Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alikuwa wapi siku zote.
Its toooooooooo late...
Kwa hiyo mtu akikutuhumu tu bila kutoa ushahidi basi mtu ajiuzuru tu,basi hii itakuwa nchi ya wajinga!Kama ni kweli kuwa amepokea fedha zaidi ya mamilioni kutoka kwa vyanzo tata nje ya chama na utaratibu ulio wazi wa kukusanya fedha za kampeni...
Ili kulinda heshima yako, ya chama, kujenga imani ya watanzania walioko nyuma yenu, unatakiwa kujiuzulu uenyekiti wa chadema mapema.
Hili nalo likipita bila kulipa uzito ile kauli ya chadema kua chama cha kibabaishaji itasimama.
mkuu jamii inataka nini na wewe unasema nini hapa, ni sahihi kutumia fedha chafu katika jambo halali??? mpaka hapo credibility ya mwenyekiti ipo hoiTuhuma kuwa Mbowe alipewa pesa na zikatumika kwenye kampeni za chama, tarime (ubunge) na kwa Dr Slaa (uraisi), sioni kama ni tatizo. Tena tulitakiwa kumsifu Mbowe kama strategic CEO anayeweza kusolicit funds kufanikisha malengo ya organisation. Hii ni kwa sababu hapa hakupewa kama Mbowe, bali CHADEMA. Nadhani tuhuma za Zitto zingekuwa na mashiko kama angesema kama Mbowe alishapewa pesa kwa ajili ya kusaliti chama kama ilivyo kwa Zitto aliyepewa magari ili auze jimbo. After all Zitto kama mtu aliyekuwa naibu katibu mkuu tutamshangaa kwa kukosa collective responsibility na bado akajipambanua kama kiongozi anayefaa kuaminiwa. Mbona hajalalamikia pesa ambazo CHADEMA ilishawahi kupewa na Sabodo ambaye naye ni mwanaCCM? Zitto asitutoe kwenye reli, ajibu hoja, " je alihongwa na akauza majimbo ya uchaguzi kwa CCM? Full stop.
Pili, inawezekanaje sasa hivi Zitto anataka tumuamini kwa asemayo, ili hali maneno yake yamekuwa yakibadilika siku hadi siku. Ikumbukwe, ni Zitto huyu huyu aliyesema kwenye press conference kuwa alijiondoa kuwa signatory wa chama tangu mwaka 2010, ilhali kumbe hajawahi hata kuwa. Pili ni Zitto huyu huyu aliyejipambanua kuwa ana majina ya watu walioficha fedha Uswisi, na hadi leo kushindwa kuyatoa, na badala yake kuishia kuapa kuwa hana. Tatu, ni Zitto huyu huyu aliyetudanganya kuhusu mshahara wa waziri mkuu. Nne ni Zitto huyu huyu kwenye moja ya maandiko yake amewahi kusema ana magari matano, lakini jana kasema anayo mawili. Sasa tutamwaminije. je huoni kuwa kama ilivyo kawaida yake anataka kudivert attention yetu? Uongo wake unaweza kuorozeshwa kwa listi ndefu sana.
Zitto si msafi tena na hasafishiki. Period
Zitto hajajibu mashtaka kwake kuhusu magari aliyopewa na Mkono. Two wrongs do not make a right.
Kabla ya ku deflect mashtaka kwa kuibua uozo wa mpinzani wako, jibu mashtaka kukuhusu wewe. Hata kama ni kwa kukubali tu.This deflection is one of the oldest tricks in the playbook.
Kwa wazoefu wa habari hizi, usipojibu tuhuma maana yake umekubali ni kweli. Kwa hiyo Zitto kakubali kwamba ni kweli kapewa magari na mkono, lakini anasema wanaomtuhumu nao wana yao kama hayo.
Hili saga linathibitisha yale niliyokuwa naandika hapa kitambo.
Hakuna Zitto wala uongozi wa CHADEMA, wote ni wale wale tu.
Wewe ni nani hasa hata umuamuru Mbowe kujiuzuru..!!?
kwa maelezo ya mbowe hapo mwiso katika gazeti la raia mwema ina maana kakubali ni mpiga dili..
Mkuu acha kutumia lugha usiyoijua tafadhali
Kamanda! Kama suala la kutokuwa na mke mbona Chadema viongozi wake hawajawahi kufunga ndoa? labda tufahamishe lini John Mnyika alifunga ndoa? Lini Dr.Slaa alifunga ndoa? Acheni siasa za makengeza.
kwa maelezo ya mbowe hapo mwiso katika gazeti la raia mwema ina maana kakubali ni mpiga dili..