Tetesi: Zinazodaiwa kuwa sababu za RC Meck Sadiki, Jaji Mujulizi na Jaji Upendo Msuya kuacha kazi

Tetesi: Zinazodaiwa kuwa sababu za RC Meck Sadiki, Jaji Mujulizi na Jaji Upendo Msuya kuacha kazi

Sababu za kitoto sana hizi. FYI kama hayo makosa ya kusadika yangekua kweli katu wasingeachia madaraka maana wangekua na somewhat diplomatic immunity ila baada ya kuachia hawana immunity yeyote Ndo wataswaga ndani only kama ingekua kweli. Ni wajinga kiasi gani wasijue Hilo. Hizi story za kusadikika za haziwasaidii nyinyi wala kuwapunguzia wao chochote

Kwenye nchi za watu kujiuzulu ni utaratibu wa kawaida kabisa ila bongo ni kitu cha ajabu. Smh
 
Put your evidence over the table. Imesemwa na nani?
Lisemwalo lipo! Mind we do not always work with evidence in ethical issues. Ukimuona mtu ana mali ya bilioni nyingi for example, lakini mshahara wake ni laki mbili kwa mwezi na hana biashara inayojulikana, tunaweka ????????
 
Mhh ebu tuiandike kwanza tuone inaonekanaje 2,000,000,000

Humo kwenye bilioni 2 (mbili) unapata millioni moja moja zile ziwe 2000 (elfu mbili) sasa ukisema ndogo mkuu napatwa na mashaka kidogo, au mkuu kwa mwezi unaingiza zaidi ya hiko kiasi ??? [emoji1] [emoji1]
Siingizi hizo, lakini kwa mtu mwenye upenyo wa hela sio kubwa.
 
Mbona kina Manji, Gwajima na (TID, Chid Benz, Wema, Masogange, Babu wa Kitaa) waliotajwa na Bashite wamepewa dhamana na serikali hiyo hiyo haijamlalamikia jaji aliyewapa dhamana wakati Bashite kasema wao ni wauza madawa wakubwa, au wao hawana miguu ya kutorokea?
Hawa walitajwa tu. Hakuna aliyekutwa na drugs za say 6 billion kama pakistanis! soma sheria ya madawa ya kulevya hata kama siyo mwanasheria
 
Akili nyingine ni matope plus. Yaani unakuja JF kuaminisha watu kwamba wamejiuzulu kwa sababu ya makosa?? Kwa nini haka uliyajua makosa yao hujawahi kushauri wafukuzwe kazi au wafikishwe Mahakamani? Kwa nini kusubiri mpaka mtu ajiuzulu ndipo unaanza kutaja makosa yake???
 
Makonda anautaka ukuu wa mkoa wa kilimanjaro,soon anahamishiwa hapo,lzm mzee awekewe zengwe asepe.
 
Kwanini rufaa haikukatwa? Mkuu,usiamini porojo.
Kama ni kweli Mkulu aliyepita ndo anahusika na kumshinikiza jaji UM awape watuhumiwa dhamana ili watoroke, unafikiri wakili wa serikali ana ubavu wa kukata rufaa?
 
Sasa kama ni hivyo kwa nini hawakukataliwa kuachia ngazi ili badala yake wakamatwe, Washitakiwe ili sheria ichukue mkondo wake?

JF siku hizi imebakiza Members wachache sana wenye uwezo wa kufikiri. Nikiwa kama member wa JF, nakuthibitisha, wewe ni mmoja kati ya hao wachache. Swali lina mantiki sana kwa mwenye uelewa.

Na ningekuwa mimi ni Mod; kitambo uzi huu ungekuwa kwenye chakacha ya taka.
 
Hawa walitajwa tu. Hakuna aliyekutwa na drugs za say 6 billion kama pakistanis! soma sheria ya madawa ya kulevya hata kama siyo mwanasheria
Kulikuwa na sababu gani ya kuwataja wakati huna uhakika kama wanauza? Na kama sheria ya madawa inasema aliyekutwa nayo asipewe dhamana, je hukumsikia Siro akisema Manji amethibitika kuwa mtumiaji. Na je ni kiasi gani cha madawa unatakiwa kukutwa nacho kama hiyo sheria wewe umeisoma ndio ukose dhamana? Wema ni miongoni mwa watu tuliombiwa wamekutwa na madawa(bangi) ukiachilia mbali kuwa mtumiaji.
 
