Zipi Sababu baada ya kuweka pamoja kwa friji chupa 3 za maji kampuni uhai, hill na kilimanjaro, nimekuta chupa 1 tu ndiyo imeganda kabisa?

Fanya kitu kimoja chagua chupa za kampuni moja, then weka maji ya hizo kampuni nyingine. Yaan tumia chupa za aina moja kugandisha halafu rudi utupe mrejesho.

Anyway, Yakitofautiana muda wa kuganda, andaa kuku mweupe na mbuzi dume mmoja tuchunguze zaidi tatizo
 
Properties za chupa zinatofautiana, mkuu tumia basic principle za physics kung'amua.
 
Muuza vinywaji mzoefu hapa, sababu zinaweza kuwa kadhaa lakini kubwa ni aina ya chupa. Vimiminika yenye chupa nyepesi mara nyingi huwahi kuganda na chupa ngumu hufuatia, hapa ongezea soda kampuni ya Coca(Plastic bottle) zinawahi kuganda kuliko pepsi.

Mbili ni viambata, japo yote ni maji lakini hivyo vitu wanaweka humo hutofautisha hapo ongezea na ujazo, vyenye ujazo mdogo vinawahi kuliko vyenye ujazo mkubwa. Hapa kuna maji ya Mo(Maisha) pamoja na ugumu wa chupa, hata ukiyatikisa yakishakuwa baridi sana yanaganda kama soda zinapotikiswa.

Mwisho ni sehemu unapoweka ndani ya friji/freezer. Japo lote ni moja, kitu kinachokaa ubavuni huwa kinawahi kuganda, kuna mafreezer baridi inaanzia chini mengine juu etc. Pia pale pipe inapoanzia au karibu yake ikitoka kwenye compressor ya freezer ndio patapowahi kugandisha.
Asante kwa maelezo mazuri ila maji ya "mo" sio maisha nadhani ni haya apa
 
Attachments

  • 20250127_143621.jpg
    20250127_143621.jpg
    305.4 KB · Views: 2
Wakipeleka sampo wakipata ile tbs kinachofuata nikufyutua tu
 
Muuza vinywaji mzoefu hapa, sababu zinaweza kuwa kadhaa lakini kubwa ni aina ya chupa. Vimiminika yenye chupa nyepesi mara nyingi huwahi kuganda na chupa ngumu hufuatia, hapa ongezea soda kampuni ya Coca(Plastic bottle) zinawahi kuganda kuliko pepsi.

Mbili ni viambata, japo yote ni maji lakini hivyo vitu wanaweka humo hutofautisha hapo ongezea na ujazo, vyenye ujazo mdogo vinawahi kuliko vyenye ujazo mkubwa. Hapa kuna maji ya Mo(Maisha) pamoja na ugumu wa chupa, hata ukiyatikisa yakishakuwa baridi sana yanaganda kama soda zinapotikiswa.

Mwisho ni sehemu unapoweka ndani ya friji/freezer. Japo lote ni moja, kitu kinachokaa ubavuni huwa kinawahi kuganda, kuna mafreezer baridi inaanzia chini mengine juu etc. Pia pale pipe inapoanzia au karibu yake ikitoka kwenye compressor ya freezer ndio patapowahi kugandisha.
👍
 
Wadau hamjamboni nyote?

Leo nimeweka kwenye friji yangu chupa tatu za maji kutoka kampuni tatu tofauti za Hill water, Kilimanjaro na Uhai

Baada ya muda nimefungua tena friji na kukuta maji ya kampuni moja ya Uhai ndiyo yameganda na kuwa barafu kabisa huku mengineyo bado kuganda

Mazingira yapo sawa ikiwemo temperature kwa chupa zote 3 kwanini chupa 1 igande haraka kuliko nyingine

Tafakuri ya kina kwa wenye ilimu ya kemia
Jibu ni wingi wa chumvi kwenye maji ya hizo chupa mbili.
 
Good analysis. Well done
 
Wadau hamjamboni nyote?

Leo nimeweka kwenye friji yangu chupa tatu za maji kutoka kampuni tatu tofauti za Hill water, Kilimanjaro na Uhai

Baada ya muda nimefungua tena friji na kukuta maji ya kampuni moja ya Uhai ndiyo yameganda na kuwa barafu kabisa huku mengineyo bado kuganda

Mazingira yapo sawa ikiwemo temperature kwa chupa zote 3 kwanini chupa 1 igande haraka kuliko nyingine

Tafakuri ya kina kwa wenye ilimu ya kemia
Mkuu angalia uimara wa hizo chupa! mbili kati ya ulizotaja chupa zake ni nyepesi utadhani maji ya Kandoro. Chupa nyepesi na nzito kuganda kwake nitofauti.
 
Pitia concept ya freezing point depression. Chemistry hiyo. Humo utaona effect ya solute/chumvi inavyoongeza muda wa maji kuganda.
 
Ila ukiangalia hapa na pale basi unajikuta tu unakunywa maji ili kukata kiu
kwa muda huo.
 
Back
Top Bottom