Uchaguzi 2020 Zitto 2015 ulikataa UKAWA, why leo utake Coalition?


NCCR na NLD walinufaika nini kwenye huo UKAWA?

Kwa ubinafsi huu kila chama kisimame kivyake na CCM itaondoka tu haiwezi kutawala milele nchi hii.
 
hata Wassira alishawahi kusema kabla ya mwaka 2015 Chadema itakua imeshakufa.
Wasira aliyasema haya na kubakia maneno matupu, vitendo ikawa hakuna. Kwasabb enzi hizo Kikwete alikuwa ameacha wanasiasa wafanye siasa.

Lkn enzi hii JPM anadeal na chadema kwa vitendo. Amedhamiria kuiua chadema na anatekeleza. Angalia chaguzi ndogo za wabunge Kinondoni, kule Kakonko, Siha, Longido.nk.

Angalia pia uchaguzi wa serikali za mitaa. Fungua macho pia uangalie kwann wabunge wa chadema wanakimbilia ccm. Unatapa wapi ujasiri wa kusema chadema haifi?
 
Mimi sio shabiki wa Membe na sijawahi kumuelewa unaweza kunisoma kwenye thread za nyuma. Lakini kwenye medani za siasa Membe akigombea ACT obviously CDM ndio mtakuwa na wakati mgumu kuliko hata CCM. Ukweli Mchungu huu!
 

kwanza umeanza andiko lako kwa kunihukumu. Polisi wewe, mwendesha mashtaka wewe, Jaji wewe. Sio sawa.

leta uthibitisho kuwa Mimi au ACT Wazalendo ilikataa UKAWA. CHADEMA, kwa sababu zinazoeleweka na wala silaumu, ndio walikataa Ushirika na ACT. Sisi tuliomba kuingia UKAWA tukakataliwa. Tuna ushahidi wa barua tulizoandika kuomba kuingia UKAWA. Tukakataliwa. CHADEMA walitangaza waziwazi kuwa adui yao Mkuu sio CCM bali ni Zitto Kabwe. Hali ya wakati ule niliielewa. Nikasema haijalishi tutakutana mbele ya Safari kwani safari yetu ni moja.
Sasa CHADEMA na ACT tunaelewana, tunafanya kazi pamoja kwa maslahi mapana ya Taifa. CCM wanatumia watu wao kutaka kutugawanya. Mimi binafsi najua hila hizo na sitaingia huo mtego. Nina hakika Kuwa viongozi wa CHADEMA wanajua mtego huu na wao hawatauingia Pia.
Hatuwezi kuwa watumwa wa historia. Ni lazima tuwe na Ushirika ili kupambana na CCM. Sisi ACT tupo tayari na hatutakuwa kikwazo cha Coalition kamwe
 
Si ameshapata somo na yaliyojitokeza 2015,
Ukawa ilikuwa darasa zuri kwa wapinzani na Mwiba kwa CCm.
 
Mleta mada muongo au kumbukumbu zako ndogo sana. 2015 Zitto alikuwa anataka sana kuungana na UKAWA lakini wanachama wote mkamezeshwa sumu kuwaa ACT ni tawi la CCM. Matokeo yake hata pale alipofanikiwa kusimamaisha wagombea ubunge karibu majimbo yote ya Tanzania mkahoji kuwa haiwezekani kwa chama kichanga kusimamisha wagombea nchi nzima bila kuwa na back up ya CCM hivyo 2015 mlimuona ZItto ni CCM na Mbatia ndio upinzani halisi.
Nadhani matokeo mnayaona sasa nani CCM na nani mpinzani. Cha ajabu mnabaki na kauli kuwa ZItto hatabariki au kigeugeu ukiuliza ukigeugeu wake nini utasikia ni msaliti hakuna jibu lingine zaid.
Kila uchwao Zitto anataka muungano uwepo wa upinzani ili kushinda CCM lakini tatizo lipo CHADEMA mnajiona mnaimarika zaidi wakati mnazidi kupotea tu. Na hata katika suala la uchaguzihuu Zitto alishakubali kuungana na CHADEMA na pia Lissu awe mgombea wa urais, lakini CHADEMA mnampuuza. Nakumbuka alishawahi kushambuliwa sana Twitter kuhusu hilo na wale kina Yeriko Nyerere.
Sasa katika mazingira kama hayo mnataka mtu afanye nini? Ataendelea kukipigania chama chake tu nyie mnaozidi kuimarika kila siku endeleeni kuimarika tu.
 
Kwa hiyo tukose wote?
Mbona huzungumzii kura nyingine nyingi kuzipata tokea wana CCM wanao waunga mkono upinzani?
Kama ACT inatafuta uungwaji mkono Bara,wajitathimi upya.
 
Mkuu maneno umeyamaliza,
Nimefarajika kwa maelezo haya ,
Aluta continua,
Wasio taka Umoja wote huwa ni wachawi, wanaipalilia ccm ili kura zigawike na kuipa CCM ushindi laini.
Nakumbuka jimbo la ukonga,Mgombea wa Chadema ambaye nadhani alinunuliwa na CCm wakakomaa kugombea na mgombea wa CUF huku tukiwa tumekubaliana asimameme CUF pekeyake, wakazigawa kura pasu kwa pasu na kumpa CCM upenyo ambao haukustahiki.
Ytosha ,sasa tumejifunza, Tuanze Upya.
 

