusaza mamaa,
Nikaenda kuishi na bibi yule mjini,
kazi yake ilikuwa ni vituko,
nikaenda kuishi na bibi yule mjini kazi yake ilikuwa ni vitiimbwi,
Alianza kuweka sukari kwenye mboga,
nikaonja haviliki tukalala na njaa,
kafuatia na kuweka chumvi kwenye chai,
nilikuwa na wageni wakatoka bila kuaga,
kafuatia kuchelewa akienda sokoni,
nikimuuliza anitukana hadharani aibu,
kuna gari imekuja hadi mlangoni,
kujitetea akasema mjomba wake kaja,
hivi juzi kavunja kioo cha dirisha,
apate kuchungulia wapitao njiani,
hatimaye kunibeza na kunidharau,
shikamoo ikaisha ikabaki
Vipi babu, mambo zakoo ee x2
Nilishindwa kumuuliza ee sikutaka kumuudhi,
sababu nilikuwa nampenda nampenda saana x 2
chorus:
walisemaa dalili ya mvua ni mawingu,
niliyempenda kanitoroka mama,
(Eddy Sheggy)
Nilinyang'anywa tonge mdomoni,
nilinyang'anywa tonge kinywani,
niliyempenda kanikimbia mama yoyo,
niliempenda kanikimbia masikini nifanye nini mama,
(chorus)
Vituko ee, vituko vya bibi huyoo,
sitaweza kusahau mimi oo mama ee,
sitaweza kusahau mimi oo sheggy ee,
alikuwa kama helikopta, ndege isiyochagua mahali pa kutua ee,
kila mtaa hapa mjini jamani tazameni oo,
ana bwana mmoja ama wawili mama mama oo,
nifanye nini mama oo,
Umenikumbusha mbali uncle!!! Daah - iyo historia kwani imeshaisha? Mbona nasikia mavitu yanazidi kuporomoshwa na hivi vichwa kama supu umeitia nazi,Jinamizi la talaka etc Malizia tafadhari!! wanakosa airtime tu kwa media mbalimbali.Kwa leo ngoja nimalize na DDC Mlimani Park Orchestra..........Dah....Hata sijui nianzie wapi hapa maana maelezo yatakuwa marefu kweli,ngoja japo niyafupishe kidogo....
Historia ya Bendi hii inaanzia mwaka 1978 ambapo takriban wanamuziki wanane waliihama bendi ya Dar International na
kwenda kuanzisha bendi ya Orchestra Mlimani Park.Baadhi yao ni aliyekuwa mtaalamu wa kupiga ala zote King MichaelEnock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum na Habib Jeff,hawa waliungana na Muhidin Maalim Gurumo,Hassan Rehani Bitchuka na Abel Barthazar(ambaye ndio hasa muanzilishi wa Mlimani Park)..... Ilijulikan hivyo(Mlimani Park Orchestra) kutokana kuwa na maskani yake pale Mlimani Club mitaa ya Mwenge jijini Dar es Salaam chini ya umiliki wa Tanzania Transport and Taxi Services.
Mwaka 1983 waliokuwa wamiliki wa bendi hiyo walifilisika na na hatimaye bendi hiyo ikachukuliwa na Dar es Salaam Development Corporation (DDC) na hapo ndiyo ikaanza kuvuma kwa jina la DDC Mlimani Park Orchestra ikiwa chini ya wanamuziki galacha na waasisi, Muhidin Maalim Gurumo, Abel Baltazar, Hassan Rehani Bitchuka, ambao walitokea JUWATA Jazz Band huku Cosmas Thobias Chidumule, Michael Enoch King Michael na mpiga gitaa la solo mahiri, Joseph Batholemeo Mulenga, wakiwa wametwaliwa kutoka Dar International. ............Mtindo walioutumia tangu enzi hizo ni ule wa Sikinde Ngoma ya ukae.....
Baadhi ya nyimbo zilizotamba sana za Sikinde ni pamoja na Sauda/MV Mapenzi(namba 1 na 2),Neema,Usitumie Pesa kama fimbo,Mume wangu Jerry,Clara,Hiba,Matatizo ya nyumbani,Majirani huzima redio,Nidhamu ya kazi,Kassim amefilisika,Talaka ya hasira,Hadija,Barua toka kwa mama,Celina,Editha,Fikiri nisamehe,Pole mkuu mwenzangu,Diana,Pesa,Hata kama,Bubu ataka sema,Mnanionesha njia ya kwetu,Tangazia mataifa yote,Mtoto akililia wembe,Nalala kwa tabu,Duniani kuna mambo,Kiu ya jibu,Dua la kuku,Nawashukuru wazazi,Pata potea,Nelson Mandela,Uzuri wa mtu,mdomo huponza kichwa,Taxi Driver,Tucheze Sikinde,Conjesta na nyimbo niyngine nyingi tamu.....
Wanamuziki walioipitia bendi hii ni pamoja na King Michael Enock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum,Habib Jeff,Muhidin Maalim Gurumo,Hassan Rehani Bitchuka,Abel Barthazar,Henry Mkanyia,Fresh Jumbe,Hussein Jumbe,Benno Villa Anthony,Tino Masinge 'Arawa',Hassan Kunyata,Francis(Nassir) Lubua,Maalim Hassan Kinyasi,Abdallah Gama,Max Bushoke,Muharami Said,Kassim Mponda,Julius Mzeru,Said Chipelembe,Ally Jamwaka,Machaku Salum,Ally Yahaya,Shaban Lendi,Joseph Bernard,Juma Hassan Town na wengine wengi....
Tumwagie data za vijana jazz, vijana orchestra, air pambamoto, saga rhumba:Umenikumbusha mbali uncle!!! Daah - iyo historia kwani imeshaisha? Mbona nasikia mavitu yanazidi kuporomoshwa na hivi vichwa kama supu umeitia nazi,Jinamizi la talaka etc Malizia tafadhari!! wanakosa airtime tu kwa media mbalimbali.