ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Haya kazi kwako mkuu Bujibuji
Asante sana mtu wangu.
i salute u
salute-flag.jpg
 
28 OKTOBA 2013: SUPER KAMANYOLA kina Roy Mukuna, Parash, Benno & co AT VILLA PARK MWANZA g sengo mpeg1video source: Gsengo wa youtube
 
Last edited by a moderator:
Nanreen......Eddy(mtoto wa Tambaza almaarufu kama msomi wa Tambaza huyu) kwa kweli alikuwa anavutia hasa,alikuwa ana sauti ya kipekee kabisa,sikiliza nyimbo alizoimba kama Wivu,Mwisho wa mwezi,Ngapulila(Vijana Jazz), Julie,Nelson Mandela,Yaliyopita si ndwele(Washirika Tanzania Stars), Shakaza(Bima Lee Orch), Milima ya kwetu(Super Rainbow), Ngondoigwe,Baba Jane(Bantu Group) utagundua ni kwa nini nasema Eddy Sheggy 'Mzee Shakaza'(R.I.P) alikuwa na sauti ya kipekee........Japo wadogo zake Francis na Christian Sheggy walijaribu kumuiga,hawakuweza.....Jamaa alikuwa sayari nyingine kabisa.......

Hebu angalia kitu hiki ulichokiomba ambacho Eddy alikitunga na kukiimba akiwa na Super Rainbow,aliimba kwa kushirikiana na Nanah Njige.....Kitu Milima ya kwetu...

Milima ya Kwetu

Nikitazama milima ya kwetu ee,
machozi yanitoka kwa uchungu na mawazo,
tulitoka wawili ninarudi peke yangu,
baba na mama wataniuliza bibi yako yuko wapi ee,
Ndugu jamaa wataniuliza bibi yako yuko wapi eee,

japokuwa ninakaribia kufika nyumbani ee,
Ninatamani gari isifikie upeesi,
kwa ile aibu nitakayopata mbele ya wazazi ii,
kwa vile ni miezi michache imepita nilitoka na bibi yangu,

(Eddy)
Nitasema nini kwa baba mimi najuta aa,
kwa pesa zake nyiingi alizopotezaa,
harusi ilifanyika kwa gharama kubwa sana,
watu walikula na kunywa na kusaza mamaa,

Nikaenda kuishi na bibi yule mjini,
kazi yake ilikuwa ni vituko,
nikaenda kuishi na bibi yule mjini kazi yake ilikuwa ni vitiimbwi,

Alianza kuweka sukari kwenye mboga,
nikaonja haviliki tukalala na njaa,

kafuatia na kuweka chumvi kwenye chai,
nilikuwa na wageni wakatoka bila kuaga,

kafuatia kuchelewa akienda sokoni,
nikimuuliza anitukana hadharani aibu,

kuna gari imekuja hadi mlangoni,
kujitetea akasema mjomba wake kaja,

hivi juzi kavunja kioo cha dirisha,
apate kuchungulia wapitao njiani,

hatimaye kunibeza na kunidharau,
shikamoo ikaisha ikabaki
Vipi babu, mambo zakoo ee x2

Nilishindwa kumuuliza ee sikutaka kumuudhi,
sababu nilikuwa nampenda nampenda saana x 2

chorus:

walisemaa dalili ya mvua ni mawingu,
niliyempenda kanitoroka mama,

(Eddy Sheggy)
Nilinyang'anywa tonge mdomoni,
nilinyang'anywa tonge kinywani,
niliyempenda kanikimbia mama yoyo,
niliempenda kanikimbia masikini nifanye nini mama,

(chorus)

Vituko ee, vituko vya bibi huyoo,
sitaweza kusahau mimi oo mama ee,
sitaweza kusahau mimi oo sheggy ee,
alikuwa kama helikopta, ndege isiyochagua mahali pa kutua ee,
kila mtaa hapa mjini jamani tazameni oo,
ana bwana mmoja ama wawili mama mama oo,
nifanye nini mama oo,

Kaka umenikumbusha my childhood. Hii ngoma niliikariri japo nilikua mdogo. Eddy Sheggy ndo alikua mtunzi na kuimba akishirikiana na Nana Njige
 
Nimekumbuka pamba moto daresalama awamu ya pili
 
Kwa leo ngoja nimalize na DDC Mlimani Park Orchestra..........Dah....Hata sijui nianzie wapi hapa maana maelezo yatakuwa marefu kweli,ngoja japo niyafupishe kidogo....

