Mkuu,unajua kuwa Jaji Upendo Msuya amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu? Msifanye kila jambo kuwa la kisiasa na kuwapakazia watu. Kujiuzulu si dhambi,ni haki ya mtu.
Acha ramli chonganishi kwakuwa,kama wengi wetu,hukuziona barua zao za kujiuzulu zinazoainisha sababu. ID yako feki isikupe haki ya kuropoka na kupakazia.
Jambo la wazi ni kwamba Majaji na watu wengine wamekuwa wakijiuzulu kwa muda mrefu,, na hasa hasa wakifikia muda wa kustaafu kwa hiari. Tatizo ni kwamba utawala huu umekuwa ukiandika kila jambo kwa lengo la kupata sifa zisizo na maana. Nakumbuka Jaji Kalegeya na Jaji Chingwile ,,wao walijiuzulu kipindi cha Kikwete lakini hatukutangaziwa hivyo,, na walikubaliwa kuacha. Pia kuna Jaji Mwalusanya ,,,the late yeye aliacha ujaji Kipindi cha Mkapa. Na mara nyingi sana sababu za kuacha huwa zinakuwa personal sana,, kwa mfano ugonjwa,,,au kuichoka kazi hiyo isiyokuwa na uhuru kabisa,, au kuamua kwenda kuishi maisha mapya. Na mtu anayeacha na kukubaliwa anapatiwa mafao yote (Ambayo ni mazito sana,, ikiwepo Gari aina land Cruiser Mpya). Kwaiyo si sahihi kuhusisha mambo yasiyo uhakika kwa watu wanaoacha kazi za Ujaji. Jaji Upendo Msuya amefanya kazi kubwa mahakamani,, kazi ya kuthibitisha kosa au makosa waliyotenda watu katika jinai ni ya DPP si ya mahakama na kama hujaridhika unakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.Na amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu.
Jaji Mujulizi ni jaji ambaye historia yake inaanzia IMMMA Advocates,,. Na alifanikiwa sana akiwa wakili wa kujitegemea ,, na wengi walishangaa yeye kwenda kujiunga na Judiciary,,, lakini inaonekana aliombwa sana na JK ili kuweka mchango wake kwenye judiciary na Law Reform Commission.