Zama zipi kaka wakati Bongo ni ile ile, yaani Watanzania mbona ni wale wale ninaowajua.
Tatizo wana habari wenu watepetevu sana, yaani wapo wapo tu, hawajui kudadavua taarifa hususan zinazohusu mahesabu, wengi labda utawakuta wamejazana kwenye taarifa za burudani.
Kuna jamaa amepost picha inayodhihirisha mapungufu ya wana habari wenu, hebu ione hapa chini kwamba Zitto anapigia makelele uchotwaji wa 1.5 trillion na wanaompa vinasa sauti ni wachache tu, lakini Diamond akiomba kikao na wanahabari wanamjazia vinasa sauti hadi anakosa pa kupumulia
Aibu kwa vyombo vya habari
Sasa nataka uone jinsi wanahabari wanastahili kuanika taarifa za mafisadi, ona media za Kenya hapa