Historia ya Bendi hii inaanzia mwaka 1978 ambapo takriban wanamuziki wanane waliihama bendi ya Dar International na
kwenda kuanzisha bendi ya Orchestra Mlimani Park.Baadhi yao ni aliyekuwa mtaalamu wa kupiga ala zote King MichaelEnock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum na Habib Jeff,hawa waliungana na Muhidin Maalim Gurumo,Hassan Rehani Bitchuka na Abel Barthazar(ambaye ndio hasa muanzilishi wa Mlimani Park)..... Ilijulikan hivyo(Mlimani Park Orchestra) kutokana kuwa na maskani yake pale Mlimani Club mitaa ya Mwenge jijini Dar es Salaam chini ya umiliki wa Tanzania Transport and Taxi Services.

Mwaka 1983 waliokuwa wamiliki wa bendi hiyo walifilisika na na hatimaye bendi hiyo ikachukuliwa na Dar es Salaam Development Corporation (DDC) na hapo ndiyo ikaanza kuvuma kwa jina la DDC Mlimani Park Orchestra ikiwa chini ya wanamuziki galacha na waasisi, Muhidin Maalim Gurumo, Abel Baltazar, Hassan Rehani Bitchuka, ambao walitokea JUWATA Jazz Band huku Cosmas Thobias Chidumule, Michael Enoch ‘King Michael’ na mpiga gitaa la solo mahiri, Joseph Batholemeo Mulenga, wakiwa wametwaliwa kutoka Dar International. ............Mtindo walioutumia tangu enzi hizo ni ule wa Sikinde Ngoma ya ukae.....

Baadhi ya nyimbo zilizotamba sana za Sikinde ni pamoja na Sauda/MV Mapenzi(namba 1 na 2),Neema,Usitumie Pesa kama fimbo,Mume wangu Jerry,Clara,Hiba,Matatizo ya nyumbani,Majirani huzima redio,Nidhamu ya kazi,Kassim amefilisika,Talaka ya hasira,Hadija,Barua toka kwa mama,Celina,Editha,Fikiri nisamehe,Pole mkuu mwenzangu,Diana,Pesa,Hata kama,Bubu ataka sema,Mnanionesha njia ya kwetu,Tangazia mataifa yote,Mtoto akililia wembe,Nalala kwa tabu,Duniani kuna mambo,Kiu ya jibu,Dua la kuku,Nawashukuru wazazi,Pata potea,Nelson Mandela,Uzuri wa mtu,mdomo huponza kichwa,Taxi Driver,Tucheze Sikinde,Conjesta na nyimbo niyngine nyingi tamu.....

Wanamuziki walioipitia bendi hii ni pamoja na King Michael Enock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum,Habib Jeff,Muhidin Maalim Gurumo,Hassan Rehani Bitchuka,Abel Barthazar,Henry Mkanyia,Fresh Jumbe,Hussein Jumbe,Benno Villa Anthony,Tino Masinge 'Arawa',Hassan Kunyata,Francis(Nassir) Lubua,Maalim Hassan Kinyasi,Abdallah Gama,Max Bushoke,Muharami Said,Kassim Mponda,Julius Mzeru,Said Chipelembe,Ally Jamwaka,Machaku Salum,Ally Yahaya,Shaban Lendi,Joseph Bernard,Juma Hassan Town na wengine wengi....
Umenikumbusha mbali uncle!!! Daah - iyo historia kwani imeshaisha? Mbona nasikia mavitu yanazidi kuporomoshwa na hivi vichwa kama supu umeitia nazi,Jinamizi la talaka etc Malizia tafadhari!! wanakosa airtime tu kwa media mbalimbali.
 
Tumwagie data za vijana jazz, vijana orchestra, air pambamoto, saga rhumba:
 
Nawatakiwa maandalizi mema ya Krismas na Mwaka mpya 2014

Last edited by a moderator:
Watoto wamekuja Juu....

Hayati Adam Bakari ' Sauti ya Zege' na Washirika Tanzania Stars 'Watu njatanjata'

Ningali bado najiuliza usiku na mchana, na mume wangu kanitoka upweke umenizunguka...
Watoto wamekuja juu, wanadai nyumba yao, Watoto wamekuja juu, wanadai nyumba yao....

Na kila nikifikiria jinsi nilivyotabika, na malezi ya watoto ingawa sikuwazaa...
Watoto wamekuja juu, wanadai nyumba yao, Watoto wamekuja juu, wanadai nyumba yao....

