Zimebaki siku nne tu kwa mujibu wa katiba kumtangaza, kuthibitishwa na bunge na kuapishwa kwa Makamu wa Rais

Zimebaki siku nne tu kwa mujibu wa katiba kumtangaza, kuthibitishwa na bunge na kuapishwa kwa Makamu wa Rais

Sijaona mahali popote kwenye katiba panapoonyesha makamu wa Rais anatakiwa awe ameteuliwa ndani ya siku 14
 
🤣🤣 Nimecheka sana!!, Wizara ya afya inakoelekea kama hazitachukuliwa jitihada za haraka kuinusuru tunaenda kuipoteza. Gwajima+Mollel,, sijui jiwe alifikiriaga nini au ndio kutokushauriwa
Hahahahahaa waliomshauri Mzee Baba Wizara ya Afya amuweke huyu GWAJIMA WA KIKE ndio wanaopigia Chapuo awe VP waTz. Yanayoendelea huko mjengoni, mbona mtanikumbuka
 
Wakuu

Kuanzia tarehe 17/3/2021 mpaka leo ni siku kumi. Kwakuwa katiba inatamka ndani ya siku 14 makamu awe amepatikana, basi sasa rais na chama wamebakiwa na siku 4 kutuletea makamu.

Niwatakie kila la heri na watuletee mtu mwenye uwezo.
Jumatatu subiri blinking news
 
Sioni kama rais atafanya mabadiliko makubwa hivyo maana inaonesha wanaendelea alipoishia jpm.
Kisiasa kuendeleza alipoishia jpm kuna maana gani?. Inawezakuwa ni kufanikisha ilani ya chama maana ndo mwongozo. Kutekeleza ilani ya chama si lazima utumie mtindo wa Jpm.

Kwani Kuendeleza alipoishia Jpm na kuongoza kwa mtindo wa Jpm ni kitu hichohicho?

Uwezekano ni mkubwa pm akabaki, ila akibadilishwa haitamaanisha kuwa haendelezi ilani ya chama. Tukumbuke Jpm alipaswa kutekeleza ilani ya chama hivyo Samia ataendeleza hilo.
 
Back
Top Bottom