Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Picha hii naiona kama magari yamepaki tu bila mpangilio.
Safi sana kamanda haya ndo maendeleo tunayoyasema, barabara safi taa za barabarani na vivuko kwa watembea kwa miguu.Street light zikiendelea kuwekwa hii ni Barabara ya makambako to njombe na hizi zimewekwa makambako, njombe,wangingombe,ilembula,na igwachanya
View attachment 2520039
Mji ukiendelea wachawi itabidi wahamie maporini huko.Njombe kumbe nao ni mji natamani kuwekeza huko sema nakwama kwenye uchawi wa wakinga tu
Kila sehemu uchawi upo Cha msingi ni kupambanaNjombe kumbe nao ni mji natamani kuwekeza huko sema nakwama kwenye uchawi wa wakinga tu
Na maambukizi ya HIV ni fursa kiuchumi?Mkoa wa Njombe: Mkoa wa Njombe una Halamashauri 6 ambazo ni Njombe Mjini, Vijijini, Ludewa, Makete, Wangingombe na Makambako.
Wenyeji wa Mkoa wa Njombe 70% ni wabena, ambao wanapatikana Wilaya za Njombe mjini,Vijijini, Makambako, Wangingombe na wakinga-Halamashauri ya Makete na Halamashauri ya Ludewa wapo Wapangwa na wanyasa.
Sifa muhimu za kiuchumi katika Mkoa wa Njombe
Sifa nyingine:
- Ndio Mkoa unaongoza kwa Idadi ndogo ya watu kwa takwimu za awali za sensa ya 2022 Mkoa huo unakadiriwa kuwa na watu 889,946
- Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa Mikoa top 5 iliyo na watu wa vipato vikubwa zaidi kuliko Mikoa mingine.
- Mkoa wa Njombe-Makambako kuna upepo wa kiwango kikubwa ambao unaweza kuzalisha umeme wa megawati zaidi ya 300
- Unaongoza kwa uzalishaji wa mbao-Asilimia 60-70 ya mbao zote zinazotumika Tanzania zinatoka katika huo Mkoa-na zinalimwa karibu Halamashauri zote za Mkoa huo.
- Unaongoza kwa uzalishaji wa zao la viazi mviringo 70% ya viazi vyote Tanzanua vinalimwa huko.
- Unaongoza katika uzalishaji wa zao LA parachihi Tanzania nzima.
- Ndio Mkoa unaongoza kwa madini ya Chuma na Makaa ya mawe. Kwa Tanzania akiba kubwa ya madini hayo yapo Mkoa huo na yanapatikana kule Luganga na Mchuchuma Wilayani Ludema.
N.B. Kama mtu upo interested kuishi mazingira kama ya Ulaya ulaya yenye baridi na green-Mkoa wa Njombe ndio jibu sahihi. Huko Mbu na nzi ni kama hakuna. Maelezo mengine kuhusu investment opportunities katika Mkoa huo tembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
- Unaongoza kwa wafanyabiashara wakubwa Tanzani a.k.a Wakinga
- Ndio Mkoa unaongoza kwa baridi Tanzania nzima hasa Njombe Mjini na Makete
- Mkoa wa Njombe ndio Mkoa pekee kwa kipindi cha miaka 5-10 unaongoza kwenye top 3 ya maambukizi ya HIV
- Mkoa wa Njombe ina Idadi kubwa ya Wanawake kuliko Wanaume kuliko Mikoa yote Tanzania.
![]()
HIV yasukumwa na ujinga, ulevi, umaskini na kutoelimika.Na maambukizi ya HIV ni fursa kiuchumi?
Kila penye mafanikio hapakosi changamoto na hii imetokana na mwamko mkubwa wa upimaji afya wa watu wa njombe na wengine walikuwa wa mikoa ya jirani kutokana na uwepo wa huduma Bora za afya ndani ya mkoa mfano ikonda hospitalNa maambukizi ya HIV ni fursa kiuchumi?
Mkuu, safi sana, naona nimechokoza nyuki waleta mizinga ya maana.