Zimbabwe: Wakamatwa kwa kuuza tiketi za kwenda mbinguni

Yaani ningeshauri wafungwa woote waachiliwe huru;wafungwe WANUNUZI WA TICKETS HIZO

Ha ha haa.. Kwenye Ukristo ticket sio hata haihitaji kununua ki ujinga namna ile...eti Yesu kaongea mgahawani!!!! Stupidity of drug dealer at maximum
 
Hawa vichaa wamenifanya niandike humu baada ya muda mrefu. Ati amrekodi Yesu kwa kificho.
 
Unatukana Waumini Wa Dini Tukufu Ya...... Omba Radhi Ebo!.

Sijatukana mkuu na naheshimu uhuru wa kila mtu... Ila nasema tena hao jamaa ni zaidi ya wapumbavu kabisa...ticket? Yesu mgahawani? Wawatake radhi wakiristo kuwaaibisha ... For christians the only ticket is faith to Jesus and follow the scriptrure, period!!
 
image3.jpg

Tito and Amanda Watts mtu na mkewe, walikamatwa mwishoni mwa wiki kwa kuuza ''ticket za dhahabu za kwenda mbinguni'' kwa mamia ya watu. Wanandani hawa, waliokuwa wanauza tiketi hizo kwa dola za kimarekani 99.99 kwa kila tiketi, huku wakiwaambia wanunuaji kuwa zilikuwa zimetengenezwa kwa dhahabu halisi na kila tiketi ilikuwa na uwezo wa kumpeleka mtu mbinguni-- mara ukionyesha hii tiketi kwenye lango la mbinguni unakuwa umefika, walidai.

Polisi wazungumza:
''Hatukatazi watu kuuza tiketi za kwenda mbinguni'' msemaji wa polisi wa eneo la Jacksonville alisema

''lakini hawa ndugu walifanya ulaghai '' Tiketi zilikuwa ni miti iliyopuliziwa rangi inayofanana na dhahabu huku zikiwa zimeandikwa ''Tiketi ya kwenda mbinguni- jinyakulie moja''. Huwezi kuuza kitu unachosema ni dhahabu kumbe sio. Hapa ndipo hawa wanandani walipovuka mpaka''

Tito kwenye maelezo yake kwa polisi aliandika:

"Sibabaishwi na wanachokisema polisi. Hizi tiketi ni dhahabu halisi na sio kweli kuwa nimepulizia rangi. Ni Yesu mwenyewe aliyenipa pale nyuma ya mgahawa wa KFC huku akiniambia nikauze ili nipate fedha za kwenda anga za juu.

"Kwanza nilikutana na kiumbe wa sayari nyingine anayeitwa Stevie ambaye aliniambia kuwa kama nikiwa na fedha ataninyakuwa mimi na mke wangu kwenye ungo wake unaopaa mpaka kwenye sayari yake ambayo imeumbwa kwa cocaine tupu. Nitaweza kuvuta unga wa cocaine kadiri nipendavyo... tena bila malipo.

Jaribuni kumpeleka mtu asiye na hatia jela ndio mtakiona cha mtema kuni. Kama ni kukamata basi akamatwe Yesu kwasababu ndio yeye aliyenipatia hizi tiketi na kuniambia nikauze. Niko tayari kumrikodi kwa kificho ili ukweli ujulikane"

Mke naye alijitetea:

"Nia yetu ni kuondokana na dunia hii tuende zetu anga za juu tukavute unga wa cocaine.

Sijafanya chochote. Mume wangu ndio alikuwa anauza hizo tiketi za dhahabu za kwenda mbinguni. Mimi nilikuwa mwangaliaji."

Polisi wanasema waliwakamata na zaidi ya dola za kimarekani 10,000 taslimu, mabomba matano ya kuvutia unga na mamba mdogo.

Couple Arrested for Selling “Tickets to Heaven” | CelebTriCity

Huyo ni maza Ishmael akiwa na mchumba wake.
Its a family business.
 
