Wana JF
Hali ya kisiasa kwa Mh ZZK itakuwa mbaya zaidi kwa mujibu wa rafiki yangu mmoja wa Lumumba. Wanadai kuwa habari za kupokea rushwa ya magari kwa mheshimiwa zzk hachomoki kutokana na vielelezo mpaka vya picha vipo. Kwa mujibu wa mtoa habari wangu inawezekana ushaidi huu ilivujishwa kwa Lisu na mtu ambaye wanasema ni rafiki wa karibu wa ZZK waliyemtaja kwa jina moja Habib kupitia kwa Mtendaji mmoja mkubwa wa Serikali wa wizara moja nyeti ambaye ndiye aliyemkabidhi Lisu kwa ajili ya kumaliza ZZK. Inasemekana kuwa Lusi amepatiwa na Mtendaji huyo wa wizara nondo ambazo atakuwa anazishusha moja baada ya nyingine kulingana na jinsi zzk atakavyokuwa anajitetea. Mtoa habari anasema jamaa aliingia king muda mrefu na jamaa wamejipanga na wameanza na kakombora kadogo. Inasemekana jamaa wamemshauri ZZK asijaribu kupambana na Lisu ila yeye mara zote apeleke mashambulizi kwa Mbowe. Wamemwambia ati Lisu ni hatari sana kushindananaye, pia inasemekena ameshauriwa asikanyage tena JF kuzungumzia chochote aishie huko facebook.