Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 16,879
- 31,253
Mkoa wa Njombe: Mkoa wa Njombe una Halamashauri 6 ambazo ni Njombe Mjini, Vijijini, Ludewa, Makete, Wangingombe na Makambako.
Wenyeji wa Mkoa wa Njombe 70% ni wabena, ambao wanapatikana Wilaya za Njombe mjini,Vijijini, Makambako, Wangingombe na wakinga-Halamashauri ya Makete na Halamashauri ya Ludewa wapo Wapangwa na wanyasa.
Sifa muhimu za kiuchumi katika Mkoa wa Njombe
Wenyeji wa Mkoa wa Njombe 70% ni wabena, ambao wanapatikana Wilaya za Njombe mjini,Vijijini, Makambako, Wangingombe na wakinga-Halamashauri ya Makete na Halamashauri ya Ludewa wapo Wapangwa na wanyasa.
Sifa muhimu za kiuchumi katika Mkoa wa Njombe
- Ndio Mkoa unaongoza kwa Idadi ndogo ya watu kwa takwimu za awali za sensa ya 2022 Mkoa huo unakadiriwa kuwa na watu 889,946
- Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa Mikoa top 5 iliyo na watu wa vipato vikubwa zaidi kuliko Mikoa mingine.
- Mkoa wa Njombe-Makambako kuna upepo wa kiwango kikubwa ambao unaweza kuzalisha umeme wa megawati zaidi ya 300
- Unaongoza kwa uzalishaji wa mbao-Asilimia 60-70 ya mbao zote zinazotumika Tanzania zinatoka katika huo Mkoa-na zinalimwa karibu Halamashauri zote za Mkoa huo.
- Unaongoza kwa uzalishaji wa zao la viazi mviringo 70% ya viazi vyote Tanzanua vinalimwa huko.
- Unaongoza katika uzalishaji wa zao LA parachihi Tanzania nzima.
- Ndio Mkoa unaongoza kwa madini ya Chuma na Makaa ya mawe. Kwa Tanzania akiba kubwa ya madini hayo yapo Mkoa huo na yanapatikana kule Luganga na Mchuchuma Wilayani Ludema.
- Unaongoza kwa wafanyabiashara wakubwa Tanzani a.k.a Wakinga
- Ndio Mkoa unaongoza kwa baridi Tanzania nzima hasa Njombe Mjini na Makete
- Mkoa wa Njombe ndio Mkoa pekee kwa kipindi cha miaka 5-10 unaongoza kwenye top 3 ya maambukizi ya HIV
- Mkoa wa Njombe ina Idadi kubwa ya Wanawake kuliko Wanaume kuliko Mikoa yote Tanzania.