Hizi ni habari za uhakika za ndani kabisa kuhusu kuacha kazi kwa Majaji wawili na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

1. Ndg. Saidi Meck Sadiki - Aliyekuwa mkuu Wa Mkoa wa Kilimanjaro

Ukweli ni kuwa anakabiliwa na kesi mbaya sana ya hela hewa za usafi alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, imethibitika alifuja kiasi kikubwa takribani bilioni mbili za usafi ktk Jiji la Dsm na ilikuwa akamatwe na PCCB lakini kaamua kuachia ngazi nadhani atashughulikiwa.

2. Ndg. Aloysius Kibuuka Mujulizi - Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

Huyu ana makosa mawili makubwa, la kwanza ni lile la ESCROW Account alipokea fedha chafu za Rugemalira na kukosa sifa za kuwa Jaji mwaminifu, la pili huyu si raia wa Tanzania hivyo si mtanzania yeye ni Mganda habari za uhakika zimethibitisha hilo, Hivyo hana sifa ya kuwa Jaji huyu.

3. Ndg. Upendo Hillary Msuya - Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania.

Huyu ndiye Jaji wa hovyo kabisa yeye ameshiriki kuwaachia watuhumiwa wa kesi za madawa ya kulevya na kupokea rushwa kitendo hicho kinamuondolea sifa ya kuwa Jaji mwaminifu.


TAARIFA HIZI NI ZA UHAKIKIA KABISA KUTOKA CHANZO CHA NDANI!
Uchochezi
 
Ndg. Saidi Meck Sadick??? 2b?? Labda kama alizitia kwenye kampeni za chama 2015. Vinginevyo, pesa haiongopi, hata kama umeshika ya mtu utaonekana tu.
 
Mkuu,unajua kuwa Jaji Upendo Msuya amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu? Msifanye kila jambo kuwa la kisiasa na kuwapakazia watu. Kujiuzulu si dhambi,ni haki ya mtu.

Acha ramli chonganishi kwakuwa,kama wengi wetu,hukuziona barua zao za kujiuzulu zinazoainisha sababu. ID yako feki isikupe haki ya kuropoka na kupakazia.
Jambo la wazi ni kwamba Majaji na watu wengine wamekuwa wakijiuzulu kwa muda mrefu,, na hasa hasa wakifikia muda wa kustaafu kwa hiari. Tatizo ni kwamba utawala huu umekuwa ukiandika kila jambo kwa lengo la kupata sifa zisizo na maana. Nakumbuka Jaji Kalegeya na Jaji Chingwile ,,wao walijiuzulu kipindi cha Kikwete lakini hatukutangaziwa hivyo,, na walikubaliwa kuacha. Pia kuna Jaji Mwalusanya ,,,the late yeye aliacha ujaji Kipindi cha Mkapa. Na mara nyingi sana sababu za kuacha huwa zinakuwa personal sana,, kwa mfano ugonjwa,,,au kuichoka kazi hiyo isiyokuwa na uhuru kabisa,, au kuamua kwenda kuishi maisha mapya. Na mtu anayeacha na kukubaliwa anapatiwa mafao yote (Ambayo ni mazito sana,, ikiwepo Gari aina land Cruiser Mpya). Kwaiyo si sahihi kuhusisha mambo yasiyo uhakika kwa watu wanaoacha kazi za Ujaji. Jaji Upendo Msuya amefanya kazi kubwa mahakamani,, kazi ya kuthibitisha kosa au makosa waliyotenda watu katika jinai ni ya DPP si ya mahakama na kama hujaridhika unakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.Na amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu.
Jaji Mujulizi ni jaji ambaye historia yake inaanzia IMMMA Advocates,,. Na alifanikiwa sana akiwa wakili wa kujitegemea ,, na wengi walishangaa yeye kwenda kujiunga na Judiciary,,, lakini inaonekana aliombwa sana na JK ili kuweka mchango wake kwenye judiciary na Law Reform Commission.
 
Mkuu,unajua kuwa Jaji Upendo Msuya amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu? Msifanye kila jambo kuwa la kisiasa na kuwapakazia watu. Kujiuzulu si dhambi,ni haki ya mtu.

Acha ramli chonganishi kwakuwa,kama wengi wetu,hukuziona barua zao za kujiuzulu zinazoainisha sababu. ID yako feki isikupe haki ya kuropoka na kupakazia.
Wale wapakistan sijui wa iran unawakaumbuka wa heroine?wadhamini wantakiwa wakamatwe,hata wakili wao ameungana na mwanasheria wa serikali!
 
Back
Top Bottom