Zitto aanika siri nyeti za Mbowe! Adai hatakufa kama Chacha Wangwe

Kitwange

Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
47
Reaction score
48
Wakuu, inasemekana Zitto Kabwe ali-post facebook hii kitu halafu aka-edit later.

1736169401058.jpeg

Original post:

"Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. NaaminiMkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini.

Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa.

Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative party?

Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda. Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas.

They must know I am not a push over. Chacha died, I won't. Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu kidole kuhusu maadili."

Revised Post:

Nukuu:

Wakili Tundu Lissu amenituhumu kuwa nimehongwa magari 2 na mheshimiwa Nimrod Mkono. Mimi ninamiliki gari moja mbili, freelnder ninayotumia Dar Es Salaam na Toyota Carina ninayotumia jimboni. Tuhuma hii haimo katika tuhuma nilizotuhumiwa nazo na kuandikiwa na chama ili kujibu.

Kama Tundu lissu anadhani tuhuma hii ana ushahidi nayo wa kutosha aiongeze kwenye tuhuma walizoniandikia ili niweze kujitetea kwenye vikao, vinginevyo ni mipasho tu. Nawapa changamoto Tundu lissu na wenzake kama wana tuhuma Mpya dhidi yangu waniandikie kwa mujibu wa taratibu. Tuhuma nilizo nazo hivi sasa na ambazo nimezikatia rufaa katika Baraza Kuu zinahusu mkakati wa kugombea uenyekiti Taifa na kutaka mahesabu ya chama yakaguliwe na CAG.

Kutoka Gazeti la Raia Tanzania

Zitto aanika siri nyeti za Mbowe

- Mbowe asema ni utoto tu


CHALILA KIBUDA NA MARY VICTOR

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ameshusha tuhuma nzito dhidi ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, zikimhusisha na ufisadi.

Hata hivyo, Mbowe naye amejibu tuhuma hizo akisema ni busara zaidi kwa mhusika kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake badala ya kuibua tuhuma nyingine.

Madai hayo ya Zitto kwa Mbowe ni kilele cha siasa za kuchafuana, kutukanana na kuvunjiana heshima kilichodumu kwa takribani miezi mitatu sasa kupitia vyombo tofauti vya habari.

Akiandika katika ukurasa wake binafsi wa facebook jana jioni, Zitto alisema Mbowe hawezi kumnyooshea yeye kidole kuhusu masuala ya maadili kwa vile yeye mwenyewe (Freeman) ndiye mvunja maadili namba moja ndani ya chama hicho.

Jana mchana, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwamba Zitto amepewa magari mawili na Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono; ambaye ni mmoja wa watu waliotajwa na chama hicho kama mafisadi.

"Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Mbowe Sh. milioni 40 ili Mbowe asifanye kampeni Jimbo la Musoma Vijijini.

Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman Sh. milioni 20 za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa.

Nadhani alimwambia pia kuwa mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe Sh. milioni 200 za Kampeni ya Slaa. Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe Sh. milioni 100 za kampeni. Lissu anajua....?

Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda.


Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu. Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas.

They must know I am not a push over (Ni lazima wafahamu kwamba mimi si mtu wanayeweza kumchezea wanavyotaka). Chacha (Wangwe) died, I won't (Chacha Wangwe alikufa, Mimi Hawaniwezi.


Mtu ambaye hawezi kuheshimu ...... hawezi kunyooshea mtu kidole kuhusu maadili," aliandika Zitto katika ukurasa wake wa facebook baada ya Tundu kutoa tuhuma zake.

Lissu alikuwa akizungumza katika mkutano ambao Chadema ilitangaza kuwafuta uanachama wanachama wake wawili; Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.

Zaidi ya kuwafukuza akina Kitila, chama hicho jana kimewaagiza viongozi na wanachama wake kutoshirikiana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia chama hicho, Zitto Kabwe.

Zitto alifungua kesi wiki iliyopita akitaka kamati hiyo isijadili uanachama wake, lakini hatua hiyo ya kamati kuu kuwaagiza viongozi wake wasishirikiane na Kabwe kwenye masuala ya Chadema, imetafsiriwa kama kumfanya si mwanachama.