Last edited by a moderator:
........"Kwanza nilikutana na kiumbe wa sayari nyingine anayeitwa Stevie ambaye aliniambia kuwa kama nikiwa na fedha ataninyakuwa mimi na mke wangu kwenye ungo wake unaopaa mpaka kwenye sayari yake ambayo imeumbwa kwa cocaine tupu. Nitaweza kuvuta unga wa cocaine kadiri nipendavyo... tena bila malipo...............
  • Hawa badala ya kupelekwa polisi, wapelekwe hospitali kwanza!!
 
hawa jamaa ni magenius. convincing power yao ni kali. hapo wamekula vichwa kama 100.

halafu wao hawajasema wanataka kwenda kwa Yesu, wao wanamfuata stevie huko juu. hii ni
sehemu nyingine ambayo wao wanaitangaza tofauti na zile pepo tulizozoea kuzisikia. pepo yao mpango mzima
ni cocaine ambayo haina overdose wala nini...
 
Msiwadharau jamani. Huwezi jua kingereza wanacho kitumia mpaka wenzao kikawa kigumu wakajiachia. Tiketi ya kwenda mbinguni, tena kaileta Yesu, akakwambia weye uza, ila pesa umlipe mwingine akupeleke kwenye dimbwi la cocaine.
Ama kweli, mengi tunayakosa, tusioijua hiyo coke.
Hii kitu imekaa poa sana. Furaha yangu ni hizo njimbo walojiweka, duhhh Halafu ukiwaangalia ka mtu na dadake vile. Sijui wangebahatika wakampata mtoto angekuwaje
 
Wameona kuna fursa nyingi za kupiga hela kwenye ukristo nao wakachangamkia fursa.
 
image3.jpg

Tito and Amanda Watts mtu na mkewe, walikamatwa mwishoni mwa wiki kwa kuuza ''ticket za dhahabu za kwenda mbinguni'' kwa mamia ya watu. Wanandani hawa, waliokuwa wanauza tiketi hizo kwa dola za kimarekani 99.99 kwa kila tiketi, huku wakiwaambia wanunuaji kuwa zilikuwa zimetengenezwa kwa dhahabu halisi na kila tiketi ilikuwa na uwezo wa kumpeleka mtu mbinguni-- mara ukionyesha hii tiketi kwenye lango la mbinguni unakuwa umefika, walidai.

Polisi wazungumza:
''Hatukatazi watu kuuza tiketi za kwenda mbinguni'' msemaji wa polisi wa eneo la Jacksonville alisema

''lakini hawa ndugu walifanya ulaghai '' Tiketi zilikuwa ni miti iliyopuliziwa rangi inayofanana na dhahabu huku zikiwa zimeandikwa ''Tiketi ya kwenda mbinguni- jinyakulie moja''. Huwezi kuuza kitu unachosema ni dhahabu kumbe sio. Hapa ndipo hawa wanandani walipovuka mpaka''

Tito kwenye maelezo yake kwa polisi aliandika:

"Sibabaishwi na wanachokisema polisi. Hizi tiketi ni dhahabu halisi na sio kweli kuwa nimepulizia rangi. Ni Yesu mwenyewe aliyenipa pale nyuma ya mgahawa wa KFC huku akiniambia nikauze ili nipate fedha za kwenda anga za juu.

"Kwanza nilikutana na kiumbe wa sayari nyingine anayeitwa Stevie ambaye aliniambia kuwa kama nikiwa na fedha ataninyakuwa mimi na mke wangu kwenye ungo wake unaopaa mpaka kwenye sayari yake ambayo imeumbwa kwa cocaine tupu. Nitaweza kuvuta unga wa cocaine kadiri nipendavyo... tena bila malipo.

Jaribuni kumpeleka mtu asiye na hatia jela ndio mtakiona cha mtema kuni. Kama ni kukamata basi akamatwe Yesu kwasababu ndio yeye aliyenipatia hizi tiketi na kuniambia nikauze. Niko tayari kumrikodi kwa kificho ili ukweli ujulikane"

Mke naye alijitetea:

"Nia yetu ni kuondokana na dunia hii tuende zetu anga za juu tukavute unga wa cocaine.

Sijafanya chochote. Mume wangu ndio alikuwa anauza hizo tiketi za dhahabu za kwenda mbinguni. Mimi nilikuwa mwangaliaji."

Polisi wanasema waliwakamata na zaidi ya dola za kimarekani 10,000 taslimu, mabomba matano ya kuvutia unga na mamba mdogo.

Couple Arrested for Selling “Tickets to Heaven” | CelebTriCity

Watu wawe makini. This is another Kibwetere
 
Back
Top Bottom