Muuza vinywaji mzoefu hapa, sababu zinaweza kuwa kadhaa lakini kubwa ni aina ya chupa. Vimiminika yenye chupa nyepesi mara nyingi huwahi kuganda na chupa ngumu hufuatia, hapa ongezea soda kampuni ya Coca(Plastic bottle) zinawahi kuganda kuliko pepsi.
Mbili ni viambata, japo yote ni maji lakini hivyo vitu wanaweka humo hutofautisha hapo ongezea na ujazo, vyenye ujazo mdogo vinawahi kuliko vyenye ujazo mkubwa. Hapa kuna maji ya Mo(Maisha) pamoja na ugumu wa chupa, hata ukiyatikisa yakishakuwa baridi sana yanaganda kama soda zinapotikiswa.
Mwisho ni sehemu unapoweka ndani ya friji/freezer. Japo lote ni moja, kitu kinachokaa ubavuni huwa kinawahi kuganda, kuna mafreezer baridi inaanzia chini mengine juu etc. Pia pale pipe inapoanzia au karibu yake ikitoka kwenye compressor ya freezer ndio patapowahi kugandisha.