Mwanasheria wa Zitto, Albert Msando, ameliambia gazeti hili jana kwamba ilichofanya Kamati Kuu (CC) kwenye kikao hicho kuhusu Zitto ni kuingilia uhuru wa mahakama kwa vile tayari wameshampa adhabu wakati Mahakama inasikiliza shauri lake.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, alisema wamechukua hatua hiyo kwa sababu wamebaini Kitila na wenzake walikuwa na lengo la kubomoa Chadema.

Viongozi hawa walikuwa wameandaa mkakati wa muda mrefu wa kukibomoa chama kwa kukichafua kwa wananchi na kuwachafua viongozi wa juu kwa kutumia tuhuma za uongo za ufisadi, alisema Slaa.

Slaa alikuwa akizungumzia waraka wa siri ulioandaliwa na Kitila na Mwigamba uliotaka kufanyika kwa mabadiliko katika ngazi ya juu ya uongozi wa chama hicho.

Majibu ya Mbowe

Akizungumza na mwandishi wetu Mbowe alisema ni utoto kukwepa kujibu hoja kwa kuanzisha tuhuma dhidi ya mtu mwingine ambazo si za kweli.

Mimi nimekuwa nikisimamia ukweli, mtu anapotuhumiwa ni lazima ajibu tuhuma hizo. Ni utoto kuacha kujibu tuhuma na kuzusha tuhuma nyingine. Anapaswa kufanya utetezi wa tuhuma zinazoelekezwa kwake.

Mimi ni mbunge, bungeni nimekuwa nikichangia watu mbalimbali mimi kama Freeman, si ajabu watu wengine kunichangia. Hapa jambo la msingi ni kwamba unapewa pesa kwa sababu gani, kwa nia ipi? Kupewa pesa na Kikwete au CCM si tatizo lakini unapewa pesa kwa sababu zipi, kwa malengo gani? alihoji Mbowe.

Mbowe alilaumu baadhi ya vyombo vya habari kushiriki kumchafua kwa taarifa za kutunga kutoka kwa watu anaodhani wamekuwa na uhusiano na Zitto.
 
Haha haha technically na yeye amechukua magari mawili haha big show ccm ni whatsup sana...huenda dogo naye kataka uenyekiti apige haha uzalendo ma s a bu ri yao!
 
Funguka ZZK,funguka,ndio usaliti wako unapoonekana,mbona hayo yote hukuwahi kuyasema?Kwa hiyo mafisadi kama wako CDM unawafumbia macho,mnafiki mkubwa,yako wapi ulivyokuwa unajipambanua unapiga vita rushwa,kumbe umewafuga ndani ya chama;unasubiri wanamwaga mboga unamwaga ugali!!Unajidhalilisha tu Zito,its better u shut up!!Kumbe kweli --------- kwa kuwa wakubwa zako ----------,utateteaje tena mali za Umma Zito kama sio unafiki?!
 
Kwa tuhuma hizi nzito alizozitoa mh. Zitto Kabwe dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema mh. Freeman Eikaeli Mbowe, Chadema inabidi ijibu coz its very serious na wakikaa kimya ina maana yanayosemwa na mh. Zitto dhidi ya mh. Mbowe ni ya kweli...basi Chadema haitakuwa na locus standi ya kunyooshea watu kwa tuhuma za ufisadi na michezo michafu...tunamtaka mh. Mbowe atoke kukanusha au tuziamini.
 
Naona sasa ni hadithi za "ukimwaga ugali,mi namwaga mboga"!

Niliwahi sema na leo narudia "ukifuatilia sana siasa na wanasiasa wa Tanzania,unaweza kuwa mwehu"

Anyway,tutafuka tu japo kwa ghrama kubwa za mali,fedha na maisha ya watu.
 
Mkuki kwa nguruwe sio??

Mwenyekiti CHADEMA anatia aibu,aje akanushe tuhuma zake sasa na yeye

Tundu lisu anacheza ngoma ambayo haijui,wanamtanguliza tu kichwa kichwa yeye hajui kama anajidhalilisha!

Ni ujinga mtu mwenye elimu kama ya tundu kupelekwa pelekwa na kujazwa uongo na mbowe...

Mbowe atoke atuachie chama chetu alishashindwa kabla hajaanza

Na Dr Slaa ajiangalie naona anapotea taratibu
 
Mtanzania mwenzangu Zitto Kabwe, umekuwa very reactive. Be cautious and control your emotions. Unaanza kuexpose your weakest side.

