....Ni heri Mbowe angeishia kuhongwa tu lakini hili la kuiba pesa za chama ndio baya zaidi,kamata mwizi!!....

Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa.

. Lissu anajua
kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative party?
 
mbowe kapewa pesa zisaidie uchaguzi
zitto kapewa pesa za kuvuruga chama

...Hivi unajua kusoma kijana?kwa Mbowe Chadema ni biashara...

Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa.

. Lissu anajua
kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative party?

Kwa wasiojua:Gazeti la Tanzania Daima ni gazeti binafsi la Mbowe ambalo Mbowe kalianzisha kwa pesa zilizotolewa na Wafadhiri kwa Chadema,hiki ni kiwango cha juu cha ufisadi.
 
Mbowe kama mme kamsaliti mkewe mpaka kufikia kuzaa na mbunge wa viti maalum,atashindwa kuwasaliti watu wa kuja tu?
 

Kinacho msumbua zitto niwivu wakike wamali za Mbowe pamoja nakuonga bado hawezi kumfikia kinacho mpoteza zaidi anajua Mbowe kapatia pesa kwenye siasa bila kujua kuna pesa za hasili.
 

MKuu haya ni ya kweli kabisa yametokea. inabidi mwenyekiti nae ajiuzuru nafasi yake. niaamini kuna wabunge wengine ndani ya chama walikiwa wanajua lakini wanaogopa kufukuzwa, bt dogo amemwaga unga na mboga naamini wengine watafuata nyayo za zito hawataogopa kufukuzwa wameshatiwa ujasili wa kusema hadharani maovu ya chama, nafikiri huo ndo ukomavu wa chama.
 
Afadhali unavyoendelea kuganga njaa huko kwa maccm,inasemekena wewe ni mwalimu kwa taaluma(sina hakika)wanafunzi wako ungewafundisha ujinga tu, mungu kaepusha hayo.
 

Daaa, hata kama ccm waliwachukua ili mkawe mtaji wa kuiua cdm itabidi wajiulize mara 2mbili. Maana kama ndio nguvu ya kijana anayejiita msomo iliyoongezeka ccm basi hakuna ya kupeleka vijana vyuo vikuu. Mwampamba kwa elimu yako wangalau ungeweza kutengeneza mchanganuo mdogo wa kijana anavyoweza kuwa mjasiliamali na. Yungeheshimika sana tu. Yetu macho na masikio
 
Wakati tukisubiri CHADEMA "wajifafanue" kuhusu mtafaruku huu ambao, bila shaka kabisa, umeharibu sana taswira ya chama, Serikali nayo iwe makini. Siku zote tumekuwa tukiamini marehemu Chacha Wange alifariki katika ajali ya kawaida, lakini kwa kauli iliyotoka kwa Mh. ZZK, basi vyombo vya Dola viifanyie kazi. Kwa kuanzia ZZK na Mbowe wahojiwe kikamilifu hadi tuondolewe shaka kabisa kuhusu kifo hicho.

Ni unafiki mkubwa kwa Watanzania kujidai tunajenga taifa la amani huku idadi ya misiba isiyoeleweka au kuelezeka ikizidi kuongezeka. Inawezekana wanasiasa wananufaika kwa kuacha mashaka katika mambo muhimu lakini sisi ni binadamu kwanza kabla hatujajumuika katika jamii zetu mbalimbali ziwe za kiukoo, kikabila, kidini, kisiasa, n.k. CHADEMA inaweza kujiadhiri kiasi chochote na hata kufa ikitaka, lakini haikubaliki katika "michezo ya kisiasa" maisha ya binadamu nayo yachezewe kiasi hiki - hata kama ni kwa kauli za kizushi tu; lazima watu wawajibike. Kama aliuawa, wauaji wachukuliwe hatua; kama ni uzushi, mpayukaji naye achukuliwe hatua. Hiki sio kitu cha kujinasibu nacho.
 