Haya ni maneno yako ndugu:

Hatuwezi kujiunga na UKAWA kwa kuwa CCM na vyama vingine hawana tofauti kwa sera, lakini ACT ni tofauti kwa kuwa inaheshimu miiko ya uongozi na kubwa zaidi chama chetu kinaongozwa na azimio la Tabora,”
 

Mlikataliwa kwa sababu mlikuwa Wabinafsi. Na ndiyo maana Chadema waliwaona nyie ni adui namba moja. Mwaka 2019 ndipo uliporuhisiwa kujiunga na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni baada ya kuanza kujiandaa kwa Movie hii tunayoiona sasa, na kumbuka wakati Mbatia akielezea kuruhusiwa kwako alisema sasa utapaswa kufuata taratibu zao tofauti na awali ambapo ulikuwa ujafanya kama unavyotaka. Na mostly ulitusaliti wapinzani wenzako kwenye movements kibao Bungeni. Chonde Chonde CHADEMA msiingie mtego huu mtanasa vibaya sana.
 
Ny
Nyie ndio mnaorudisha nyuma upinzain Tanzania. Sasa huyo Mbatia mliekubaliana nae yupo wapi sasa?CCM itaendelea kutawala kwa sababu ya wajinga kama nyinyi mnashindwa kuendana na wakati mmekuwa watumwa wa historia.
Mngeweza kuitumia combination ya Lissu na Zitto Kabwe hakika CCM ingepata wakati mgumu sana lakini kwa ujinga wenu bado mmelala tu mkiamini adui namba moja ni Zitto. Amkeni
 
Mimi sio shabiki wa Membe na sijawahi kumuelewa unaweza kunisoma kwenye thread za nyuma. Lakini kwenye medani za siasa Membe akigombea ACT obviously CDM ndio mtakuwa na wakati mgumu kuliko hata CCM. Ukweli Mchungu huu!
I wish huyo Membe agombee kupitia ACT halafu CDM wamuweke Lissu upate majibu yako, unaonekana huijui nguvu ya Lissu, huyo Membe labda kama angekuwa anagombea umoja wa mataifa ndio anafahamika.
 

Wew naona 2015 ulikuwa chekechea na hivyo hujui politics zilivyokuwa 2015. Zitto hakukataa UKAWA, ni kwamba hakukaribishwa. Alitamka mara kwa mara kwamba anataka kujiunga lakini kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi hakukaribishwa.
 
Wew naona 2015 ulikuwa chekechea na hivyo hujui politics zilivyokuwa 2015. Zitto hakukataa UKAWA, ni kwamba hakukaribishwa. Alitamka mara kwa mara kwamba anataka kujiunga lakini kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi hakukaribishwa.
Na hakukaribishwa kwa sababu alikuwa haaminiki, ni wajibu wake sasa kuthibitisha kwa vitendo imani kwa waliokuwa na shaka nae.
 
We jamaa nimjinga sana, kwenye thread yako unasema alikataa kujiunga na ukawa, hapa una comment kuwa alikataliwa, sasa sisi wapenda mageuzi tukuelewe vipi?. Kama una agenda za ccm tunaomba uziache , Zitto alisema kabisa yuko tayari kwa ushirikianoo hata mgombea akiwa Lisu sasa tatizo lake liko wapi?.

Unajua watu wengine wenye mawazo kama yako niwajinga sana, hebu jichukulie wewe ni Zitto na upo katika nafasi aliyopo utaacha kujenga chama kisa utaonekana unatumiwa na ccm?.

Sisi tunachohitaji ACT & CDM washirikiane ili wagawe majimbo Kisha uraisi asimame Lisu tutawapigia Kura, Sasa kwa bahati mbaya wote hatuna uhakika kama Lisu atarejee kulingana na mazingira yaliyopo. Kwahio lazima vyama vyote iwe CDM au ACT kila chama kiendelee na mipango yake mpaka pale ushirikiano viongozi watakaporidhia uwepo. Huwezi kuacha kukiaandaa chama na uchaguzi kisa unasubiri kesho ambayo huifaham.
 
Wanasiasa wote ni wabinafsi.

Kipindi cha Ukawa, ilikuwabaliwa kwamba wagawane majimbo, kilichotokea, CDM ilisimamisha wagombea kwenye majimbo yaliyokuwa yamekubaliwa kuwa ya vyama washirika.

Nina uhakika, kama Membe angekuwa anaenda CDM, huu muungano ungepita, ila kwa sababu anaenda ACT, it's not happening.

Acha wagawane kura, CCM aendelee kuongoza.

Magufuli ameamua kwa nguvu zake kuiua CDM, CDM hawaamini mpaka pale watakapo chemsha kupata wabunge, si kwa uchache wa kura, bali kwa nguvu ya dola.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…