Ningali bado najiuliza usiku na mchana, na mume wangu kanitoka upweke umenizunguka...
Watoto wamekuja juu, wanadai nyumba yao, Watoto wamekuja juu, wanadai nyumba yao...

Na kila nikifikiria jinsi nilivyotabika, na malezi ya watoto ingawa sikuwazaa...
Watoto wamekuja juu, wanadai nyumba yao, Watoto wamekuja juu, wanadai nyumba yao....

Adam Bakari:

Kila nilifanyalo wao haliwapendezi, na wala hawakumbuki usia wa baba yao;
Kila nilifanyalo wao haliwapendezi, na wala hawakumbuki usia wa baba yao;

Marehemu aliusia wasinitupetupe, na wala wasininyanyase mama....ooh mama...
Marehemu aliusia wasinidharau, na wala wasininyanyase mama....ooh mama...

Majirani wameshauri eti nirudi nyumbani kwani sina baba wala mama, jama niende kwa nani....
Wengine wameshauri eti niwashitaki wakati nyumbani ni mali yao, Jama nifanye nini....

Marehemu aliusia wasinitupetupe, na wala wasininyanyase mama....ooh mama...
Marehemu aliusia wasinidharau, na wala wasininyanyase mama....ooh mama...

Marehemu aliusia wasinitupetupe, na wala wasininyanyase mama....ooh mama...
Marehemu aliusia wasinidharau, na wala wasininyanyase mama....ooh mama...
 
Christina Moshi ....

International Orchestra Safari Sound....wana Ndekule

Sina budi mama kukueleza, katika wimbo mpenzi Moshi...
Mchana kutwa huwa nashinda sina raha mkono kwenye shavu...
Sina budi mama kukueleza, katika wimbo mpenzi Moshi...
Mchana kutwa huwa nashinda sina raha mkono kwenye shavu...

Kusema kweli moyo wangu umeridhika kwa penzi lako mpenzi Christina...
Nimeamini penzi ni kiungo kwa wapendanao unanitoa upweke...
Kusema kweli moyo wangu umeridhika kwa penzi lako mpenzi Christina...
Nimeamini penzi ni kiungo kwa wapendanao unanitoa upweke...

Christina Moshi sikiliza maelezo yangu katika wimbo mamaa...
Naelewa penzi li bado ni changa usije tena ukabadilika baadae...
Tulipokubaliana kwa hiari tulikuwa wawili wa tatu Mungu wetu...
Tulipokubaliana kwa hiari tulikuwa wawili wa tatu Mungu wetu...

Christina Moshi sikiliza maelezo yangu katika wimbo mamaa...
Naelewa penzi li bado ni changa usije tena ukaniruka baadae...
Tulipokubaliana kwa hiari tulikuwa wawili wa tatu Mungu wetu...
Tulipokubaliana kwa hiari tulikuwa wawili wa tatu Mungu wetu...

Bridge....

Pendekezo langu kwako liwe kama benki, benki imara kwa usalama...
Pendekezo langu kwako liwe kama benki, benki imara kwa usalama...
Akiba yangu ya mapenzi nakupa wewe Moshi ee mama...
Akiba yangu ya mapenzi nakupa wewe Moshi ee mama...

Uwezo sina ningekujengea nyumba, uwezo sina ningekununulia gari...
Bali matatizo madogo hayatanishinda.....
Uwezo sina ningekununulia mtumbwi, uukabidhi kwa wavuvi wakakuvulie samaki....

Uwezo sina ningekupeleka Arusha, ukapunge hewa nzuri na kutazama wanyama mbugani...
Bali matatizo madogo hayatanishinda...

Nitajipigapiga ili niyatatue, sababu jungu kuu halikosi ukoko, sababu jungu kuu halikosi ukoko...
Mpenzi Moshi lea hili penzi letu, usiliweke juani litakuja nyauka.....

Pendekezo langu kwako liwe kama benki, benki imara kwa usalama...
Pendekezo langu kwako liwe kama benki, benki imara kwa usalama...
Akiba yangu ya mapenzi nakupa wewe Moshi ee mama...
Akiba yangu ya mapenzi nakupa wewe Moshi ee mama...

Kibwagizo:
Hebu sikia maneno ya kuambiwa na wana Ndekule, Moshi ee, ee Ndekule..
Hebu sikia maneno ya kuambiwa na wana Ndekule, Moshi ee, ee Ndekule..
 
Back
Top Bottom