ZZK anatapatapa kama mfa maji, badala ya kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake anaibua tuhuma za kutunga dhidi ya mbowe? Aondoke tu aende CCM badala ya kuipotezea muda mahakama. Hivi anadhani kwamba atang'ang'ania CHADEMA mpaka lini. Hizo tuhuma ilipaswa aziseme siku anajiunga CCM au baada ya kufika CCM. Kutamka hayo anayosema leo huku akiwa anang'ang'ania kubaki CHADEMA kwa nguvu za mahakama, ni utoto.
 
Siasa zenye mafanikio ni siasa zisizo na tamaa wala kuzulumiana na wala kugeukana kwa sababu ya Pesa.

Angalieni sana wana Siasa wanaookotwa kwa Pesa wanatushangaza kama wanakuja na tamaa namna hii si watakuwa akina kibwetere wengine.

Zito nadhani kuna mahali umekosea na japo sina uhakika kama mimi mtu wa mbali kabisa, jutia tu kwa upande wako na angalie njia sahihi zaidi yenye mwanga kwa sasa. hata kama Kina Mbowe wana matatizo, is too late kuanika sasa maana unatoa tuhuma wakati tayari zako zipo juu. hata kama una ukweli ndani yake, basi jua kwa sasa unasomeka kama mfa maji.

Very sorry, i am Chadema ila naangalia upepo mwisho wake...
 
Haha haha technically na yeye amechukua magari mawili haha big show ccm ni whatsup sana...huenda dogo naye kataka uenyekiti apige haha uzalendo ma s a bu ri yao!

unafiki mtupu,chacha wangwe kafa leo,iweje hilo liseme leo baada ya kuvuliwa madaraka.Kweli zitto ni ndumilakuwili anaangalia.maslahi yke
 
tundu lisu ni kifaranga tu...
kwa lugha nyingine zito haongei na mbwa, anaongea na mwenye mbwa!!
Hiyo kumwita kifaranga ni kuonyesha hishima yake kwa CDM...Otherwise angesema mengine!
 
Wana JF

Hali ya kisiasa kwa Mh ZZK itakuwa mbaya zaidi kwa mujibu wa rafiki yangu mmoja wa Lumumba. Wanadai kuwa habari za kupokea rushwa ya magari kwa mheshimiwa zzk hachomoki kutokana na vielelezo mpaka vya picha vipo. Kwa mujibu wa mtoa habari wangu inawezekana ushaidi huu ilivujishwa kwa Lisu na mtu ambaye wanasema ni rafiki wa karibu wa ZZK waliyemtaja kwa jina moja Habib kupitia kwa Mtendaji mmoja mkubwa wa Serikali wa wizara moja nyeti ambaye ndiye aliyemkabidhi Lisu kwa ajili ya kumaliza ZZK. Inasemekana kuwa Lusi amepatiwa na Mtendaji huyo wa wizara nondo ambazo atakuwa anazishusha moja baada ya nyingine kulingana na jinsi zzk atakavyokuwa anajitetea. Mtoa habari anasema jamaa aliingia king muda mrefu na jamaa wamejipanga na wameanza na kakombora kadogo. Inasemekana jamaa wamemshauri ZZK asijaribu kupambana na Lisu ila yeye mara zote apeleke mashambulizi kwa Mbowe. Wamemwambia ati Lisu ni hatari sana kushindananaye, pia inasemekena ameshauriwa asikanyage tena JF kuzungumzia chochote aishie huko facebook.
 
mbowe ni mwizi tu,
tena wizi ameanzia bot.

Angalia hata midomo yake imekaa kilaghai laghai tu.

Nawashangaa huu ujasiri wa kuwafukuza wenzie kwenye chama
anaupata wapi.

kwa sasa endeleeni kulipuka tu, itafika siku ukweli utakuwa wazi. Iweje leo ndo mseme kuna fedha zilitolewa kinyemela na rostam and ki "hand" au nanyi ndo mmevurugwa?
 
Tuhuma tuhuma tuu mbowe na machadema wezi mafisadi
 
Mnakula Pesa za Pembe za Ndovu kutoka china :A S 112:
 
uhusiano wa hoja unaoitoa na hoja ya machali ipo wap?

Ungejibu kwanza kuliko kuuliza swali ungeona nini Nataka kusema!

Naamini kua Mimi na wewe Hatuwezi kua na mawazo au mitazamo sawa! Na ndio maana mtu anakua madarakani kwa vipindi ili kuwapisha Na wengine!

Kwa hoja ya Machali Km swala la uongozi ndio shida hapo lazima kuangalia Hayo mambo kwa kina na kwa pande zote mbili! Siasa na vyama vya Siasa na mashindano ya kisiasa ni vita! Kuna mbinu nyingi tu zinatumika za maendeleo ya chama au kuua chama! Au wanasiasa kujikuza kisiasa!

Mbowe ni mtu Wa kujenga chama kitu ambacho wapinzani wake wasingependa kuona anaendelea kuongoza! Tunaona maendeleo aliyofanya ktk chama!

Siwezi mzungumzia sn ZZK lkn kwa uchache Ni mtu aliejijenga yeye binafsi!

Kwakua kamwe watu Hawawezi kulingana mawazo na mitazamo hapo ndipo unapata tofauti za Hawa watu!
Mtu anataka madaraka kwa ajili ya kuua chama na mtu anataka kubaki madarakani kwaajili ya kujenga chama! Hiyo ndio shida!

Mh Machali angeliangalia na hili swala sio kusema jujuu tu!
 
Hii ndo akili ya yeyote atakaye hamia CCM!

Inasikitisha sana!
 
Unaaminisha Kura ndio kula?
Nakushauri karudi upya ukajifunze kufanya propaganda na sio kuja kuropokaropoka mitandaoni kama hivi.

Wewe ni mwanaCCM lakini kutwa unakesha kufuatilia issue za CHADEMA, Is that your priority?
 
Kuna vijana wa chadema maalumu wa kumtetea M/Kiti Mbowe hapa JF,
Naomba waje kutuelekeza hili likoje.....na kama ni sahihi m/kiti kuvuta mpunga kwa ccm.
 
Siku hizi hata kusikia neno chadma sitaki kabisa chama cha hovyo kabisa.
 

Ongeza na dr slaa nae alikula milioni 200 alizopewa Mbowe na Nimrod Mkono!
Leo Mbowe kajibu eti yeye alichukua hizo hela sio kwa lengo la kusaliti chama!
 
Ukiangalia kwa undani kabisa hii sinema, na ukaa cha ushabiki utagudua hatuna demokrasia na UPINZANI WA KWELI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…