Siyo mwepesi kwa ajili ya uchawi na ushirikina anaotambia Eti 'panya hatasalia nyumbani kwao wabaya wake' ngoja tumsikie Dr au Lissu akiumia kwa uchafu anaojivunia huyu kijana!!
We nawe si twaongea ya mbolea waleta stor za uchawi,ukiuona uchawi utaujua wewe?piga mbege acha porojo
 

Hiifilamu tamu sana. Hebu waendelee tujue nyeupe na nyeusi. Ila naona CCM tusiyoitaka ikatud madarakan kwa nguvu zaid ya 2010. Kama felix mrema akisimama arusha na yule jaa aliyekuwa TFF akasimamishwa iringa, basi mayokeo ni asubuhi tuu makamanda watapotea
 
Huyo zito ni mnafiki na hana ujasiri ,alikua wapi siku zote.yeye ni mzungumzaji mzuri,kwanini hakuzungumza kipindi hicho yalipotokea.

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Mahakamani ni sehemu ya haki siyo kulia mbona lema na lisu wameenda mahakamani mara kibao acha gongo zako.
Hahaaaaaa! Kwani lema na lisu ndio uliwaambia hawatishwiii!! Bhaahaaaaaaaaaa! Jibu hoja hapa kima wewe sio kuish kwa kutegemea mifano ya lema na lisu, wewe si ----------- kumtetea huyo hasid mwenzio jibu hoja kibaka wewe si mbwembwe hapa,
 
Sasa kama mwenyekiti wa chama anahongwa pesa hiki chama vipi siku akipata urais siatahongwa auze nchi yetu.
 
Wassira aliwambia mkabisha kilo wapi,
Mmekufa mioyoni mwa watu.

Aliyekufa mioyoni mwa watu ni ZZK kama unabisha mwambie arudi kigoma akaitishe mikutano mingine,sijui itakuwa kwa mwavuli upi?kwi kwi kwi kwii.
 
hahahahahahahahaha
Naona vijana wa mbowe hawaamini macho yao.
 
Nafurahi sana pale ambapo watu wenye akili wanasoma mambo yanayo andikwa humu jf na kuyatafakari. Mtu ukitafakari saana mambo ya humu jf utaona kuwa wengi huenda kwa mihemko zaidi ya halisia.
Mh. Zitto Kabwe, umetuhumiwa na CC ya CDM. Unaacha kujitetea hizo tuhuma ulizo vikwa, unatoka kabisa kwenye somo unaenda kuleta mambo ya mwaka 47!!!Muda wote weye ulikuwa kimyaa. Hasira ni M/kiti wako kamtuma Lisu akuseme. Mjibu basi huyo Lisu. Unapomwacha Lisu ukaleta issue ya Mbowe tena ambayo usingaliisema inaonesha kuwa moyo wako haupo sawa na Mbowe.
Mambo ya kifamilia ya Mh. Mbowe yanahusu nini hongo ulizopokea weye kutoka kwa Mkono? ZZK jibu tu tuhuma zako, tena sio kwenye fb bali fuata the right channel na utajibiwa tu. Kila hatua unayochukua ni hatua mbovu zaidi. Kama ungeandika barua yako ya kujitetea kwa CC na ukaomba msamaha kwa tuhuma hizo, ukaeleza kuwa litakuwa pigo kubwa kwa Wananchi wa Kigoma Kask. wewe kuupoteza ubunge wako, hapo sasa, hata sisi tungeweza kuomba msamaha pamoja na weye kwa CC.
Tungesema umeliona kosa hivyo kurudia hapana na kwamba CC lazima nao wakuamini. Hayo hutaki kwa sababu ulihakikishiwa na hao waliokutuma ambao hujakanusha mpaka sasa. Wao walikuhakikishia kuwa watakuweka CDM kama mwanachama wa Mahakama na ndicho wanakazania kufanya. Sawa, kabisa lakini nadhani CCM ndiyo watalia zaidi siku si nyingi. This is going to be a reference in every court proceedings to come of which am quite sure they will be many from ccm soon and very soon.
Mzanzibari walie mrimua mbona hakwenda mahakamani? Kiburi mnachopewa na hilo lichama kitawaharibu tu. Ungeshuka ukaonwa na umma ndipo ungekaa juu siku zote wala si kwa hizi fitna zako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…