Unarejea matukio ya 2005 leo 2014, ulikuwa wapi? Unatuaminisha umenyamazia mangapi ktk taifa hili? On every action theres equal and opposite reaction. DID U?

WAMEMWAGA UGALI? Unamwaga mboga wakati wenzio weshashiba??!!
 
Pole sn kaka'angu!
Ila mwisho wa yote tutajua ukweli ni upi!
Kuna manyongoloto mengi sn nao pia wanayo lkn hawasemani,
VUTA SUBIRA. Just a matter of time!!!
 
Zitto hajajibu mashtaka kwake kuhusu magari aliyopewa na Mkono. Two wrongs do not make a right.

Kabla ya ku deflect mashtaka kwa kuibua uozo wa mpinzani wako, jibu mashtaka kukuhusu wewe. Hata kama ni kwa kukubali tu.This deflection is one of the oldest tricks in the playbook.

Kwa wazoefu wa habari hizi, usipojibu tuhuma maana yake umekubali ni kweli. Kwa hiyo Zitto kakubali kwamba ni kweli kapewa magari na mkono, lakini anasema wanaomtuhumu nao wana yao kama hayo.

Hili saga linathibitisha yale niliyokuwa naandika hapa kitambo.

Hakuna Zitto wala uongozi wa CHADEMA, wote ni wale wale tu.
 
AMA KWELI FADHILI MBUZI UTAMLA NYAMA.............

Nampa pole sana Mh Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chadema Taifa kwa kutukanwa na kukosewa adabu na kijana mdogo, Msaliti Zitto Kabwe, ambaye leo mafanikio yake yametokana na yeye Mh Mbowe, lakini kasahau na kaamua kukutuna ati wewe ndo kamati kuu!

vile vile nimpe pole Mh Tundu Lissu Mbunge wa Singida mashariki na Mwanasheria wa chama, kwa kuitwa Kifaranga na huyu kijana ----- asiye na Adabu, we mpuuuze kwani leo amewadhihirishia watanzania kuwa hafai hata kuwa Balozi wa nyumba kumi......

Zitto Z Kabwe mpaka sasa hujakanusha tuhuma za kweli kabisa kwamba ulihongwa Magari mawili na Mh mkono iliusimsimamishe mgombea Msoma Vijijini, badala yake uliishia kujitoa ufahamu na kuwatukana Viongozi mtandaoni kuonyesha ulivyofilisika mawazo kama si kufilisika hoja!

Zitto Kabwe amejitoa ufahamu na kudai eti mtu asiyemuheshimu mke wake aliyewazalia watoto wake hawezi kumfundisha mtu maadili.......
Zitto, kabla ujanyoosha kidole kwa mwenzako embu jaribu kujitazama wewe mpaka leo una umri miaka 37 umeshindwa kuoa, na kinacho kusumbua ni uzinzi, embu kumbuka April tukio la aibu ulilolifanya pale Mount Meru Arusha, baada ya kunywa KONYAGI, mbona sisi hatusemi..........

Si jambo jema kujadili misha ya Binafsi ya Kiongozi, kwani hakuna aliye mkamilifu Chini ya Jua.......

SI VEMA MAAMUZI YA KAMATI KUU KUMBEBESHA MH MBOWE NA LISSU PEKE YAO..
 
Naona pamoja na wajumbe kufungwa macho na fisadi Mbowe, sasa nadhani watafunguka na kumjadili kwa pesa ambazo amekuwa akipokea toka CCM, pia Dr. Slaa ambaye hata kadi ya CCM hajarudisha.

Tulishasema hawa ndo wasaliti wana wasingizia wengine, mengi tu yatakuja hapa. Hivi inakuwaje unamwomba Baba yako akupe hela umpelekee Mama yako halafu unamwambia Mama nakukopesha pesa hii na kweli Mama yako bila kujua anatafuta huku na kule anakulipa.

Jamani Mbowe uwe na hofu ya Mungu, utakufa vibaya sana. Pesa za Mkono kapewa yeye anakuja kuwakopesha CHADEMA, kwani alipewa zake binafsi au alipewa za Chama?

Hivi hiki chama kina akaunti kweli au inatumika ya Mbowe?
 
Back
Top Bottom