Zimbabwe Vs Tanzania : Full Time Zimbabwe 3 Tanzania 0

Zimbabwe Vs Tanzania : Full Time Zimbabwe 3 Tanzania 0

Nsubhi

Senior Member
Joined
Jan 27, 2015
Posts
159
Reaction score
51
Mechi ya Zimbabwe vs Tanzania itakua saa ngapi? Na itarushwa mubashara na vituo gani vya runinga?

========
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, jana ilikuwa na mechi ya Kirafiki na Zimbabwe.Pamoja na Safu ya ushambuliaji ya Tanzania kuongozwa na Mbwana Ally Samatta lakini watanzania waliishia kuambulia kichapo cha mabao matatu patupu.

Katika kufuzu kucheza Kombe la Dunia litakalofanyika mwaka 2018 nchini Urusi, Uganda iko vizuri katika nafasi ya pili nyuma ya Misri katika kundi E baada ya kuwabamiza Congo Brazaville bao moja kwa sifuri.

Jana Jumapili majirani wa Congo Brazaville, hapa nawazungumzia DRC wao wakawabamiza Guinea nyumbani kwao bao 2-1 na hivyo kuongoza kundi A.Na kule mjini Alexandria, Misri ikawabamiza Ghana bao 2-0 .

Majina ya wachezaji watano wanaowania Tuzo ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika kwa Mwaka 2016 yameshatangazwa.Wachezaji hao ni Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Riyad Mahrez, Sadio Mane and Yaya Toure.

Hadi tarehe 28 ya mwezi huu endelea kupiga kura kupitia bbc.com/africanfootball, mimi na wenzangu tutaendelea kukupa habari kuhusu shindano hili kwa kadri tuwezavyo mpaka pale tarehe 12 Desemba, mshindi wa tuzo hiyo atakapotangazwa.

Na hatimaye mashindano ya kimataifa ya mbio za baiskeli Tour of Rwanda yanatimua vumbi nchini Rwanda ambapo leo washindani 75 wanaelekea mkoa wa mashariki.

Chanzo: BBC
 
Mechi ya Zimbabwe vs Tanzania itakua saa ngapi? Na itarushwa mubashara na vituo gani vya runinga?
Sa 10 jioni,na itarushwa na channels za Azam Two na Azam Sports HD za Azam tv.
 
itakuwa saa 9:00 za zimbabwe huku kwetu ni saa10:00jion na itarushwa kupitia ZBC ya zimbabwe pamoja na AZAM TWO
 
Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa Zimbwabwe Vs Taifa Stars

Iko live on Azam Tv

Enjoy it
 
Kimya Kimya

Zaidi ya Ngwear!

Hivi hii timu ndio ile iliyochukua kombe juzi?

Maana siku ile niliwaona hadi wadada wakiwasaidia wanaume wa Dar kuleta kakombe nyumbani

KICHWA CHA >>>> tujifunze na sie kunyoa wajameni!
 
Yule mchezaji anaecheza uingereza nae amekuja?
 
Dk 9 Zimbabwe 1 Tz 0

Kuna shida kidogo kwenye beki
 
Kushabikia Taifa star ni kujiongezea pressure bure
 
Back
Top Bottom